EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,708
- 35,719
Urusi na Ukraine: Milipuko na moto mkubwa vinaripotiwa katika jimbo la Odessa
Suspilne OdessaCopyright: Suspilne Odessa
Katika Odesa kuna moshi mkubwa unaopaa angani, kulingana na vyombo vya habari, roketi mbili zilipiga mji huo mapema leo asubuhi.
Mashambulio katika Odessa yamethibitishwa na msemaji wautawa wa jeshi jimboi humo, Sergei Bratchuk, na mwakaili wa operesheni za kijeshi za "Kusini"
Waokoaji wako katika eneo la tukio la moto. Hakuna taarifa rasmi kuhusu majeruhi kwa sasa.
"Kulikuwa na mashambulio katika ghala la biashara na viwanda, kulikuwa na moto mkubwa. Namshukuru Mungu hakuna majeruhi.
Na kuna kitu muhimu hapa nilishotaka kusema asubuhi hii: walinzi wa ghala walifuata kanuni za mienendo wakati wa uvamizi wa anga, na hililimeyaokoa maisha yao," alisema Bratchuk.