neo1
JF-Expert Member
- Sep 1, 2013
- 576
- 840
Jeshi la Anga la Urusi limetumia makombora sita ya masafa marefu kupiga majeshi ya magaidi kwenye maeneo yenye mafuta nchini Syria.
-Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kuwa, kikosi cha kurusha makombora hayo cha Tu-22M3, kimefanikisha zoezi hilo kwa kurusha makombora toka mpakani mwa Urusi hadi maeneo yaliyolengwa na kusababisha maafa kwa magaidi wa IS(wanaoujulikana kama ISIS), huko jirani mji wa Palmyra.
Tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, kati ya Serikali ya Rais wa nchi hiyo Bashir Assad,na waasi nchini humo, Urusi imekuwa ikipigana kuisaidia Syria dhidi ya waasi hao.
Syria na Urusi ni nchi zilizo na ushirikiano wa karibu zaidi, kuliko uhusiano ilionao Urusi na nchi nyingine Mashariki ya Kati. Kwa upande wa pili, Marekani na washirika wake, wako kinyume na Serikali ya Assad, huku wakiwaunga mkono waasi wa nchi hiyo