Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 32,263
- 44,391
Mkuu kuna vitu vya ki-IT umeniacha hapo kama nm, naomba ufafanuzi and I hope utasaida wengi wadadisi kama mie...
Natanguliza shukurani
Mkuu kuna vitu vya ki-IT umeniacha hapo kama nm, naomba ufafanuzi and I hope utasaida wengi wadadisi kama mie...
Natanguliza shukurani
Duh upo sahihi sikusoma vizuri post yakeNinavyojua NM ni nanometer, yaani ndio unene wa ile processor, sijafanya uchunguzi zaidi ila naamini ndio hivyo.
Duh upo sahihi sikusoma vizuri post yake
Ni manufacturing process jinsi inavyokuwa ndogo ndio jinsi ambavyo processor inakuwa energy efficient
Kinachopimwa huwa ni ile core ya processor sio unene wa full chip
Ila sijajua kama wanapima unene wa chip kwa nje au wanapima zile core peke yake
heri yao wameanza na hiyo ya 2010 itakayokuja ni more advance baada yakupata response nzuri..Hatimae intel na amd wamepata mpinzani japokuwa mpinzani mwenyewe anasuasua
Kuna design za processor za aina mbili duniani ambazo ni kubwa
-arm
-x86
Arm ndio hutumika kwenye simu ukiskia snapdragon za qualcomm, A series za apple, mediatek au tegra za nvidia zote hozi ni arm.
Arm hazina nguvu sana na pia hazili umeme sana ndio maana zinatumika kwenye simu.
Aina ya pili ya design za processor ni x86 ambazo hutumia umeme mwingi lakini pia zina nguvu sana. Hizi ndio zipo kwenye laptop, deaktop, server kubwa na super computer.
Hizi x86 zina watengenezaji wawili tu tena wote toka marekani ambao ni intel na amd. Inamaana serikali zote duniani na makampuni makubwa kama bank, atm nk wanategemea hawa jamaa.
Kipindi cha karibuni kuna jamaa anaitwa snowden akatoa siri kuwa marekani anaspy dunia nzima kupitia technology na computer even maraisi wa nchi kubwa kama ujerumani.
So nchi nyingi zikalalamika ila baadhi kama urusi wakaanza kudesign tech zao, na moja ya mafanikio makubwa ndio hizi cpu. Japo zipo slow ila ni zao
Mkuu Chief Mwawa asante kwa hii elimu. Mie nina swali moja. Kwanza kwa uelewa wangu Processor ni core component ya simu au computer, hivyo bila kuwa na kitu hicho huwezi kusema umetengeneza simu au computer, sasa swali langu ni hili, haya makampuni kama Sumsung, sijui Tecno, Huawei nk kama hayatengenezi hizo processor, yanatengeneza nini?
Yaani wao wanatengeneza ile shape ya nje tu? Naomba unisaidie nijue hasa wao wana kitu hasa wanachotengeneza kama the core component of the device si yakwao!
Inategemea na kampuni.
Samsung ana processor zake za arm zinaitwa exynos, na apple ana zake na huawei ana zake zinaitwa kirin. Tofauti na hawa sidhani kama kuna mwengine mwenye processor zake. Ila processor za simu zote ni za arm hivyo samsung/apple/huawei hawafanyi kazi kubwa sababu tayari arm ameshadesign wao wanalipia licence na kuziredesign wanavyotaka wao.
Samsung pia ni mtengenezaji mkubwa wa memory kama internal storage na ram.
Sony yeye anatengeneza sana sensor za camera pamoja na toshiba
Sharp na lg wanatengeneza sana display.
Nokia na erricson wao ni wakali wa network.
Kampuni inapotengeneza simu inanunua technology toka makampuni mengine na kutengeneza simu.