KakaKiiza
JF-Expert Member
- Feb 16, 2010
- 11,902
- 9,323
MACE XIII
Haya yalikua ni mazoezi ya kivita yaliyofanywa na NATO 16-23/4/2012 maalum kwa ajili ya kujifunza ni jinsi gani wanaweza kupambana na kuishinda mitambo ya ulinzi wa anga wa Urusi na nchi nyingine zenye mitambo ya ulinzi wa anga iliyotengenezwa nchini Urusi na Soviet ya zamani.
Mazoezi hayo yalifanyika nchini Slovakia katika uwanja wa ndege wa Sliac na maeneo yanayozunguka uwanja huo na yalikua ni mazoezi yaliyofanywa rasmi kupambana na mitambo ya S-300PMU-1 yanayomilikiwa na jeshi la anga Slovakia moja kati ya nchi za NATO zinazotumia siraha za kirusi.
Ndege zilizotumika katika oparesheni hii zilikua ni
**Ndege inayotoa taarifa za mapema juu ya hali ya anga(AWACS) ya Amerika aina ya E-3
**Ndege inayotumika kujam mitambo ya ulinzi wa anga ya adui aina ya E/F-18 ya Spain
**Ndege zinazotumika kwa mapambano ya angani na ardhini aina ya F-16 kutoka Denmark,
Mirage 2000 na Rafale D kutoka Ufaransa, DA-20 ya Norway, LAARJET-40 kutoka Ujerumani, F-4 ya Uturuki na MIG-20 na L-39(Albatros) za Slovakia.
Kilichafanyika katika mazoezi hayo ilikua ni kuingilia mawasiliano na kujam mitambo ya S-300 ili iwe rahisi kuishambulia mitambo hiyo bila yenyewe kuweza kujibu mashamulizi.
NATO walichokigundua ni kua pamoja na kua na ndege za kisasa zinazoweza kujam mawasiliano ya mitambo hiyo bado mitambo hiyo iliweza kuendelea kutrack ndege zote zilizohusika kwenye oparesheni hiyo na kama ingekua ni vita halisi basi mitambo hiyo bado ingeweza kushambulia na kuziharibu ndege za adui.
Pia NATO waligundua kua ikiwa mitambo hiyo inapata maopareta wenye ujuzi wa kutosha na ikatengenezwa network nzuri za hii mitambo inauwezo wa kulinda anga kwa zaidi ya asilimia 80
Swali la kujiuliza kwa watu wa NATO ni je kama walishindwa kuijam S-300PMU-1 ambayo ni version ya kuuza nje ya nchi itakua vipi wakipambana na S-300V ambayo ni version iliyoboreshwa zaidi kwa ajili ya jeshi la Urusi na mtambo wa kisasa zaidi wa S-400 na Pantsir-S1.
Nawakumbusha tena Amerika kua kama hawatatuliza vichwa wakajidanganya kuivamia Urusi, vita hii haitakua rahisi kwao