Urusi kujenga vituo vya nyuklia Sudan

Urusi kujenga vituo vya nyuklia Sudan

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Russia kuijengea Sudan kinu cha nyuklia cha kuzalisha umeme
Waziri wa Maji na Umeme wa Sudan amesema nchi hiyo na Russia zimefikia makubaliano ambapo Moscow itaijengea Khartoum kinu cha nyuklia cha kiwango cha chini kwa ajili ya kuzalisha umeme.
Mu'taz Musa ameongeza kuwa mbali na hayo, Sudan ina mpango wa kujenga kinu kikubwa cha nishati ya nyuklia katika kipindi cha miaka minane ijayo chini ya usimamizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).
Waziri wa Maji na Umeme wa Sudan amebainisha kuwa wizara yake inakusudia kuongeza kiwango cha uzalishaji umeme na kuleta uthabiti katika usambazaji nishati hiyo kwenye maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Sudan imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa nishati ya umeme kutokana na miundombinu mibovu katika sekta hiyo.
Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita umeme ulizimwa mara tatu kwenye maeneo yote ya nchi hiyo.
Mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana, Russia na Sudan zilisaini mkataba wa ushirikiano katika sekta ya nishati ya nyuklia wakati wa safari ya Rais Omar Al Bashir wa Sudan nchini Russia.
Shirika la Nishati ya Atomiki la Russia Rosatom lilitoa taarifa wakati wa safari hiyo ya al Bashir kwamba makubaliano hayo ya nyuklia yaliyosainiwa na pande mbili yatandaa mazingira ya kuwepo ushirikiano maalumu hususan katika ujenzi wa miundomsingi ya nyuklia, utoaji mafunzo kwa wataalamu, kuanzisha vituo vya sayansi na teknolojia ya nyukllia na kujenga kinu cha nyuklia ndani ya ardhi ya Sudan.
 
Hivi HM, BM, JK na JPM wameshindwa kabisa kuitumia mchuchuma na liganga kuingia makubaliano na nchi yeyote kuzalisha umeme wa nyuklia Tz?..
 
Hivi HM, BM, JK na JPM wameshindwa kabisa kuitumia mchuchuma na liganga kuingia makubaliano na nchi yeyote kuzalisha umeme wa nyuklia Tz?..
Risk sana asee

Bora hio stigler
 
Hivi HM, BM, JK na JPM wameshindwa kabisa kuitumia mchuchuma na liganga kuingia makubaliano na nchi yeyote kuzalisha umeme wa nyuklia Tz?..
Liganga na Mchuchuma hkuna Nyuklia. Liganga kuna Chuma na Mchuchuma kuna makaa ya mawe. Nyuklia kule Selous ambapo kuna Uranium.
 
Back
Top Bottom