Urusi inashambulia vikali eneo la kusini mwa Ukraine

Urusi inashambulia vikali eneo la kusini mwa Ukraine

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,708
Reaction score
35,719
Ukraine inasema mji wa kusini wa Mykolaiv umekumbwa na mashambulizi ‘’mkubwa’’ ya Urusi kufanya mashambulizi usiku kucha.

Mmoja wa watu tajiri zaidi wa Ukraine, Oleksiy Vadatursky, na mkewe Raisa waliuawa, gavana alisema.

Bw Vadatursky, 74, anamiliki Nibulon, kampuni kubwa ya kilimo.

Meya wa jiji aliita ufyatuaji wa makombora ‘’bila shaka kuwa ndio mkali zaidi kuliko mwingine wowote’’.

Kulikuwa na uharibifu wa hoteli, uwanja wa michezo, shule mbili na kituo cha huduma, pamoja na nyumba.

Mykolaiv iko kwenye njia kuu ya kuelekea Odesa, bandari kuu ya Ukraine, na imekuwa ikigongwa mara kwa mara.

Wakati huo huo, Urusi imeahirisha sherehe za Siku ya Wanamaji katika eneo la Crimea inayolikalia.

Sababu iliyotolewa na Gavana wa Sevastopol Mikhail Razvozhayev ilikuwa shambulio la ndege zisizo na rubani za Ukraine kwenye makao makuu ya Fleet ya Bahari Nyeusi.

Kwa muda mrefu, ya kivita imekuwa ikiwa katika eneo la Sevastopol.

Lakini afisa mkuu wa Ukraine, Serhiy Bratchuk, alipuuzilia mbali ripoti hiyo ya Urusi na kusema ni ‘’uchokozi’’.

‘’Ukombozi wa Crimea yetu utafanyika kwa njia tofauti na kwa ufanisi zaidi,’’ alisema.

Vikosi vya Urusi vilitwaa eneo la Crimea mwaka wa 2014. Hilo lilishutumiwa kimataifa kuwa haramu na lilisababisha vikwazo dhidi ya Urusi.

Source: BBC

Screenshot_20220731-220729_Facebook.jpg
Screenshot_20220731-222013_Facebook.jpg
 
Niny pro russia embu muwe mnaeleweka na kuwa na misimamo iliyothabiti.

BBC sio chombo cha westerns? Mmeanza kukubali kuwa vyombo vya habar vya Ulaya na US ni reliable source?

Au ni reliable pale ambapo inaposema negative kuhusu Ukraine ila ikiwa positive kwa Ukraine ni propaganda?
 
Hii inanikumbusha mapigano during WW2 wakati jeshi jekudu la URUSI chini ya Uongozi wa shujaa Field Marshal Zhukov wakati wa operation ya kuuteka mji wa Berlin - wana historia wanasema Red Army ilipiga mizinga pamoja na Katyusha kwa masaa 24 mfurulizo bila ya kupumzika,wanasema wanajeshi million moja walihusika katika operation hiyo.

Ninacho taka kusema hapa ni kwamba Putin na Jeshi lake wakihamua kufanya kweli no one can stop them,watu hawajui kwamba hivi sasa jeshi la Putin linapigana vita Ukraine kwa kindugu ndugu tu,jeshi la Putin likihamua to remove gloves Ukraine patachimbika.

Kwa maneno mengine ni wazi jeshi la Zelensky litashindwa tu na mamuluki wa magharibi kutimuka kama watabahatika kupona - yaliyo jitokeza Afghanistan mwaka juzi ndio yatakuja kujirudia tena Ukraine - Putin atawashinda NATO na Kiranja wao mkuu.
 
Yale yale ya wale wazee wa kwenye muvi ya Titanic walipotembelewa na waokoaji wakiwa na boti za kuokoa uhai wao lakini walipotoka nnje ya meli na kuona ukwasi wao unavyotamanisha wakarudi kujifungia ndani ili wafe na mali zao [emoji16]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hii inanikumbusha mapigano during WW2 wakati jeshi jekudu la URUSI chini ya Uongozi wa shujaa Field Marshal Zhukov wakati wa operation ya kuuteka mji wa Berlin - wana historia wanasema Red Army ilipiga mizinga pamoja na Katyusha kwa masaa 24 mfurulizo bila ya kupumzika,wanasema wanajeshi million moja walihusika katika operation hiyo.

Ninacho taka kusema hapa ni kwamba Putin na Jeshi lake wakihamua kufanya kweli no one can stop them,watu hawajui kwamba hivi sasa jeshi la Putin linapigana vita Ukraine kwa kindugu ndugu tu,jeshi la Putin likihamua to remove gloves Ukraine patachimbika.

Kwa maneno mengine ni wazi jeshi la Zelensky litashindwa tu na mamuluki wa magharibi kutimuka kama watabahatika kupona - yaliyo jitokeza Afghanistan mwaka juzi ndio yatakuja kujirudia tena Ukraine - Putin atawashinda NATO na Kiranja wao mkuu.
Iwwe,hii si vita bali ni OPERESHEN MAALUM YA KIJESHI
 
Back
Top Bottom