URUSI ilijisababishia vita ya Dunia na gharama ilizozipata (Kumbukumbu ya Ushindi wa Mei 9)

Pearce

JF-Expert Member
Dec 15, 2018
577
1,381
Katika mataifa yaliyopata Hasara kubwa sana katika Vita ya Dunia ni Urusi kwa kuanzia miji yake mikubwa kuwa sehemu ya mapambano.

Wakati Joto la vita likianza kutukuta Stalin na Viongozi wengine waliingia ushirika wa Siri na mikataba ya kugawana ulaya Mashariki na Ujerumani ya Hitler (NAZI) mpaka eneo la Poland ligawanywe mara mbili

Hivyo wasisi wa chokochoko wakianza na Musolinni, Hitler na Stalin Kila mmoja akaanza kuvamia jirani zake kwa wakati wake

Jaribio la awali akianza bwana Stalin na Urusi lakini mambo yakaenda ndivyo sivyo kutokana na sera yake ya Great Purge ambapo aliua raia wake ikiwemo makamanda wenye uzoefu wa Vita hivyo vita iliishia akipata matokeo asiyotarajia kutokana na upinzani wa Finland

Intelejensia yake kutokea ubalozi wa ujerumani Japan (alikua shushushu wa Stalin) ilimpa taarifa kuhusu mipango ya uvamizi dhidi ya Urusi kutoka kwa Mshirika wake Hitler, Lakini Stalin alikataa kuziamini taarifa kutokana na mikataba ya Siri waliyowekeana na Axis Power.

Kila mtu anaelewa Russia Soviet likawa taifa lililogharimika kuliko yote Ushindi wake akipoteza askari na wananchi zaidi ya Milioni 20 huku Ujerumani akipambana na pande mbili yaani Magharibi na Mashariki akipoteza watu milioni 5

Maadhimisho ya Mei 9 na hotuba alioitoa bwana Putin na hali ya muonekano wake kiafya na confidence ameshafahamu Vita imeelekea wapi Lakini hajui anajitoa vipi ili kulinda heshima yake.

Mbwembwe za kupiga nyuklia zimeisha na kisaikolojia anatafuta meza ya mazungumzo na nchi za Magharibi kwa walioisikia hiyo hotuba.

PUTIN ANAPITA KAMA ALIVYOPITA LYNDON JOHNSON na RICHARD NIXON

Kudanganya na Propaganda kuhusu vita ya Vietnam ndio ilisababisha kumng'oa Rais wa Marekani Richard Nixon wakati askari wao wanakufa waliamua kuficha kwa zaidi ya miaka 9 au 10. Lakini mambo yakawa wazi na akaondoka ofisini ndivyo Putin alipo Sasa

ZIADA
Ukweli wengi tuliojiunga upande wa Ukraine ni kundi la watu ambao hatupendi uonevu sio kila mtu anashabikia Marekani au Ulaya.
 
Naona putin kawapiga chenga ya mwili wachambuzi uchwara, walitegemea putin angetoa hutoba ya vitisho na kuonesha silaha za maangamizi ili wapate cha kushinda wanabwabwaja kwenye vyombo vyao vya habari lakini wameambulia patupu.

Kama ni mazungumzo ya kumaliza vita Urusi na Ukraine wanafanya mazungumzo tangu siku ya tatu ya vita sema wameshindwa kukubalia mambo kadhaa, sasa ww unapo sema alikuwa anaomba mazungumzo ebu tuambie ni mazungumzo yapi hayo?
Wtz tupunguze ujuaji.
 
Naona putin kawapiga chenga ya mwili wachambuzi uchwara, walitegemea putin angetoa hutoba ya vitisho na kuonesha silaha za maangamizi ili wapate cha kushinda wanabwabwaja kwenye vyombo vyao vya habari lakini wameambulia patupu...
Atatoaje vitisho sasa ikiwa Hana jinsi ya kupambana tena na Ukraine Kila dakika anayoikalia Ina mgharimu kiuchumi, watu wake kufariki na hujuma ndani ya ardhi ya Urusi.....maana adui anaingia anahujumu anaondoka

Hadi vita kuisha Kuna gharama kubwa sana Urusi kurudi kiheshima na kiuchumi
 
Nyinyi si ndo mlikuwa mnajifanya watabili ho sijui putin atatangaza vita rasmi na Ukraine mara sijui atatangaza kutumia Nukilia yako wapi sasa?

Kurudisha heshima kwani ni heshama gani hiyo aliyo ipoteza Urusi ?
Hata ikitokea Urusi akashindwa vita na kukimbia ndani ya Ukrain hilo halitoshi kuiondolea hadhi ya kuwa taifa lenye nguvu kubwa za kijeshi ulimwenguni.

Tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia Marekani kapigana vita nyingi ya ardhini lakini vita pekee aliyo fanikiwa kuishinda ni vita ya Iraq tu tena na hapo alikuwa na rundo la nchi washirika, lakini vita nyingine zote aliishia kupata kipigo na kukimbia kwa aibu ,lakini hilo halijawahi kuiondolea Marekani sifa ya kuwa taifa lenye nguvu kubwa za kijeshi duniani.

Ukisikia taifa lenye nguvu za kijeshi haimaanishi umahili wa kupigana maana kama ni umahili wa kupigana hata sisi Tz tunao, hata Alshababu wana umahili wa kupigana iwapo wakipewa silaha nzuri.

Nguvu ya jeshi la nchi husika huwa inapimwa kwa silaha ilizo nazo na kiwango cha uharibifu kinachoweza kusababishwa na hizo silaha, mfano sasa hivi kwenye vita inayo endelea, Urusi ina uwezo wa kufanya mashambulizi kwenye miji yote ya Ukrain na kufanya uharibifu , lakini Ukraine haina uwezo wa kufanya hivyo ndani miji ya Urusi,hiyo sasa ndio nguvu yenyewe yaani kuwa na uwezo wa kufanya kitu ambacho mwenzako hawezi kufanya.

Urusi ana uwezo wa kuiangamiza Ukraine kwa kuidondoshea mabomu 10 kumi tu ya nyukilia lakini Ukraine haina uwezo hata wa kuangamiza mji wenye hadhi ya manisipaa ndani ya Urusi hiyo ndio nguvu yenyewe.

Hata Marekani alikuwa na uwezo kuiangamiza Vietnam lakini Vietnam haikuwa na uwezo wa kufanya hivyo kwa Marekani, hizo ndio nguvu zenyewe yaani kuwa na uwezo wa kufanya kitu ambacho mwenzako hawezi kufanya.

Kama ni Uchumi dunia nzima ipo inagharamika ikiwemo nchi yako kutokana na vita vinavyo endelea Ukraine.

Hata Uchumi wa Marekani Uchumi wa Marekani umeporomoka kwa aslimia 1.2 kutokana na athari za hii vita, ukuaji wa uchumi wa nchi za umoja wa Ulaya utapungua kutoka aslimia 3.5 mpaka aslimia 1.6 kwa hiyo kiuchumi inawaumiza wengi akiwemo mimi na ww.
 
Chezea yooote usichezee vikwazo vya kiuchumi Putin kwaheri yakuonana anatakiwa the Hague kujibu mashitaka
 
Nyinyi si ndo mlikuwa mnajifanya watabili ho sijui putin atatangaza vita rasmi na Ukraine mara sijui atatangaza kutumia Nukilia yako wapi sasa?

Kurudisha heshima kwani ni heshama gani hiyo aliyo ipoteza Urusi ...
🙏🙏🙏
Kuna jambo umenielimisha hapa, nilikuwa sijui.
 
Nyinyi si ndo mlikuwa mnajifanya watabili ho sijui putin atatangaza vita rasmi na Ukraine mara sijui atatangaza kutumia Nukilia yako wapi sasa?

Kurudisha heshima kwani ni heshama gani hiyo aliyo ipoteza Urusi ...

Hivi unajua kwamba Ukraine Makombora yake ya Nyukria alikabidhiwa Urusi ili kubalance Power na vinu vyake na mitambo ya kutishia Nyuklia vilibomolewa.

Urusi alipewa heshima ya kukaa na siraha hizo...Sasa atangaze kutumia Nyuklia nchi anazozitishia kwani hawana?

Anajua wazi akiharibu na yeye ataharibiwa kama ndio angekuwa na Nyukria peke yake Ulimwengu ungepata shida sana
 
Uonevu
Congo DRC
Yemen
Syria
Palestine
Tigray
MALI
cAR
LIBYA
IRQQ
SOUTH SUDAN
Where do you stand
 
Nyinyi si ndo mlikuwa mnajifanya watabili ho sijui putin atatangaza vita rasmi na Ukraine mara sijui atatangaza kutumia Nukilia yako wapi sasa?

Kurudisha heshima kwani ni heshama gani hiyo aliyo ipoteza Urusi ?
Hata ikitokea Urusi akashindwa vita na kukimbia ndani ya Ukrain hilo halitoshi kuiondolea hadhi ya kuwa taifa lenye nguvu kubwa za kijeshi ulimwenguni.

Tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia Marekani kapigana vita nyingi ya ardhini lakini vita pekee aliyo fanikiwa kuishinda ni vita ya Iraq tu tena na hapo alikuwa na rundo la nchi washirika, lakini vita nyingine zote aliishia kupata kipigo na kukimbia kwa aibu ,lakini hilo halijawahi kuiondolea Marekani sifa ya kuwa taifa lenye nguvu kubwa za kijeshi duniani.

Ukisikia taifa lenye nguvu za kijeshi haimaanishi umahili wa kupigana maana kama ni umahili wa kupigana hata sisi Tz tunao, hata Alshababu wana umahili wa kupigana iwapo wakipewa silaha nzuri.

Nguvu ya jeshi la nchi husika huwa inapimwa kwa silaha ilizo nazo na kiwango cha uharibifu kinachoweza kusababishwa na hizo silaha, mfano sasa hivi kwenye vita inayo endelea, Urusi ina uwezo wa kufanya mashambulizi kwenye miji yote ya Ukrain na kufanya uharibifu , lakini Ukraine haina uwezo wa kufanya hivyo ndani miji ya Urusi,hiyo sasa ndio nguvu yenyewe yaani kuwa na uwezo wa kufanya kitu ambacho mwenzako hawezi kufanya.

Urusi ana uwezo wa kuiangamiza Ukraine kwa kuidondoshea mabomu 10 kumi tu ya nyukilia lakini Ukraine haina uwezo hata wa kuangamiza mji wenye hadhi ya manisipaa ndani ya Urusi hiyo ndio nguvu yenyewe.

Hata Marekani alikuwa na uwezo kuiangamiza Vietnam lakini Vietnam haikuwa na uwezo wa kufanya hivyo kwa Marekani, hizo ndio nguvu zenyewe yaani kuwa na uwezo wa kufanya kitu ambacho mwenzako hawezi kufanya.

Kama ni Uchumi dunia nzima ipo inagharamika ikiwemo nchi yako kutokana na vita vinavyo endelea Ukraine.

Hata Uchumi wa Marekani Uchumi wa Marekani umeporomoka kwa aslimia 1.2 kutokana na athari za hii vita, ukuaji wa uchumi wa nchi za umoja wa Ulaya utapungua kutoka aslimia 3.5 mpaka aslimia 1.6 kwa hiyo kiuchumi inawaumiza wengi akiwemo mimi na ww.
Umetumia akili kubwa kuwaelimisha shabiki huyo wa zelesky
 
Back
Top Bottom