Urusi haitashinda hii Vita

Urusi haitashinda hii Vita

My Son drink water

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
4,930
Reaction score
13,333
Wakuu,hii vita inayoendelea Ukraine imegawa watu ktk makundi makubwa mawili, yaani Pro -Russia ambao wanaamini kuwa Urusi lazima ishinde Vita, na Pro America ambao wanaamini kuwa Urusi lazima ishindwe Vita.

Hii haina Tofauti na ushabiki wa Liverpool na Manchester City, kwamba mashabiki huwa hawazungumzii uhalisia bali mapenzi na ushabiki tu.

Mada yangu haipo kwenye ushabiki bali ktk uhalisia.

NII KWANINI URUSI HAITASHINDA HII VITA?

Urusi ni Taifa kubwa Duniani, lenye nguvu kubwa za kijeshi na nguvu kidogo za Uchumi,lengo na ndoto za Urusi, ni kuangusha dola la Marekani ili yenyewe iwe juu.

Na lengo la Marekani ni kuiminya kabisa Urusi ili ipotee kwenye nguvu za kijeshi na isiweze tena kuinuka. Mataifa yote haya yana urafiki wa kinafiki mno,hayapendani kabisa,yanawindana usiku na mchana.

Bahati mbaya mno kwa Urusi ni kwamba haina nguvu za kiuchumi Marekani ina vyote. Tangu Rais Putin aivamie Ukraine, Mataifa yote yenye nguvu kubwa Ulaya za kiuchumi na kijeshi yamesimama upande wa Ukraine.

Yanaipa Silaha Ukraine na Pesa nyingi ili ipate uwezo wa kupigana Vita. Na pia Yameiwekea vikwazo vikubwa vya kiuchumi Russia.
Russia,haitaweza tena kupita ktk anga lolote la Jumuiya ya Ulaya kwa ndege.

Jana Waziri wa mambo ya nje wa Russia Segei Lavrov alishindwa kusafiri kwa ndege kwenda nje ya Russia kwa sababu ndege zote za Russia zikiweno Private Jets zimepigwa marufuku kuruka kwenye anga la mataifa yote ya Umoja wa Ulaya.

Sasa Russia watapita wapi?

Si hivyo tu, mfumo wa SWIFT BANKING unaowezesha kutuma pesa nje ya nchi na kupokea kutoka nje ya nchi umezuiwa kufanya Kazi kwa Russia.

Tayari Ufaransa imeikamata meli ya mizigo ya Russia na kuipaki ktk Bandari zake. Hata kwa akili ndogo tu unawezaje kushinda vita ?
Yaani Russia kasuswa na Ulaya yote kasoro Belarus Taifa maskini mashariki ya Ulaya. Hata kama mtu unapenda kitu kitu kwenye ukweli simama na ukweli.

Ndo maana Rais Putin amechanganyikiwa kabisa,na kutishia kulipua mabomu ya nyuklia. Akithubutu kupiga nyuklia na yeye watampiga nyuklia,hakutumia akili kuanzisha hii vita,alikurupuka sana, ndo mjue kuwa Hekima ndo kila kitu ktk maisha.

Uchumi wa Russia umeanza kuzorota tayari,na miezi minne ijayo Russia itakuwa hoi kabisa kiuchumi. Na pengine itashindwa kuendelea na Vita. Na sijui Putin atachukua uamuzi gani Baada ya hapo.

Wakati anaanza vita alidhani atachukua Ukraine yote ndani ya siku tatu tu. Hebu jiulizeni,umegeukwa na wote wenye nguvu unashindaje Vita?

Hata ingekuwa Marekani ingeshindwa pia. Wanajeshi wa Russia pichani waliokamatwa Baada ya Gari Lao kuishiwa mafuta
 
Ukrain itashinda hii vita mitandaoni
IMG_20220301_203641.jpg
 
Kwa kuwa ni pro beberu was Amerika lazima utamani Hilo kutokea, waliomchuuza anayeppkea kichapo wapo kimya, wamebaki kutoa taarifa za kupotosha na kuzuia taarifa wasizozipenda kusambaa.
 
Braza USA na wenzie mabepari ni watu wajanja wajanja sana, jiulize Germany ameacha kununua gesi ya Russia? Vikwazo havitaiumiza Russia pekee na hata ulaya wataanza kuosoma namba. Mtu pekee anayewachora wenzie ni USA.
US mwenyewe leo kaingiza mafuta toka Russia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh ukraine anaendelea kuchapwa russia imetoa taarifa masaa 2 yaliopita kwamba wananchi watulie ndani wana jambo lao... Jambo lenyewe ni hili wanataka kutandika kws mizinga jengo flani la kiitelijensia la kiukreni ambali humo ndani ndimo zinamopikwa misinformation zote, rumours zote nk dhidi ya urusi na warusi
 
Back
Top Bottom