City Of Lies
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 5,703
- 7,287
Serikali ya Urusi imesema hakutakuwa na mpango wowote wa kuwarudisha nyumbani Wakenya wanaodaiwa kuhudumu katika jeshi la Urusi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Musalia Mudavadi na Waziri mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov wamesema mataifa hayo mawili hayakuwa sehemu ya mikataba iliyotiwa saini na waliojiunga jeshini.
Lavrov amesema sheria za Uurusi zinaruhusu kusitishwa kwa mikataba hiyo iliyosainiwa binafsi kwa hiari. Aidha, Moscow na Nairobi zimekubaliana kwamba raia wa Kenya hawatajiunga na jeshi la Urusi katika vita vyake nchini Ukraine. Zaidi ya Wakenya 1,000 wanadaiwa kupigana upande wa Urusi nchini Ukraine.
#dwkurunzi