Urithi wa Kikwete kwa Watanzania ni ubaguzi?

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Baba wa taifa alituachia urithi wa umoja wa kitaifa, lakini JK akiwa kiongozi wa CCM na rais wa nchi ameamua kuubomoa umoja wetu Watanzania ambao ulitupatikia heshima si Afrika tu bali ulimwenguni kote. Ni dhahiri kuwa ubaguzi ni urithi ambao Kikwete anaiachia nchi yetu. Kwanza kuanzia kwenye chama chake, uongozi wake umeleta makundi ya kibaguzi. Pili uongozi wake umesababisha umoja wa nchi yetu kuvunjika kwa kupitia udini ambao pamoja na kuwa ni chama chake kimesaidia kuuongeza kasi yake kwa kuuweka katika ilani yake ya uchaguzi lakini ameamua kuupalilia kwa kukaa kimya kabisa. Baba wa Taifa Nyerere aliujenga umoja huo na alikemea vikali pale anapoona hatari za kibaguzi.

Sasa ni kiongozi gani atatusaidia kurejesha umoja wetu wa kitaifa unaopotea badala ya Kikwete mwaka 2010. Je ni Dk. Slaa, labda, je ni Zitto labda. Je ni Shibuda sijui kwa vile napata mashaka kama kuna mtu wa CCM anayeweza kuurejesha umoja wetu kwa vile tayari, JK ameshapanda mbegu ya ubaguzi hata katika chama chake. Kitu ambacho nina uhakika kwa asilimia 100 ni kuwa Lipumba na Seif hawafai kabisa kuungoza nchi hii kwa sababu ni mashabiki wa siasa za udini zinazobomoa umoja wetu chini ya uongozi wa J.K.

Je JK anafahamu kuwa urithi wake kwa Watanzania ni ubaguzi wa kidini na pia ubaguzi na makundi ndani ya chama chake?
 
Mimi niliupenda udini wa Nyerere, kwake yeye Nyerere udini ilikuwa mtu kuupenda uislamu, yeye alivyopenda dini yake hakuwa mdini, tokea tupepata uhuru 1961 mpaka anang'atuka 1985 anasema hakuchagua waziri wa elimu muislamu wote walikuwa wakiristo na labda walikuwa wakatoliki, lakini yeye hakuwa mdini, Chambilecho, Sungura alimpa Chambi mkwewe
 
ila kwa JK hilo lipo wazi kabisa ni mdini hadi inasikitisha kuwa na kiongozi kama yeye na tunapoelekea hii nchi itakuwa haitawaliki labda alazimishe iwe ya kidini, ila nyerere akirudi atasikitika sana kuikuta nchi aliyeipenda ipo katika hali hii,

mungu ibariki tanzania,
mungu tuondolee udini huu
mungu tuondolee mdini huyu
 
ila kwa JK hilo lipo wazi kabisa ni mdini hadi inasikitisha kuwa na kiongozi kama yeye na tunapoelekea hii nchi itakuwa haitawaliki labda alazimishe iwe ya kidini, ila nyerere akirudi atasikitika sana kuikuta nchi aliyeipenda ipo katika hali hii,

mungu ibariki tanzania,
mungu tuondolee udini huu
mungu tuondolee mdini huyu

Siamini kama dhambi ya kuvuruga umoja wetu imefanywa na JK tu. Wengi wamefanya na wengi tunaendelea kufanya. Wengine ndio wa mwanzo kupigia kelele umoja huo wakati maneno, fikira, mitazamo na hata matendo yetu ni ya uvunjaji umoja huo. Tena wengine wameshazoea kiasi ya kwamba upeo wa kutambua makosa hayo kuwa ni makosa umewaishia..

Kama kuteua majina ya ALY. ASHA na GHASIA kwa wingi zaidi ya tulivyozoea ndio kunamfanya awe mdini basi ni bora ukajiangalia wewe mwenye muono huo kama sio udini huohuo ndio unaokupelekea ukawa na muono ama mtazamo huo..

Kosa la JK ni kutokuwa na nguvu, utashi na uthubutu wa kusimama kwa ukakamavu kukemea yanayoendelea sasa kutoka katika pande zote za kijamii, ziwe kikabila, kidini, kitabaka, kisiasa na vinginevyo.
 
ila kwa JK hilo lipo wazi kabisa ni mdini hadi inasikitisha kuwa na kiongozi kama yeye na tunapoelekea hii nchi itakuwa haitawaliki labda alazimishe iwe ya kidini, ila nyerere akirudi atasikitika sana kuikuta nchi aliyeipenda ipo katika hali hii,

mungu ibariki tanzania,
mungu tuondolee udini huu
mungu tuondolee mdini huyu

Sipendi kabisa utawala wa JK kwa mengi mno na madudu yake hasa ukizingatia kwa yeye kukosa power ya kiraisi.

Ila kwa hili la U-dini kwa kweli tunaweza tukawa tunamsingizia, sidhani kama JK ni mdini, yeye kama kiongozi ana dini na anawajibu wa kuifuata dini yake.

Ukiangalia safu yake ya uongozi anajitahidi sana ku-balance hasa mambo haya ya dini sioni kama kuna mahali amemteua mtu kwa dini yake huwa anajitahidi kuwapa watu wenye sifa kutokana na vyeti wanavyomwonyesha na ambavyo vimefanyiwa kazi na wizara ya kazi huko kwa Dr. Milton makongoro.

Tatizo kubwa ni kwamba hakuna anayewajibika kuanzia Raisi mpaka mfagizi na hawa wote wana dini mbalimbali mpaka wapagani kama kingunge. ni afadhali basi kama wangekuwa hata wanafuata hizo dini kwani wangekuwa wema na wala wasinge saini mikataba ya wizi mibovu, wasinge tuibia fedha zetu kwa kutumia majina kibao mara Meremeta, EPA, Richmond. utawala wa Tanzania hauharibiki kwa dini wala dini haitaleta vita ila ufisadi.

Nchi kuanza kuona makundi na kubaguliwa ni umasikini unaosababishwa na ufisadi, ni vyema tukaunganisha nguvu kupigana na ufisadi kuliko hizi siasa rahisi za kusingizia dini, hata tukisema ni dini ni watanzania gani wenye maisha bora zaidi ya wengine kwani hospitali, barabara, maji, shule, umeme si wote wanakosa, je kuna mtaa gani ni wa waisilamu au wakristo hakuna. awe John au Juma sote tunapata madhila yale yale.

Kikwete si mdini ila hawezi uongozi. hajawahi kumteua mtu kwa dini yake, hizi kelele ni za wachache wenye uchu wa madaraka. Hawezi kumfanya kila rafiki yake waziri kuna nafasi sitini tu. hawezi kumfanya kila mmoja katibu mkuu au jaji au mkurugenzi, hivyo waliobaki wafanye kazi uteuzi umekwisha walime vitunguu, nyanya, na uewele. Kanyaga twende.
 
JK sio mdini ni kiongozi legelege. Msimuonee wajameni kwa mengine yasiyohusika.
 
Hata Julius K. Nyerere alikuwa mdini, hujui? Una umri gani?

Neno hilo la ''hata'' ulilotumia linaonesha kuunga mkono hoja ya kuwa urithi wa Kikwete ni ubaguzi. Habari ya umri, kama mimi ni mzee, au kijana au wa makomo, lakini wewe na mimi tunauhitaji umoja wa kitaifa.

Hapa ni vyema kujua kuwa tanzania, Afrika na ulimwengu mzima wafahamu kuwa Nyerere katuachia umoja, ndio maana watu wa dini tofauti tuliishi pampja vizuri kwa upendo na hata kuoana.
 
Transparency,
freedom of expression and
Government of all talents, ndivyo JK anvyoendesha Serikali ya awamu ya 4, sio ubabe wa Serikali ya Nyerere na zilizo pita mliyozoweya. mnashangaashangaa huu uwazi tulionao ambazo ni muhimu kuleta maendeleo nchini
 
Siamini kama dhambi ya kuvuruga umoja wetu ni ya JK
Kosa la JK ni kutokuwa na nguvu, utashi na uthubutu wa kusimama kwa ukakamavu kukemea yanayoendelea sasa kutoka katika pande zote za kijamii, ziwe kikabila, kidini, kitabaka, kisiasa na vinginevyo.

Naomba kufafanua maana ya urithi. Urithi ni kitu unachoachiwa na mtu aliyekutangulia. Kama JK ni mdini au la, na kama ni kiongozi legelege au anafanya makusudi, Watanzani tunajua kuwa ubaguzi wa kidini na ubaguzi wa makundi ndani ya CCM umeibuka na kushamiri katika kipindi chake cha uongozi na hivyo huo ndio urithi anaotuachia Watanzania.

Kama vile Nyerere ulivyotuachia umoja, Mkapa akaacha mfumo wa kifisadi, JK katika kipindi chake ameacha nyuma ubaguzi. Kitu ambacho nimesema nina uhakika asilimia 100% ni kuwa Lipumba na Seif ni wabomoaji wakubwa wa umoja wa taifa letu kwa udini -hawafai. Je ni Slaa, Zitto au Shibuda anayefaa kuurudisha umoja wetu badala ya Kikwetu 2010?
 
Hapa ni vyema kujua kuwa tanzania, Afrika na ulimwengu mzima wafahamu kuwa Nyerere katuachia umoja, ndio maana watu wa dini tofauti tuliishi pampja vizuri kwa upendo na hata kuoana.[/QUOTE]


Waislam walilalamika sana na utawala wa Nyerere kuwa ulikiwa wa kibaguzi, labda wao walikuwa wavumilivu sana na hawakutaka kuleta fujo, as result kwasababu wewe hayakukugusa ndo uliona kulikua na umoja.

Nyerere aliikuta Tanganyika ikoshuary kabla yeye kuwa rais na ndo yeye aliwezakuchaguliwa kuongoza Tanu ktk jamii ya wadini nyingine. yeye ndo alikuja na ubaguzi mpaka wale waliomkaribisha wakaanza kumchukia kwa ubaguzi wake. How old are
?
 
Last edited:
Baba wa taifa alituachia urithi wa umoja wa kitaifa, lakini JK akiwa kiongozi wa CCM na rais wa nchi ameamua kuubomoa umoja wetu Watanzania ambao ulitupatikia heshima si Afrika tu bali ulimwenguni kote. Ni dhahiri kuwa ubaguzi ni urithi ambao Kikwete anaiachia nchi yetu. Kwanza kuanzia kwenye chama chake, uongozi wake umeleta makundi ya kibaguzi. Pili uongozi wake umesababisha umoja wa nchi yetu kuvunjika kwa kupitia udini ambao pamoja na kuwa ni chama chake kimesaidia kuuongeza kasi yake kwa kuuweka katika ilani yake ya uchaguzi lakini ameamua kuupalilia kwa kukaa kimya kabisa. Baba wa Taifa Nyerere aliujenga umoja huo na alikemea vikali pale anapoona hatari za kibaguzi.
.

Hakika Nyerere ndie alieifikisha nchi ya Tanzania hapo ilipo. Yeye alikuwa haambiliki na mbabe sana. Alikuwa ni mtu aliyevunja haki za binadamu kwa kuzuia freedom of speech. Ilikuwa ukipingana naye basi nchi utaiona. Muulize Mwl Kazibure wa Kibaha Sec atakwambia au muulize Mzee Aboud Jumbe na wapo wengi wengi na wanamlaani mpaka leo kwa ku destroy maisha yao.

Yeye aliloamua alifanya hata likiwa la kuvunja katiba alifanya. Alileta Ubalozi wa VATICAN huko Tanzania ambao ni kinyume cha katiba ya Tanzania. lakini hakuwa na wa kumpinga.

Alimbania Kikwete kuwa rais mwaka1995 na kumpa Mkapa kwa kuvunja utaratibu wa CCM kuchagua kiongozi wao.

Alimlaani sana Malechela kwa issue ya G 55 kudai Serikali ya Tanganyika. na leo yapo wapi.

Mimi nasema JK ni mzuri ila amezidi upole kwa watendaji wake na wao ndio wanatumia mwanya huo kumwalibia.

Hakika alikuwa mnafiki sana alihubiri usawa lakini mwenyewe alikuwa mbaguzi. Je kwenye jeshi,polisi au hata magereza kuna mhindi, mwarabu au hata mzungu. Ina maana wao hawataki kujiunga huko. Mbona JKT walipita.

Wanaodai JK ni mdini ni WAKATOLIKI kwani wao walijiona na waliwekwa juu wakati wote JKN alipokuwa hai sasa wanabanwa basi kila kitu watasema.Hakika wakatoliki wanajiona ni bora kuliko Uislam au hama madhehebu mengine ya kikristu.

Poleni sana WAKATOLIKI mlilelewa vibaya na JKN
 
nasikia wakatoliki hao hao wana mpango wa kuleta hoja JKN apandishwe daraja kutoka Baba wa Taifa na kuwa saint (Mtakatifu).

Je itawezekana hayo?
 
Ni wazi kabisa suala la udini limejitokeza sana katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya nne. Anachopaswa kufanya sasa JK ni kukemea udini kwa nguvu zote ili asiache hii legacy mbaya atakapomaliza muda wake 2010. Kwa upande mwingine aache kuwachekea mafisadi waliomzunguka. Lakini kwa vyovyote vile tunahitaji Rais aliye serious na intelligent zaidi 2010.
 
Ni wazi kabisa suala la udini limejitokeza sana katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya nne. Anachopaswa kufanya sasa JK ni kukemea udini kwa nguvu zote ili asiache hii legacy mbaya atakapomaliza muda wake 2010. Kwa upande mwingine aache kuwachekea mafisadi waliomzunguka. Lakini kwa vyovyote vile tunahitaji Rais aliye serious na intelligent zaidi 2010.

Kujitokeza kwa swala la dini si kwa sababu JK anashabikia dini la hasha, ila Serikali yake imeshindwa kufanya kazi iliyokusudiwa na kupeleka mijadala ya kujikomboa kwenye nyumba za ibada, na hilo hakuna anayeweza kulizua wala kulisimamisha. Ni mpaka pale serikali itakapoweza kutimiza wajibu wake.

Ikumbukwe waumini wa dini mbalimbali ndio hao hao wananchi, hivyo ni wahanga wakubwa wa mazila ya mafisadi na maisha magumu, ahadi za uongo za JK za maisha bora kwa kila mtanzania kumbe ilikuwa maisha bora kwa kila fisadi.

Huwezi kuziba waumini na viongozi wao midomo, na hawa wanahasira dhidi ya serikali yao wala sio dini na dini. Sasa moto unawawakia wanatafuta pa kushika. JK amechoka mwili na akili ashauriwe apumzike sio mbaya akiachia first term.
 
nasikia wakatoliki hao hao wana mpango wa kuleta hoja JKN apandishwe daraja kutoka Baba wa Taifa na kuwa saint (Mtakatifu).

Je itawezekana hayo?

teh teh teh..

Huu ndio ukisikia utaahira..ama kwa hakika ukamuaji maiti kinyesi una athari mbaya za kiakili..lol
 
Hii hoja na thread kwa ujumla haya majadiliano hayana tija kwa Tz!

Inategemea mtazamo wa mtu na anavyotoa tafsiri yake, na hoja anayotoa. Lakini tunahitaji Rais mbadala wa JK mwaka 2010. Sidhani kama ni busara kama Watanzania tutajidanganya kuwa mambo yako shwari kama waswahili tunavyosema kuwa mbuni huficha shingo yake kwenye udongo huku mwili wake mzima unaonekana. Rais mlegevu kama wengine walivyosema tuachane naye 2010. Tunahotaji tanzania moja na imara.
 
Mara nyingi mijadala humu inageuka kuwa matusi badala ya hoja, na huu ndio mwanzo wa umasikini mkubwa unaotumaliza. Unapofikia hatua ya kutukana maana yake kichwa kimeishiwa, kwa wenye hekima na busara wakiona hivyo hukaa kimya ila wapumbavu huanza matusi na lugha chafu. Msingi mkubwa wa utu na ubinadamu ni kuheshimiana hata pale wanapokuwa hawakubaliani.
 
Back
Top Bottom