Urithi wa Baba

Munyaluganda

Member
Jul 13, 2022
7
21
URITHI WA BABA

Kuna watu husema kwamba nguo ni nguo tu hata iwe ya namna gani, ni kweli huo ni mgororo wa nafsi kabisa kwani si uungwana kuingilia mawazo ya mtu ila leo acha twende mbali kidogo Joho lina maana kubwa mno. Joho ni vazi la kiafalme lenye kubeba maana kuu ya heshima. Viongozi wa Imani hasa kwa Wakristo yaani Papa na Maskofu ndio huruhusiwa kuvaa Joho pamoja na ile kofia yake ila wahudumu wengine huvaa Joho pekee bila kofia na huo ndio utaratibu wa Kanisa.

Joho ni vazi refu kama koti lenye maana kunyesha kwa mvua (ufalme). Zamani kuitambua nyumba ya wasomi wala haikukuhitaji kutumia nguvu nyingi kama mpasua mbao, mambo yote yalimalizika pale sebureni tu ila sijui sasa utamaduni huo kama bado upo au ndo yale yale hata na wale wanaohitimu darasa la saba wanavaa majoho. Duuuuuuh wanadamu bwana kupenda utukufu usio kuwa na jasho ndio maana JPM hakupenda watoto wa shule za misingi wafanye sherehe wakati wa utawala wake kwa kuona wanapenda sana kuvaa majoho katika mahafali ya darasa la saba. Chukue hii, kwa mujibu wa dunia Joho linavaliwa na Muhitimu wa Chuo Kikuu pekee anayehitimu shahada ya kwanza, shahada ya uzamili au shahada ya uzamivu.

Joho sio kama mziki wa Singeli kusema kwamba ukipigwa kila mmoja atacheza, hata kila msiba una mliaji wake. Mwanafunzi ni mtu yeyote anayepokea mafunzo ya kitaaluma kutoka kwa Mwalimu. Mfuasi ni mtu aliyepokea mafundisho ya Mwalimu wake na akawa tayari kumfuata ina maana Mfuasi ni mwanafunzi aliyekomaa. Mwanazuoni ni mtu aliyebobea katika taaluma Fulani na ni mtu wa kufanya tafiti. Mkufunzi ni mtu aliyebobea kwenye taaluma Fulani na ndiye muangalizi wa Mwanazuoni katika utafit. Kwa maana hiyo mwanafunzi huvaa sare na Mwanazuoni huvaa Joho la heshima wakati wa mahafali.

Watu wengi huamini kwamba Digrii inachukuliwa. Bro Digrii hutafutwa tena katika mazingira yasiyo ya kawaida kama unabisha muulize yeyote aliyeko mwaka wa mwisho katika chuo chochote atakwambia moto anaoupitia. Na wengi tunaamini chuo ni BATA ila bata huyo alishachukuliwa na Mwewe zamani sana enzi za Mwalimu. Rangi ya kitambaa cha Joho haichaguliwi lelemama kama tunavyochagua nguo za mitumba pale Maimorio, vazi hili rangi yake huchaguliwa kulingana na Digrii ya mtu aliyoisotea ndio maana rangi ya Joho hutofautiana kutoka idara/kitivo kimoja na kingine.

Ukosefu wa ajira ndicho kirusi kinachowatesa wahitimu wengi kuliko hata kirusi cha COVID. Bro hivi wasomi waache ajira zitangazwe kwanza ndipo waende kusoma au waende kusoma kwanza ajira zikitangazwa waende kufanyakazi. Mimi ni Mtanzania hapo sijafungamana upande wowote na ndio utamaduni wangu
294499010_3309270259395873_7656574947731371863_n.jpg
 
Back
Top Bottom