Urithi tulioachiwa na wanawake

miles45

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
3,468
8,287
Kutokana na muda kwenda na mambo kubadirika nimekuja kugundua asilimia kubwa ya wanawake hawaishi kwa muda uliopo wanaishi muda ambao wanaume wengi bado hawajaufika.

Kwa kuanza naomba niwaorodheshee mambo tulio achiwa na wanawake.

1: Uvivu, wale wanawake walio kuwa wanasubiri kuletewa wanapotea na wengi wao wamekuwa watafutaji na wanajishughulisha huku vijana wengi wa kiume wamebaki kuwa tegemezi na kushinda wanaburuza ndala hizi za kisasa.

2: Umbea, wanawake saizi kuwakuta wanefanya umbea ni nadra sana ukilinganisha na wanaume vijana wa kiume ndio waendesha mijadara mikubwa ya umbea kupita wanawake wenye fani yao.

3: kupoteza muda, wanawake walikua wapoteza muda wakubwa sana ila kwa sasa vijana ndio wapoteza muda kwa sasa wanawake kitu chochote ambacho hakija ambatana na pesa huwakuti yaani wao saizi kwao kila kitu pesa haijalishi itawakosti vipi ila hela waipate.

4: Uthubutu, vijana wengi wa kiume hawana uthubutu kabisa ukilinganisha na wanawake wanawake wamekua wakithubutu kwa namna yoyote ile mfano dada yetu mobeto anavyo mpambania rickross ampate huku vijana wa kiume wakiwa ndio maripota wa harakati za huyu dada (umbea) wakati ilitakiwa pia na vijana wa kiume wajitokeze hata kwa tiwa saveg.

5: Uonga wa maisha, vijana wa kiume ni waoga haswa wakati wa kike wao hawaogopi chochote kilicho mbele yao ili mradi tu wahisi huko mbele kuna chenji.

6: Ushirikiano, wanawake kwa sasa wanaushirikiano mkubwa sana na wameungana haswa na wametengeneza jeshi imara... yaani wao saizi ni full kupiganiana kama team vile kama unabisha mpige kibao mwanamke alie taka kukuua alafu wenzie wasikie . Wakati huo vijana wa kiume ndio wanakandamizana mfano hili sakata la haji manara na wake zake yaani manara kuachana na rushana yaani vujana wa kiume ndio wamefurahia na kumpondea na kumuona manara ni mjinga au sakata la docta mwaka na mkewe yaani vijana wa kiume ndio wapo mstari wa mbele kumpopoa mwaka.

7: kutoa watu kasoro, yaani vijana wa kiume ndio wanaongoza kinacho sikitisha zaidi utakuta mtoto wa kiume anamtoa kasoro.

Mwanaume mwenzie sasa unajiuliza huyu alikua anamuangalia mwanaume mwenzie kwa jicho gani haswa hadi akagundua hizo kasoro ni ushoga au ni nini....? Wakati wanawake huwakuti sikuhizi wakitoana kasoro yaani kasoro atakayo iona kwako ni kuwa una hela au hauna hela.

Kwa hayo machache nasema hichi kizazi kisipo kuwa makini kitaburuzwa hovyo na wanawake miaka ya hizi karibuni .

Yaani vijana wa kiume wamekua wapuuuzi wa kutupwa huku wa kike wao kama mambo hayahusiani na hela huwakuti hapo.

Na siku hizi wanawake ndio huvaa viatu na wakitembea barabarani wanatembea ule mwendo wa kiume na buti zao huku vijana wa kiume wakitembea kwa kuburuza hizi ndala za kisasa wao wanaita sendo.

Vijana amkeni
 
Vijana wa siku hizi ni hasara sana kwa taifa. Kwahiyo hiki ndicho unachokiona kwenye jografia yako ya Maisha shuwain makatan wahalaana wewe.
 
Lengo la Maisha sio kushindana ni kuishi Maisha yako unayotaka nashangaa mnaopeteza Muda kuwawaza Binadamu wenzenu what f**" is
 
Kwanza jifunze kuandika, jua matumizi ya R na L bila kuchanganya, pia tuambie jinsia yako.
 
Back
Top Bottom