Mi nadhani ile kamati iliyochunguza Richmond pia inastahili pongezi kwahiyo kama inabidi basi apewe mwenyekiti Mwakiembe.....
kwanini simpendekezi Dr.Slaa, ukiwa upande wa Upinzani ni wazi kwamba wewe unakuwa mwepesi wa kusema lolote unaloona linafaa na pamoja na kupinga na kutoa mijadala ya kukosoa serikali au chama Tawala, kwa Dr. Slaa, kusema na kuendelea kusema kuhusu rushwa nchini na uozo wa serikali ni sehemu ya kazi yake; Ujasiri kwenye hili ni kwa yule mtu ambaye mazingira ya kumfanya ale rushwa yapo, kama vile yupo chama Tawala,yupo serikalini na ana nafasi nzuuri lakini akaamua kusimamia haki bila kujali maslahi binafsi na bila kuogopa, huo ndio ujasiri.
sasa ukiangalia suala la richmond lilikuwa ni suala tete,linalohusu vigogo wa chama na hata kuweka serikali sehemu mbaya maana yale yalikuwa ni maamuzi ya seriklai nzima na mtu aliyeshukiwa kuwa ni mhusika mkubwa alikuwa ni mkubwa wa nchi....lakini kamati iliweza kufanya kazi kwa ufanisi na kwa ushujaa bila woga kuonyesha dhuruma iliyotendeka.....hao ndio mashujaa, kwani walikuwa ni viongozi wa chama na waliokuwa wanawachunguza walikuwa viongozi wao....
sio hili lakini wapo viongozi wanaochukua maamuzi ya kishujaa wengi tu, hao ndio ninaoweza kusema tuwa-spot na wapendekezwe......
Zitto nae ilikuwa ni sehemu ya kazi yake kama mpinzani na amekuwa akiyumba sana kimsimamo, labda ameona sasa ameshakuwa maarufu, huwezi kuwasaliti wananchi waliokusaidia ukaingia bungeni na kuwa sababu ya kujulikana, unasema hadharani kabisa kwamba unafanya utafiti wa majimbo kujua wapi ugombee????
kuhusu mh.Sitta, hapana, hakuna hoja ya nguvu ya kuonyesha kiasi gani amepinga rushwa....
labda TAKUKURU pia wangeshauri kuhusu hili maana ndio wanaopokea taarifa nyingi za rushwa na kujua wapi kuna nini na nani?