DOKEZO URGENT: Binti wa miaka 16 ameozeshwa kwa lazima kama mke wa pili, huko Laela, Sumbawanga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Habari za jioni ndugu yangu katika JMT. Nadhani utakuwa umefuatilia mrejesho wa serikali kuhusu hoja uliyoleta. Mara kadhaa kumekuwa na mrejesho kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali juu ya ajenda hii. Hata hivyo, sidhani kama ni sahihi kutotoa msaada na ushirikiano kwa hoja iliyopo sasa dhidi ya manusura ambaye anahitaji msaada kwamba, tukae kimya tu kwa kuwa bado ile hoja ya awali haijafikia mwisho.

Sidhani kama kukaa kimya bila msaada ni sahihi. Hivyo, Kila jambo tutafanyia kazi katika kudhibiti ukatili wa kijinsia kulingana na lilivyo sasa kwa mazingira ya Sasa na wakati ujao nao utafanya kazi kwa mazingira ya wakati huo. Tumeshampata mtoa taarifa Ili kumsaidia manusura wetu. Ahsante Sana, ubarikiwe. usiku mwema,
 
Muheshimiwa kwa hili pongezi nyingi zikufikie nakuahidi kukufikishia taarifa za unyanyasaji pale tu nitakapobaini watoto wanateseka sana maeneo ya vijijini
 
Asante sana mh waziri kwa wepesi wako wa kuzingatia matatizo ya wtz kwa haraka. Mungu akubariki sana.
Hujielewi ,kama wao

Serikali ipeleke mswada wa mabadiliko ya Sheria ya ndoa Kwa umri 14yrs ,kimsingi bint amekizi vigezo vya kuolewa miaka 17

Labda awe mwanafunzi
 
Ahsanteni sana Wadau wa JF kwa taarifa hii. Huu ndiyo ushirikiano wa jamii tunaohitaji. Tunashughulikia. Ahsanteni kwa mawasiliano ya namba ya simu.

Uwajibikaji ni moja ya sifa muhimu kwa kiongozi. Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima katika hili unastahili pongezi za dhati.

Tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu akujalie uzima na siha njema ili uendelee kufanya kazi kwa weledi.

Tunahitaji kusonga mbele kwa pamoja na kujenga jamii salama ambayo itakuwa chachu ya mabadiliko katika taifa letu.

Kwa mara nyingine tena pongezi kwako Mheshimiwa.
 
Asante Sana mh.waziri

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 

Vuta pumzi kidogo!

Binti hataki kuolewa wazazi na ndugu wanamlazimisha.

Haki za Binti zinasimamiwa na serikali chini ya wizara ya Doctor Gwajima, Tatizo liko wapi?
 
ila wahuni mtaani wakimtafuna wakamtia mimba fresh au sio! waafrica inatakiwa tuachane na mentality za kipuuzi za kumezeshwa na wazungu.
Kwa niaba ya wahuni hapa sumbawanga nimekutumia inbox"TAMKO LA BARAZA WAHUNI LAELA,SUMBAWANGA" Lisomwe stendi zote nchini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…