Urais wa Zanzibar na dhana ya usulutani

Urais wa Zanzibar na dhana ya usulutani

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
17,975
Reaction score
17,380
Sio ajabu kesho kumuona mtoto wa Dr. Sheni nae akichukua fomu ya kuomba kuwa Rais wa Zanzibar Kama vile Urais Ni haki kamili ya kurithi.

Ukishakuwa na akina"Jecha" Zanzibar na Dodoma kila kitu kinawezekana.
 
Wewe usitatame nani ana chukua fomu ya kugombea urais,kazaliwa na baba gani ,ni mtoto wa rais au mfanya biashara mkubwa au ni mtoto wa masikini omba omba. Wewe angalia ubora wa mtu, ukiachana na wivu na makuzi uliyo kulia tizama uwezo wa kiongozi anae gombea, usiangalie mengineyo muhukumu kwa matendo aliyo fanya yeye. Kwani kama baba yako alikuwa ni daktari wa moyo na wewe ukasomea kazi iyo iyo je hauruhusiwi kutibu itakuwa ni ufalme?
 
Usultani na kikundi cha wahuni (CCM) ni vitu viwili tofauti, afadhali Usultan unaleta maendeleo
 
Nafikiri sisi watanzania ni wamoja tuwe na lugha safi na pia yeyote atakae pata urais bado ni ndugu yetu awe CCM. au kutoka upinzani,tusijenge chuki. Chuki haijengi taifa,badala ya chuki tuangalie ubora na msimamo wa kiongozi atakae shika madaraka ya kuongoza nchi yetu.
 
Dr Shein ni kama Mzee Mkapa, Familia zao waliziweka mbali na Dola. Walio attach familia zao na Dola ni Nyerere,Mwinyi na Jakaya

… wazee wenzangu watamkumbuka Mbunge wa Taifa Joseph Nyerere, vijana watamkumbuka Ridh moko, watu wazima watamkumbuka Abbas Mwinyi
 
Je, unamkumbuka Makongoro, Madaraka nk? Ndiyo kama ninavyosema tuangalie mtu anaye faa kuongoza Nchi tusiabgalie ni mtoto wa nani hata kama ni mtoto wa masikini tajiri mtoto wa Rais mbuge,tuangalie je anavigezo? Tusiingize wivu ndugu zangu tutashindwa kupata kilicho bora kwetu
 
Back
Top Bottom