Urais Wa Dr. Magufuli ni funzo kwa Wengine

Urais Wa Dr. Magufuli ni funzo kwa Wengine

weka akiba ya maneno.

Kuchaguliwa (kutangazwa kuwa mshindi) kwa dr. Pombe magufuli kunaleta funzo (fundisho) moja tu nalo ni
kuwa tanzania inahitaji tume huru ya uchaguzi na katiba ya wananchi.

na sanduku la kura tanzani halina maana
 
Kwako Wewe suala la kuwa na Tume huru na Katiba ya wananchi ni kelele tu?
Una imani na NEC kuwa ni tume huru na imetekeleza majukumu yake kwa uhuru na haki?

Ni kwa nini katika wadau wa uchaguzi ni CCM tu ndio wana imani na NEC?
Kati ya majimbo 264, Magufuli ameshinda majimbo 218, hata baadhi ya majimbo yaliyoenda UKAWA, Magufuli ameongoza mikoa yote ya Tz bara kasoro Arusha, Kilimanjaro na Dar, endelea kujidanganya na propaganda ila ushindi wa Magufuli ni dhahiri, kama CDM wataendeleza propaganda badala ya hoja kama zamani watadondoka muda si mrefu
 
We politiki unapiga porojo tu hapa.
Naamini Lowassa kashindwa, na hata ukimuongezea zile 'kura za mashaka' bado Magufuli kamnyoosha.

Yaani unataka kuniambia Lowassa kakosa hata fomu moja tu ushahidi wa matokeo ya jimboni (iliyosainiwa na wagombea na mawakala) ambapo NEC wamemchakachua.

Huo ni umburula.
Nashawishika kuwa Lowassa hana ushahidi wa kuibiwa.

Mchezo umegomea kwa mujibu wa data za BVR, wapiga kura waliojiandikisha Dar ni 2.7m wakati wa ile Mwanza ya Zamani (Mwanza, Simiyu na Geita) ni takribani 3.1m. Old Mwanza imeifuta Dar kwenye kiki.
Afu ngome ya Arusha. 1.06m imemezwa na Dodoma yenye wapiga kura takribani 1.1 pia.
Sasa Magufuli kafunika Dodoma na Old Mwanza na hivo kuzima kiki za Dar na Arusha.
Mchezo ukaishia hapo Mangi.

Jozi 1, siku hizi CDM na wao akili ndogo inaongoza akili kubwa, haya ndio madhara ya kina Yericko Nyerere kuwa na sauti sawa na kina Mnyika, Lowasa ameongoza mikoa mitatu tu Tz bara, halafu anakuambia ameibiwa, Magufuli ameongoza majimbo 218 kati ya majimbo 264, ameongoza mikoa yote kasoro Arusha, Kilimanjaro na Dar, ushindi wa Magufuli ni dhahiri, UKAWA inabidi watafute kilichowakwamisha kama mtandao mdogo, kampeni zisizo na tija or chochote, ila kama wataendelea na propaganda za kitoto waisahau IKULU
 
Last edited by a moderator:
Marco Polo come on ona haya usoni kaka maghufuli hakushinda Urais kwa merit bali fraudulent election hii ni wazi
hata dunia inajua kwahiyo acha kualalisha haramu
je?,fraud imefanywa ktkt majimbo 188,tumia akili..
 
Kati ya majimbo 264, Magufuli ameshinda majimbo 218, hata baadhi ya majimbo yaliyoenda UKAWA, Magufuli ameongoza mikoa yote ya Tz bara kasoro Arusha, Kilimanjaro na Dar, endelea kujidanganya na propaganda ila ushindi wa Magufuli ni dhahiri, kama CDM wataendeleza propaganda badala ya hoja kama zamani watadondoka muda si mrefu

Mbona huna hoja. Mahali unaona ameshindwa kuiba kulishindikana. Ebu leta mantiki kwa nini vifaa na watu waliojaribu kukusanya matokeo kwa kuchukua matokeo yaliyotundikwa na data za mawakala wamechukuliwa na polisi ili wasiifanye kazi hiyo. kwa nini?
 
Kwa hiyo hiyo tume ingemtangaza Lowassa mshindi ungeukataa ushindi wake??

Hiyo haitatokea kwa tume hizi NEC na ZEC kama zilivyo
Unafikiri kuna uwezekano kwa Tume za uchaguzi Tanzania kumtangaza mshindi mgombea wa upinzani?

Hilo lingefanyika Zanzibar ambako Tume imefuta uchaguzi ili kutengeneza mazingira ya CCM ishinde.

Unaweza kunisaidia kufahamu ni kwa nini NEC na ZEC zote zilitanganza majimbo ambayo CCM inaonesha kushinda kwa muda mrefu na yale ya upinzani kucheleweshwa kutangazwa?
 
Mbona huna hoja. Mahali unaona ameshindwa kuiba kulishindikana. Ebu leta mantiki kwa nini vifaa na watu waliojaribu kukusanya matokeo kwa kuchukua matokeo yaliyotundikwa na data za mawakala wamechukuliwa na polisi ili wasiifanye kazi hiyo. kwa nini?
Kwa hiyo wewe una amini hadi leo CDM wanajumlisha matokeo, wameshindwa kutangazwa hata jimbo moja waliloibiwa, wanaishia kutoa general statements tu, kamuulize EL aseme hiyo 10m votes amezipataje, usiwe na mahaba tu, tumia na akili zako.
Kuhusu hiyo Tallying center, hao foreigners walikuwa wanafanya nini humo, CDM wanajua vizuri kabisa kuwa foreigners wanaruhusiwa kama observers au guests katika siasa za Tz, na ndio maana yule balozi wa China alivyo vaa kofia ya CCM, ilimbidi hadi atoe statement, msitetee vitu visivyo na tija
 
Kati ya majimbo 264, Magufuli ameshinda majimbo 218, hata baadhi ya majimbo yaliyoenda UKAWA, Magufuli ameongoza mikoa yote ya Tz bara kasoro Arusha, Kilimanjaro na Dar, endelea kujidanganya na propaganda ila ushindi wa Magufuli ni dhahiri, kama CDM wataendeleza propaganda badala ya hoja kama zamani watadondoka muda si mrefu
Naomba ujibu maswali kwenye post hii ambayo umeyakwepa.

Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...gufuli-ni-funzo-kwa-wengine.html#post14528771
 
Weka akiba ya maneno.

Kuchaguliwa (kutangazwa kuwa mshindi) kwa Dr. Pombe Magufuli kunaleta funzo (fundisho) moja tu nalo ni
kuwa Tanzania inahitaji Tume huru ya uchaguzi na Katiba ya wananchi.

Wakati mnaingia kwenye uchaguzi hamkujua kama tume ni huru ama la? Acheni kujitoa ufaham nyinyi.
 
gape la kura million 2! na bado unadai umeibiwa
Hiyo gap imepatikana kihalali au kwa kuchakachua matokeo?

CCM haiwezi kushinda uchaguzi wowote utakaosimamiwa na tume huru ya uchaguzi. Wananchi wamechoka na "maisha bora" na "maendeleo" yaliyoletwa na serikali zinazoongozwa na CCM.
 
Hiyo haitatokea kwa tume hizi NEC na ZEC kama zilivyo
Unafikiri kuna uwezekano kwa Tume za uchaguzi Tanzania kumtangaza mshindi mgombea wa upinzani?

Hilo lingefanyika Zanzibar ambako Tume imefuta uchaguzi ili kutengeneza mazingira ya CCM ishinde.

Unaweza kunisaidia kufahamu ni kwa nini NEC na ZEC zote zilitanganza majimbo ambayo CCM inaonesha kushinda kwa muda mrefu na yale ya upinzani kucheleweshwa kutangazwa?
Magufuli ameongoza majimbo 218 kati ya 264, kwa hesabu ndogo ni katika kila majimbo 6, Magufuli anaongoza majimbo 5, sasa sijui Nonda we ulitaka hayo majimbo anayo ongoza EL yatoke wapi ? Au ulitaka waanze kutangaza Kilimanjaro na Arusha tu ?
 
Last edited by a moderator:
Hakika ni fundisho kwa watengeneza mitandao ya kwenda ikulu kisa wana viroba vya pesa , ,kazi, uadirifu,kujituma kuwatumikia watu ndo KUWA kigezo cha kupata viongozi,
Kabisa mkuu, kuna watu wanahisi wakiwa na pesa basi kila wanalotaka linakuwa. Shame on Them.!
 
Hiyo haitatokea kwa tume hizi NEC na ZEC kama zilivyo
Unafikiri kuna uwezekano kwa Tume za uchaguzi Tanzania kumtangaza mshindi mgombea wa upinzani?

Hilo lingefanyika Zanzibar ambako Tume imefuta uchaguzi ili kutengeneza mazingira ya CCM ishinde.

Unaweza kunisaidia kufahamu ni kwa nini NEC na ZEC zote zilitanganza majimbo ambayo CCM inaonesha kushinda kwa muda mrefu na yale ya upinzani kucheleweshwa kutangazwa?

Nonda,
Kuwahi au kuchelewa kutangazwa kwa jimbo ni hoja nyepesi.

Nitakubaliana na wale wote wanaosema kuwa Ukawa wameibiwa kura katika majimbo yao tu nitakapoonyeshwa fomu ya matokeo ya jimbo inayotofautiana na kilichotangazwa na NEC. Na hizi fomu ziko nyingi kwani kila mgombea ubunge na wakala wake anayo nakala.

Kutangazwa wa kwanza au wa mwisho kama NEC hawajabadili matokeo sio hoja ya msingi.
 
Magufuli ameongoza majimbo 218 kati ya 264, kwa hesabu ndogo ni katika kila majimbo 6, Magufuli anaongoza majimbo 5, sasa sijui Nonda we ulitaka hayo majimbo anayo ongoza EL yatoke wapi ? Au ulitaka waanze kutangaza Kilimanjaro na Arusha tu ?
Kwa hiyo Majimbo ya upinzani yalitangwazwa kwa kucheleweshwa na mwishoni kwa bahati mbaya?

Unaongeleaje juu ya umuhimu wa kuwa na Tume huru ya uchaguzi?
 
Wakati mnaingia kwenye uchaguzi hamkujua kama tume ni huru ama la? Acheni kujitoa ufaham nyinyi.
CCM imengia kwenye uchaguzi ikijua kuwa Tume ya uchaguzi ni huru?

Je kwa ufahamu wako tume ya uchaguzi ni huru?
 
Hiyo gap imepatikana kihalali au kwa kuchakachua matokeo?

CCM haiwezi kushinda uchaguzi wowote utakaosimamiwa na tume huru ya uchaguzi. Wananchi wamechoka na "maisha bora" na "maendeleo" yaliyoletwa na serikali zinazoongozwa na CCM.

Nonda, tuelezee basi wamechakachua jimbo gani na kura ngapi ?
Ukimaliza tuambie na EL amefikisha vipi hizo 10m votes ?
Sio lazima kila sehemu utumie mahaba, sehemu nyingine tumia akili mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Miezi kama minne iliyopita ni watu wachache sana waliokuwa wakiamini kwamba Dr Magufuli atakuja kuwa Rais wa nchi yetu, Hii ilitokana na mfumo uliokuwepo huko nyuma wa kuchagua mgombea ku-base zaidi kwenye makundi ndani ya Chama na umaarufu wa mgombea.

Kilichomwibua Dr Magufuli ni record yake ya uchapakazi, uadilifu, kutoyumbishwa hovyo hovyo kwa sababu ya kusimamia kile anachokiamini kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla, Hiyo imejidhihirisha zaidi katika wizara zote alizowahi kuziongoza mfano Ujenzi na Miundombinu pamoja na Kilimo na ufugaji.

Fundisho tunalopata hapa ni kwamba usingoje mpaka upewe nafasi kubwa ya utumishi ndio uanze kuonyesha namna ya kuwatumikia wananchi. Piga kazi tu hata kama huna cheo chochote, usingoje mpaka uwe Waziri, Mbunge, M /"kiti serikali ya mtaa, nk

WASIPOKUONA BINADAMU MUNGU ATAKUONA NA KUKUINUA TU.

mimi nadhani Magufuli kapata urais kutokana na katiba. Hata kama angepigiwa kura 5 la zima angetangazwa mshindi na hakuna mtu yeyote kuhoji. Kiuhalisia hakustahili, tusubiri matokeo ya 'kazi tu'. 5yrs sio issue sana. count down ina'za kesho.
 
Back
Top Bottom