Urais si Makinda tu, Tibaijuka, Migiro nao wamo kwenye mbio hizo kuelekea 2015

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
Mashambulizi yatolewa kwa Spika
Anne%20Makinda.jpeg

Spika wa Bunge,Anne Makinda.

Watu na taasisi kadhaa wamekosoa hatua ya baadhi ya wabunge kumpigia debe Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuwa anafaa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Waliommwagia sifa Makinda ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya, na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Anna Abdallah.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema ProfesaMwandosya na Anna Abdallah walichokifanya ni kutoa maoni yao, ambayo ni haki yao kikatiba.

Hata hivyo, alisema kutokana na siasa za sasa hivi, hawakusoma alama za nyakati ndiyo maana tangu walipotoa maoni hayo, mwitikio wa wananchi umekuwamdogo.

Alisema Makinda hawezi kuvaa viatu vya urais akamudu kupambana na wagombea wengine wa nafasi hiyo.

Dk. Bana alisema wanawake wanaofaa kuwania nafasi hiyo ni wawili; Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Asha-Rose Migiro.

Alisema hiyo ni kwa sababu sehemu zote walizozipitia, ikiwamo Umoja wa Mataifa (UN) na Uwaziri, walifanya kazi vizuri na walikubalika.

"Wanaweza kugombea kwa tiketiya CCM na wakapambana na upinzani," alisema Dk. Bana.

Alisema tofauti na Profesa Tibaijuka na Dk. Migiro, Makinda ataondoka bila ya kuwa na mvuto wowote kwa wananchi kama alivyoondoka Msajili mstaafu wa Vyama vya Siasa, John Tendwa.

KAULI YA KLFT
Askofi Mkuu wa Kanisa la Furaha Tanzania (KLFT), Jones Mola, alisema wao kama kanisa hawawezi kukubali wanasiasa wakawachagulia Watanzania mkuu wa nchi wanayemtaka wao, badala yake aliwashauri waumini wao kuwakataa na kumchagua mtu mwenye maoni na anayeweza kuliongoza taifa pasipo kupigiwa debe.

"Baadhi ya wanasiasa wameanza kuwatafutia Watanzania mkuu wa nchi ajaye wakati wakishawishi kwamba kwa hali ilivyo fulani ndiye anayestahili kubeba mikoba wa Tanzania katika uchaguzi wa mwaka 2015," alisema na kuongeza:

"Hatutaki na tunawashauri waumini wetu kumchagua mtu wanayemtaka, lakini siyo kupigiwa debe kabla ya wakati."

MSIMAMO WA BAMAKITA
Baraza la Maadili la Kiislamu Tanzania (Bamakita) limetoa kauli ya kupinga kitendo cha vigogo hao, ambao wanaaminikakuwa na ushawishi ndani ya CCM, kumpigia debe Spika Makinda kuwa Rais wa Tanzania.

Kauli hiyo ya Bamakita ilitolewa na Mwenyekiti wake, Sheikh Athumani Mkambaku, kupitia taarifa yake ya maandishi, iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari, jijini Dar es Salaam.

"Baraza letu linapinga vikali ushauri uliotolewa na Anna Abdallah na Profesa Mwandosya unaomtaka Spika Makinda agombee urais wa Tanzania 2015," alisema Sheikh Mkambaku na kuongeza:

"Tunaupinga ushauri huo kwa kuwa sisi tunamuona Spika Makinda si mtu anayefaa kuwa Rais wa nchi yetu na kwamba, hata hiyo nafasi ya Uspika aliyonayo ameshindwa kuimudu na hiyo inaonyesha wazi kuwa waliotoa maoni hayo hawana nianjema na nchi hii."

Sheikh Mkambaku alisema Makinda ameonyesha udhaifu na upungufu mkubwa katika uongozi wake wa uspika na amewafanya Watanzania kupoteza hata hamu ya kuangaliana kusikiliza Bunge.

Alisema hali hiyo imetokana na Bunge linaloongozwa na Spika Makinda kuwa kama kijiwe cha kahawa kwa zogo, kashfa, vijembe na kukosekana kwa nidhamu.

"Kila mbunge anaweza kuwasha kipaza sauti na kuzungumza chochote atakacho," alisema Sheikh Mkambaku.

Alisema hali hiyo imefikia hapo kutokana na udhaifu wa Makinda kama spika, ambaye ameshindwakutenda haki na kuisimamia kwa maslahi ya Watanzania, badala yake amekuwa mtetezi mkubwa wa serikali, wakati hiyo siyo kazi yake.

"Hivyo, tunaamini kuwa hataiweza kazi ya urais, kwani kama ameshindwa kulisimamia Bunge tu kiuadilifu, je, ataweza kuisimamia nchi nzima?" alihoji Sheikh Mkambaku.

Alisema Makinda alipaswa kuiga mfano wa mtangulizi wake, Samuel Sitta, ambaye alisema wakati akiwa Spika, aliendesha Bunge lenye kasi na viwango na bungeni hakukuwa na vurugu wala wabunge wa upinzani hawakuwahi kulalamika kwambawanabanwa.

Sheikh Mkambaku alisema hali hiyo ilitokana na ukweli kwamba,Sitta alikuwa anafanya kazi yake kwa uadilifu na kwa maslahi ya wananchi na wala siyo kulinda maovu ya baadhi ya viongozi wa serikali kwa kuwazuia wabunge wasipate nafasi za kuchangia au kuwatoa nje ya Bunge.

Aliwashauri wanaCCM kuwa makini na tabia iliyoanza kujitokeza miongoni mwao ya kila kiongozi wa chama hicho kujiona anafaa kuwa Rais.

"Ukweli ni kwamba urais ni nafasi nyeti, ambayo kwanza haihitaji mtu dhaifu asiyekuwa muadilifu, hasa huyo wa 2015 kwa kuwa atakuta nchi ikiwa imeharibika sana kimaadili, kukithiri rushwa, kushamiri kwa uuzwaji wa dawa za kulevya, matumizi mabaya ya fedha za umma kama yale yaliyofanywa naviongozi wa bandari ya kujilipa mabilioni kama posho ya vikao, ujambazi, maaskari feki na ujangili," alisema Sheikh Mkambaku.

LHRC YANENA
Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezo wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia, alisema Makinda anazo sifa za kugombea Urais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema Makinda ana miaka zaidi ya 40 kama katiba inavyotaka, lakini pia hajawahi kukutwa na kosa la jinai ikiwamo kukwepa kulipa kodi ya serikali.

Aliongeza kuwa suala la kuchaguliwa na wananchi ni suala lingine na kwamba sifa za msingi za kuteuliwa na chama chake kugombea kiti cha Rais anazo.

Alhamisi iliyopita Anna Abdallah na Profesa Mwandosya walimpigia debe Makinda ndani ya ukumbi wa Bunge, huku wakimmwagia sifa za kuwa anafaa kuwania urais wa Tanzania.

Anna Abdallah alimmiminia sifa Makinda alitoa kauli ya kuunga mkono hoja ya Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Afrika (CPA) tawi la Tanzania, Mussa Azzan Zungu, kumpongeza Spika Makinda kwa kuteuliwa kwake kuwa Rais wa chama hicho kandaya Afrika.

Alisema kwa msingi huo, anamshauri Spika Makinda kutokana na kuwa na uzoefu wa kutosha ndani na nje ya nchi kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kwa upande wa Profesa Mwandosya, ambaye pia ni Mbunge wa Rungwe Mashariki (CCM), alisema Spika Makinda amekuwa mfano mzuri wa kuigwa kutokana na uongozi wake tangu akiwa mkuu wa mkoa, mbunge, naibu waziri, waziri kamili, naibu spika na sasaspika.

Profesa Mwandosya alimwelezea Spika Makinda kuwa ni mtu mwadilifu, mtenda haki, anayejiamini, mvulimivu, mnyenyekevu, msikivu na mwenye msimamo, hivyo hashangai kupitia yeye (Spika), Bunge lijalo hata bila ya Katiba mpya, wanawake watafikia asilimia 55 katika Bunge.

Alisema hiyo inatokana na ukweliwa historia yake ya kiungozi wasichana wengi sasa wanataka kuwa viongozi, lakini pia wanawake wengi watajitokeza kugombea ubunge.

Hata hivyo, Profesa Mwandosya hakutaja moja kwa moja kama Spika Makinda anapaswa kugombea urais mwaka 2015, isipokuwa alisema kwa wale wanaofikiria 2015 watambue kwamba (Makinda) ni tishio kwao.

Habari za watu wanaoutaka urasikupitia CCM zimepamba vyombo vya habari kwa kitambi sasa, katika wanaotajwa ni pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta; Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Mwaka 1995 wakati kwa mara ya kwanza Kikwete na Lowassa walijitokeza hadharani kwa pamoja wakiendesha harakati za kuwania urais, Makinda naye alikuwa miongoni mwa makada wa CCM waliokuwa pamoja nao na alifika uwanja wa ndege siku wawili hao (Kikwete na Lowassa)walipokodi ndege kutoka Dar es Salaam kwenda kuchukua fomu za kuwania urais kupitia CCM makao makuu Dodoma.

Ingawa haijawekwa wazi juu ya harakati za kisiasa za Makinda, wakati anawania nafasi ya uspikahakuna aliyejua kuwa ana mpango huo, hadi vyombo vya habari vilipofichua kwamba naye alikuwa amejitokeza kuchukua fomu kimya kimya.

Uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM chini ya Rais Kikwete, kupitisha uamuzi kuwa nafasi ya spika ilikuwa zamu ya mwanamke, ulimbeba Makinda dhidi ya bosi wake Sitta.

Imeandikwa na Muhibu Said, Richard makora, Raphael Kibiriti, Dar na Godfrey Mushi, Moshi.
Mwisho..

CHANZO: NIPASHE
 
Nyie piganeni vikumbo weeee mpaka mchoke,CDM tutamkabili yeyote atakayeteuliwa kutoka ukoo wa PANYA-CCM!
Tunawasubiri 2015! WEZI wakubwa nyie!
 
...Naona magamba sasa yana kazi ya kupima uzito kumtafuta atakayeweza kubalance na hevyweight wa CHADEMA.
Poleni magamba.
 
Mashine nzito ya Africa na Dunia kwa ujumla hawezi kabidhiwa kwa Makinda, Lowassa, Salim au Mkapa tena
 
Tibaijuka ameshindwa kutatua matatizo hapo wizara ya ardhi na kukomalia mradi wa kigamboni tu wakati wananchi wamempelekea malalamiko chungu nzima yakuyashuhulikia!! Tibaijuka sio msikivu wa shida za watu na wala hazijali na ndio maana kwa sirisiri akapandisha land rent bila kufikiria hali ya uchumi wa wananchi. Hafai hata siku moja kuongoza nchi hata umri na afya yake vinamsuta!!
 
Kwangu mm naona hawezi

maana Bunge tu linamshinda

ataweza kupambana na kina silaa

huyo?au anamuona kikwete rais

anafkr ni rahc tuu, mara mia ya

migiro asha rose kidogo kakaa

un, ila makinda hawez , yeye anajua kutetea chama tuu
 
"Kwa CCM, rais tumchaguaye ni Mwanamke." Ndivyo itakavyotamkwa kwenyekikao cha NEC. Kama ilivyokuwa wakati wa uchaguzi wa Spka!
 
wote wanaomuona bi kiroboto kuwa presidential material wana ubongo ulojaa virusi kama taahira mmoja wa JF anayejiita Zemacopolo.Yule mama hafai hata kuwa monitress wa form one sembuse urais!!!
 
Back
Top Bottom