Urais 2015, Walimu wamuunga mkono Lowassa

Urais 2015, Walimu wamuunga mkono Lowassa

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
437
Umoja wa vuguvugu la mabadiliko ya walimu Tanzania, limesema linamuunga mkono Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, kugombea urais wa awamu ya tano....

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, walimu hao walisema wameamua kumuunga mkono Lowassa kwa kuwa wanaamini akipata nafasi ya urais atafanya mambo mazuri sana hususani katika sekta ya elimu..

Mwenyekiti wa umoja huo, Ally Umakuli, alisema wanaamini kwamba Lowassa atafanya mambo makubwa akiingia madarakani kwa kuwa hata kipindi akiwa Waziri Mkuu alifanya mambo makubwa ikiwemo kujenga shule za sekondari kila kata na hivyo kuimarisha ajira kwa walimu...

Sababu ya pili, alisema kati ya waliojitokeza kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo mpaka sasa, hakuna aliyejitokeza na kuonyesha vizuri namna ya kuipa kipaumbele sekta ya elimu na uhakika wa maslahi kwa walimu kama alivyoeleza Lowassa....

Tatu, walisema Lowassa ni mtia nia pekee mpaka sasa ndiye anaonyesha kuwa mshirika katika matatizo mbalimbali ya kutatua changamoto za walimu na elimu, na kwamba mwaka 2013 alishiriki katika harambee ya madawati katika shule za sekondari za tarafa ya Mbagala na kufanikisha kupatikana madawati 800 na zaidi, pamoja na kushiriki kutunisha SACCOSS ya Mkoa wa Kilimanjaro ambayo zaidi ya billioni moja zilipatikana...

Pia walisema, Lowassa alisimamia ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na pia wanamwamini kwamba atasaidia katika sekta ya elimu kuliko mgombea yeyote yule, ana mapenzi ya dhati kwa walimu.....

Walisema wanamwamini kwamba akiwa rais posho za walimu, nyumba, vifaa vya kufundishia, malipo ya madeni pamoja na ongezeko la mishahara litashughulikiwa ipasavyo.... Pia Ndg Ally alisema wanaamini hata maduka maalum ya walimu yataanzishwa kama ilivyo kwa wanajeshi na askari polisi....

"Matatizo ya walimu nchini yapo kila kukicha hakuna suluhisho badala yake ni maneno tu, walimu tumedhamiria kwa dhati kwamba sauti ya rais ambayo leo hii tumeitangaza ni sahihi na itatusaidia, tumefanya ili ajue kabisa kwamba tuko nyuma yake katika kufikia lengo lake ili atutatulie kero, matatizo na changamoto mbalimbali za walimu na tumeamua kufanya hivi wakati tunaelekea kumpata rais mpya tukijua kwamba tutatumia haki ya kupiga kura ya kimakubaliano ya maslahi yetu walimu wote" alisema.


Chanzo: NIPASHE, 4.06.2015
 
Mwaka huu na huyo panya wenu mtakoma,umeshasema labda atoboe mtungi asepe..ila akisubiri tuje tuinamishe mtungi na tumtoe wenyewe msilaumu.....kama hamjui kusoma basi angalieni hata picha.
 
Hivi, ndiyo hawa waalimu waliokuwa wakitaabika wakati wa enzi zake kama PM aliposema "hata kama nyasi tutakula"( lakini ndege ya Rais inunuliwe?"
 
Shule aliyosoma pale Monduli ina hali mbaya angeanza nayo hiyo tungeelewa kuwa anakerwa na tatizo la elimu nchini
 
Hivi, ndiyo hawa waalimu waliokuwa wakitaabika wakati wa enzi zake kama PM aliposema "hata kama nyasi tutakula"( lakini ndege ya Rais inunuliwe?"


Hapa hata kama angekuwa ibilisi, kasingiziwa, maneno haya kama sijakosea yalisemwa na Basil Mramba akiwa mtumishi wa Ben Mkapa na ndipo ndege ilinunuliwa JK na swahiba wake waliikuta ikiwa imenunuliwa
 
Walimu gani wajinga wanaosema lowassa kajenga chuo cha dodoma
 
Nadhani Lowassa ndie atakuwa Rais kuanzia miezi michache ijayo.
Anaungwa mkono na wengi
 
Mi mwalimu af simkubali hata chembe... na huo umoja mnaouanzisha et umoja wa walimu komeni, lini tulikubaliana huo upuuzi...,, walimu wa kiivo wameshastaafu tuliobaki hatuna hizo swagger....acheni kutukera
 
acha uzushi unafikiri tumezaliwa leo ,ndege ilinunuliwa na Benja PM alikuwa sumaye aibu zako
Hivi, ndiyo hawa waalimu waliokuwa wakitaabika wakati wa enzi zake kama PM aliposema "hata kama nyasi tutakula"( lakini ndege ya Rais inunuliwe?"
 
Mtaanzisha sana hizo umoja zenu mi mwalimu na walimu wote hawaungi mkono mgombea yeyote toka ccm wote ni wale wale
 
Huyu mwalimu ni team Lowassa mwenyewe tu asiwashawishi wenzake kumuunga fisadi
 
Hivi, ndiyo hawa waalimu waliokuwa wakitaabika wakati wa enzi zake kama PM aliposema "hata kama nyasi tutakula"( lakini ndege ya Rais inunuliwe?"

Hivi hata humwogopi mungu au hujui unachokisema...hv ndege ya raisi ilinunuliwa awamu ya nne..mijitu mingine bwana...hv kwa nn jf isije na utaratibu wa kuwaondoa watu kama haea humu....lijitu linaandika tu hata kama halina uhakika na linachoandika...muradi limeandika...nachukia mijitu kama hii mimi....
 
Back
Top Bottom