babalao 2
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 5,426
- 3,308
Makamu Mwenyekiti wa CCM ndg. Philip Mangula amekerwa na kauli ya mh. Sitta ya kutangaza NIA yake ya kuutaka Urais.
Mangula alisema kitendo alichofanya Sitta cha kujitangaza hadharani si kizuri na wote wanaojipitisha kuutaka Urais Hakika watakatwa majina yao wakati ukifika wa kuwapata wale watakaoingia kwenye mchakato wa kumpata mteule wa CCM.
Amewaasa ya kwamba muda wa Rais Kikwete bado haujaisha hivyo washirikiane kutekeleza Ilani ya CCM kwanza ili kuepuka kuenguliwa kwa kujitatangazia nia Mapema.
(Ikumbukwe wiki jana mh. Sitta alisema kwa hali ilivyo sasa yeye ndiye anafaa kuwa RAIS wa Tanzania kwani ana sifa ya kuwa Rais na Wananchi Wengi wanamtaka na kumsungumzia yeye kupewa dhamana hiyo).
Haya wataalamu wa demokrasia mnasemaje kwa hili?
Mbona Zitto alipotangaza Nia watu wa chama chake walivyosema si sahihi kwa muda huu CCM WAlisema NI HAKI YAKE KIKATIBA JE KWA CCM SI HAKI YA KIKATIBA KUTANGAZA NIA MAPEMA?
Source: Magazeti ya leo
==================
Kutoka Mwananchi
Mangula: Wanaojinadi kugombea urais CCM wanajiondolea sifa
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula amesema kada yeyote wa chama hicho anayejinadi sasa kuwa anafaa kuwa Rais ajaye, anajiondolea sifa ya kuwania nafasi hiyo ndani ya chama.
Mangula alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa.
"Siyo urais tu, hata hao wanaopita na kuonyesha nia ya kuwania nafasi za ubunge na udiwani katika majimbo mbalimbali yanayoshikiliwa na wanaCCM, hawatateuliwa na sekretarieti ya chama kuwania nafasi hizo," alisema. "Rais wetu wa sasa ni Jakaya Kikwete, huyu ndiye Rais hadi 2015.
Pia tunao wabunge na madiwani walioapa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM hadi mwaka 2015. Huyo anayepita sasa na kufanya kampeni kwa lengo la kuwania nafasi hizo anatumia ilani gani? Msimamizi wa Ilani iliyopo sasa yupo na bado hatujaandaa ilani nyingine," alisema Mangula na kuongeza:
Aruhusu kampeni majimbo ya upinzani
Mangula alitoa ruksa kwa wanachama wa CCM kuanza kampeni kwenye majimbo yanayoshikiliwa na upinzani akisema ni sahihi.
"Unapita kwenye jimbo linaloongozwa na Mbunge wa CCM unatumia ilani gani? Lakini kwa majimbo yanayoongozwa na wenzetu huko piteni," alisema Mangula. Alieleza madhara ya wanaCCM kuanza kampeni kwenye majimbo yanayoshikiliwa na makada wenzao kuwa ni pamoja na kuzalisha makundi ndani ya chama hicho tawala. "Makundi ni sumu na yanaleta mgawanyiko wenye madhara makubwa kwenye chama," alisisitiza.
Ashangaa Iringa kuwa upinzani
Katika hatua nyingine, Mangula alieleza kushangazwa na Jimbo la Iringa Mjini kuongozwa na upinzani akihoji ni pepo gani lililotokea. Aliagiza wanachama wa CCM kujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao ili kulirudisha mikononi mwao.
Aondoka uwanjani kiaina
Muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano huo Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM, aliondolewa uwanjani hapo katika mazingira ya kutatanisha baada ya kuhofiwa kuwapo kwa kundi la watu waliojianda kufanya vurugu.
Mangula alibadilishiwa njia tofauti na msafara wake ulioelekea ofisini mara baada ya mkutano wake kumalizika, baada ya kuwapo taarifa za kuwepo vurugu.
======================
PAMOJA DAIMA.