Urais 2015 kupitia CCM: Mangula amshukia Samwel Sitta...

Urais 2015 kupitia CCM: Mangula amshukia Samwel Sitta...

Makamu Mwenyekiti wa CCM ndg. Philip Mangula amekerwa na kauli ya mh. Sitta ya kutangaza NIA yake ya kuutaka Urais.

Mangula alisema kitendo alichofanya Sitta cha kujitangaza hadharani si kizuri na wote wanaojipitisha kuutaka Urais Hakika watakatwa majina yao wakati ukifika wa kuwapata wale watakaoingia kwenye mchakato wa kumpata mteule wa CCM.

Amewaasa ya kwamba muda wa Rais Kikwete bado haujaisha hivyo washirikiane kutekeleza Ilani ya CCM kwanza ili kuepuka kuenguliwa kwa kujitatangazia nia Mapema.

(Ikumbukwe wiki jana mh. Sitta alisema kwa hali ilivyo sasa yeye ndiye anafaa kuwa RAIS wa Tanzania kwani ana sifa ya kuwa Rais na Wananchi Wengi wanamtaka na kumsungumzia yeye kupewa dhamana hiyo).

Haya wataalamu wa demokrasia mnasemaje kwa hili?

Mbona Zitto alipotangaza Nia watu wa chama chake walivyosema si sahihi kwa muda huu CCM WAlisema NI HAKI YAKE KIKATIBA JE KWA CCM SI HAKI YA KIKATIBA KUTANGAZA NIA MAPEMA?

Source: Magazeti ya leo

==================
Kutoka Mwananchi

Mangula: Wanaojinadi kugombea urais CCM wanajiondolea sifa

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula amesema kada yeyote wa chama hicho anayejinadi sasa kuwa anafaa kuwa Rais ajaye, anajiondolea sifa ya kuwania nafasi hiyo ndani ya chama.

Mangula alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa.

“Siyo urais tu, hata hao wanaopita na kuonyesha nia ya kuwania nafasi za ubunge na udiwani katika majimbo mbalimbali yanayoshikiliwa na wanaCCM, hawatateuliwa na sekretarieti ya chama kuwania nafasi hizo,” alisema. “Rais wetu wa sasa ni Jakaya Kikwete, huyu ndiye Rais hadi 2015.

Pia tunao wabunge na madiwani walioapa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM hadi mwaka 2015. Huyo anayepita sasa na kufanya kampeni kwa lengo la kuwania nafasi hizo anatumia ilani gani? Msimamizi wa Ilani iliyopo sasa yupo na bado hatujaandaa ilani nyingine,” alisema Mangula na kuongeza:

Aruhusu kampeni majimbo ya upinzani

Mangula alitoa ruksa kwa wanachama wa CCM kuanza kampeni kwenye majimbo yanayoshikiliwa na upinzani akisema ni sahihi.

“Unapita kwenye jimbo linaloongozwa na Mbunge wa CCM unatumia ilani gani? Lakini kwa majimbo yanayoongozwa na wenzetu huko piteni,” alisema Mangula. Alieleza madhara ya wanaCCM kuanza kampeni kwenye majimbo yanayoshikiliwa na makada wenzao kuwa ni pamoja na kuzalisha makundi ndani ya chama hicho tawala. “Makundi ni sumu na yanaleta mgawanyiko wenye madhara makubwa kwenye chama,” alisisitiza.

Ashangaa Iringa kuwa upinzani
Katika hatua nyingine, Mangula alieleza kushangazwa na Jimbo la Iringa Mjini kuongozwa na upinzani akihoji ni pepo gani lililotokea. Aliagiza wanachama wa CCM kujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao ili kulirudisha mikononi mwao.

Aondoka uwanjani kiaina
Muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano huo Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM, aliondolewa uwanjani hapo katika mazingira ya kutatanisha baada ya kuhofiwa kuwapo kwa kundi la watu waliojianda kufanya vurugu.

Mangula alibadilishiwa njia tofauti na msafara wake ulioelekea ofisini mara baada ya mkutano wake kumalizika, baada ya kuwapo taarifa za kuwepo vurugu.


======================

PAMOJA DAIMA.

nashindwa kumuelewa mangula,keli huyu ni mangula kweli(kwetu karagwe,kitu ambacho ni fake kinaitwa 'mangula' mfano 'esabuni ya mangula'nk. hoja yangu ni kwamba,wanaoutaka urais hawasemi wanautaka kabla ya 2015,sasa kusema eti wanaotangaza waache kwa sababu kikwete bado ni rais na hajatoka madarakan mantiki iko wapi?kingine unapowazuia watu wasianze kujitangaza kuwania nafas mbalimbali eti wasubiri wakati ukifika,lakin wakati huohuo unawarahusu wengiene wanaotaka majimbo ya upinzan waanze kupiga kampen kwan hao wa upinzan wako kiaharamu??mangula acha ndimi mbili,ndo maana uliitwa chichidodo.lakin pia mangula nikuulize swali, hivi vyama vya upinzan viliruhusiwa na serikali ya ccm? ccm si ndo mnatamba kuwa mmekuza demokrasia nchini?sasa kwanin mnaviaharrass?kama vinavunja sheria ya vyama vya siasa si muvifute kama sheria inavyoelekeza?acha uchichidodo mr 'fake' yaan 'mangula' ya kihayakinyambo/kinyankole
 
Haya tuwakaribishe wale walioshupalia kuwa CDM hamna demokrasia zaidi yule mdau aliyeanzisha thread ya kwa nini unaipenda CDM..akidai mwenyewe anaipenda CCM kwani kuna Demokrasia tofauti na CDM akatolea na mfano wa Zuberi..haya tunawafungulia jimwageni na demokrasia hiyo,ni wakati wenu kujidai sasa[/QU
we nawe mbishi,hujaona tofauti hapo? Ya cdm yalikuwa mwenyekit kumtaja mgombea wakati hakujafanyika uteuzi na cdm kumpiga jungu zuberi ndo lilikuwa tatizo langu,mangula kakataa kujipitisha na kuandaa makundi kwakuwa yataleta migogoro.
 
Mzee Mangula unaweza kuwa na hoja. Tatizo langu ni kwamba hao viongozi hawaombi nafasi ndani ya chama bali nafasi za kuongoza wananchi wote, wanaccm na wasiokuwa na vyama. Sasa wasipojitokeza mapema, wananchi wengine watawezaje kuwapima, au ndio kuuziwa mbuzi ndani ya gunia. Sehemu zote duniani ambazo demokrasia ya vyama vingi ina nguvu suala la wakati gani mgombea ajitokeze hadharani ni uamuzi binafsi baada ya kupima faida na madhara yake. Kauli ya Mangula inarudisha nyuma hata demokrasia ndani ya chama kwa kuendeleza kulea dhana ya zidumu fikra za mtu mmoja.

Ashauriwe achungulie kule Mtwara na Masasi ajue kuwa zama za fikra za mtu mmoja bila kujali wadhifa wake katika chama au taifa zinaanza kukataliwa na wanachama na wananchi. Bahatri mbaya alikuwa busy huko Mwanza, Bukoba na Iringa kutambua yanayoendelea huko kusini! Anaweza kusamehewa kwa hilo. Hata hivyo la msingi ni kukubali kubadilika vinginevyo tutakumbwa na kila aina ya matatizo katika kuongoza (kutawala) nchi na hata chama. Tafakari.
 
OLe wake Mangula athubutu kulikata JINA la Sitta, kwa kisingizio chochote kile, atakuwa ameisambaratisha CCM.

chaguo la ccm 2015 ni mwanamke, naye ameisha anza kupigiwa kampeni na ccm.
 
Kama kawaida Muongo husaau kile akisemacho. poleeee ccm. Enedeni kwa amani mtuachie kanchi ketu mnakosema masikini.
 
Wazo lako ni zuri, lakini mpaka pawepo na makubaliano hayo.Watu wote waelewe hivyo na pawe na kipindi maalum walichokubalia wote. Ni kama mchezo wa mbio: Get ready. On your mark. Goooo? Sio wenzako hawajawa kwenye alama wewe unaanza kukimbia.Mapema pia iwe na kipimo: Miezi mingapi, miaka mingapi? Wote waelewe na wawe na mizania sawa. Hatukatai kujitangaza, lakini lini? Hii ndiyo hoja
Mimi naunga mkono wale wote wanaojitangaza mapema kuwania kiti cha uraisi hasa kupitia ccm ukizingatia raisi kikwete anamaliza muda wake. Mtu kutangaza nia ni jambo zuri ili wanachama wa ccm na watz kwa ujumla wawe na nafasi ya kujadili kama kweli huyu mtu anasitahiri kuliongoza taifa hili. Watz lazima watambua kuwa si kila mtu anaweza kuwa raisi. Kuna viongozi uwezo wao wa kuongoza unaishia kuwa waziri na sio raisi. Ukimpa uraisi anachemsha na nchi inaweza kuyumba kama sio kuingia ktk machafuko. Mifano hiko mingi hasa barani Afrika. Kwahiyo pamoja na kanuni na taratibu za vyama kwa wanachama wanaohitaji kugombea uraisi ni muhimu ukatolewa uhuru mkubwa kwa raia kuwajadili mapema wale wote wenye nia ya kugombea uraisi.
 
Sita hana ujanja hata jina likikatwa maake tulishaona jina likikatwa wakati wa uspika na akaendelea kuwalamba miguu mafisadi!
 
Kwa jinsi Kikwete alivyoongoza nchi kisanii naona kila mtu anaona urais ni kazi rahisi ndio maana kila mtu anatangaza kuwania urais,
 
Back
Top Bottom