Miaka ya hivi karibuni kumekuwepo hoja ya uraia wa nchi mbili, ''Dual Citizenship'' kutoka miongoni mwa baadhi ya Watanzania. Hoja hii ilipata msukumo wa kufikishwa bungeni, kwa bahati nzuri haikupata fursa ya kujadiliwa lakini hata hivyo bado iko nia miongoni mwa Watanzania walioianzisha hoja hiyo kutaka kuiendeleza kwa kuiuwasilisha.
Ni bahati nzuri haikuwahi kupata fursa ya kujadiliwa kwa sababu suala la uraia ni nyeti mno kwa usalama wa taifa changa kisiasa, na tete kiuchumi tena lenye rasilimali nyingi kama Tanzania. Rejea sakata la vijisenti vilivyohifadhiwa katika nchi za kigeni na Mwanasiasa mwandamizi wa Serikali ya CCM-Andrew Chenge (MB).
Mheshimiwa huyu alikubali na kukiri kuwa alichohifadhi yeye ni vijisenti tu, akilinganisha na kilichohifadhiwa na wenzake kama inavyojiri sasa kupitia taarifa za vyombo vya habari juu ya mapesa yaliyofichwa katika mabenki ya Uswisi. Kwa sasa waporaji hawa wanalindwa na mfumo wa utawala wenye mahakama isiyo huru, endapo hoja ya uraia wa nchi mbili itajadiliwa na hatimaye kupitishwa kuwa sheria itatoa mwanya makhsusi kwa waporaji na wanyonyaji raia waliokosa uzalendo kama hawa na kupata mahala pa kukimbilia, huko kwenye nchi nyingine ambako nako watakuwa raia wanaostahili ulinzi na haki zote za kiraia kama huku, ambako wataishi bila bughudha wakitafuna mali waliokwishaipora kutoka Tanzania.
Hebu rejea tena sakata la wizi wa fedha za EPA katika BoT. Hadi sasa Watanzania wengi hatuamini kuwa aliyekuwa Gavana wa BoT, Dk. Ballali aliugua, kufa na kuzikwa huko Marekani alikopelekwa kutibiwa. Imani yangu ni kwamba baada ya kufanikisha uporaji ule, alikimbizwa na kufichwa nchini Marekani akiendelea kula bata bila khofu ya kushitakiwa.