Urafiki wa Wasambaa na Wakoloni wa Kijerumani

Franco Zetta

JF-Expert Member
Nov 3, 2014
1,661
843
Katika kupenda kwangu kudadisi mambo na kukaa na wazee wa zamani nilipata kupewa simulizi juu ya vita ambayo haiku andikwa sana ya Wasambaa na Wajerumani.

Ikumbukwe kwamba Chifu wa wasambaa miaka hiyo Kimweri ali jijengea heshima kubwa na milki kubwa iliyoenea mpaka ndani ya mji wa mombasa na akawa na majumbe(mazumbe) wake huko mathalani sehemu za mwatate ikiwa na maana ktk kisambaa kwa baba na Kimweri alitokea kuheshimiana sana na Sultani wa Unguja kukawa na mkataba wa kutochukua mtumwa ndani ya mkoa wa Tanga ila ikawepo idhini ya kupitisha Watumwa ktk bandari ya Pangani kazi iliyo simamiwa na Ibin Batuta na kupitia maelewano yao Sultani alimuuzia Kimweri bunduki ambazo zilimwezesha kupambana vikali na wajerumani kwenye uwanda kando ya mto unaoitwa Ruvu pale Korogwe.

Vita ilipo pamba moto Kimweri alibaini kazi ina kuwa ngumu kwasababu ya silaha walizo tumia Wajerumani kama viji mizinga vidogo vinavyo toa risasi nyingi ila havistahimili maji na Kimweri alijulikana kuwa na mikoba ya utaalam wa kushusha mvua hivyo aliondoka na kikundi cha wafuasi wake kwenda kwake Vuga kuleta mikoba na pengine angeweza kutuma watu ila huko kwenda kuleta hicho kilinge chake ili semekana haki ingii mtu tofauti na yeye.

Bahati mbaya Wajerumani wakajua kuwa ana ondoka wakiamini aidha ana kwenda kuongeza askari au kuleta silaha za maangamizi hivyo wakamfuata kumzuia,Kimweri alicho fanya kwanza ni kuvusha watu wake kwenye kasehemu kembamba zaidi ktk mto Ruvu kakuweza kurudi hatua moja tu kuruka na yeye akawa wa mwisho na kufanya makafara yake akapita Askari wa Kijerumani.

Kila aliye jaribu kuvuka alivutwa na kudidimia, bahati nzuri kabla haja rejea ilifanyika suluhu na kimweri alitumiwa ujumbe juu ya hilo aka wakaribisha Wajerumani na bahati mbaya hakurudi tena na ni yeye tu aliweza kutengua alicho fanya pale mtoni na mpaka sasa madhara yana tokea na ukifika pale wenyeji wana weza kukuelekeza na kwa ubishi ndugu zetu wa kimasai walisha poteza maisha.

Hapo ndio ulipoanza urafiki huo uliopo mpaka leo na kwa taarifa barabara toka Mombo kuelekea Lushoto hakuna msambaa aliye pinda mgongo pale ila watani zetu Wasukuma na Wanyamwezi na wakaloea kule wakaoa dada zetu wakataka kutuachia majina yao ya Maganga tukaya badili usambaani hadi leo kuna kina Mganga sio Maganga.

Kwa hiyo hadi leo Wajerumani ndio wanao husika na matengenezo ya barabara ile na mara ya mwisho ni kampuni ya JBG toka Ujerumani ndio ilifanya kazi hiyo na hata kwaya za matarumbeta asili ni hao jamaa.
 
mwandishi anajisifu kwa kumkaribisha locust wakati sie tunajisifu kwa kumpiga
 
Back
Top Bottom