WADADA STYLE MDADA 1: Hello mpenzi mambo MDADA 2: Niko poa sweety, dah umenikumbuka mamii MDADA 1: Yaani nimekumiss, nikaona nikupigie nikwambie leo naja kwako MDADA 2: Dah nitafurahi mno mpenzi, shosti navunja safari zangu zote nakusubiri MDADA 1: Basi baadae sweety tutaonana...........Akikata simu tu MDADA 2, anamwambia mdogo wake MDADA 2: Yule Malaya kafosi kuja kunitembelea sijui ana umbeya gani? Au kaishiwa anataka nijee nimnunulie bia za bure, ataula wa chuya halooooo WAKAKA STYLE MKAKA 1: We mwendawazimu uko wapi? MKAKA 2: Hii kali masikini bingwa wa kubip leo umepiga? Mkeo kakuruhusu leo ? MKAKA 1: Hivi kwanini hujafa watu tule pilau? MKAKA 2: Kufa sifi na leo nakuja kunywa bia bili yako, haya nikukute wapi? MKAKA 1: Pale kwenye baa anayonywea baba yako, usipokuja ntashukuru maana hela yangu ina masharti, hakuna kulipia masikini. Alipokata simu tu MKAKA 1 akamwambia mkewe, MKAKA 1: Yaani huyu jamaa, ni rafiki yangu toka utoto, tukikutana huwa raha sana, ngoja nikamtukane hukohuko bar.