Urafiki wa TCU na chuo cha St. Joseph

The dream

JF-Expert Member
May 10, 2015
999
994
Chuo cha st. Joseph (hasa kampasi za Songea na Arusha) kimekua kikikabiliwa na tatizo la migomo ya wanafunzi kwa muda mrefu sana, na baadhi ya madai ya wanafunzi ni haya;
•Chuo kutokua na mazingira ya chuo kikuu
•Chuo kutokua na walimu/lecturers wenye hadhi ya chuo(unqalified lecturers)
•Chuo kutokutoa elimu inayostahiki
•Wanafunzi kucheleweshewa mikopo yao na chuo(sio bodi ya mikopo)
•Chuo kutoza ada kubwa sana
•Wanafunzi kutoruhusiwa kufanya Special exams
•Chuo kutokua na ungozi imara
•N.k
Kutokana na matatizo hayo na mengine mengi tu mnamo mwezi uliopita katibu mtendaji wa TCU, Yunus Mgaya alitangaza kuvifutia usajili hivi vyuo vya St. Joseph Songea na Arusha na kusema wanafunzi wake watahamishiwa katika vyuo vingine kama Sua, Udom na Rucu.
**********************************
Kitu cha kushangaza ni hivi juzi katibu mtendaji wa TCU alipotamka kwamba wanafunzi wanaohamishwa kutoka vyuo hivi vya st. Joseph watalizimika kulipa ada ambazo walikua wanadaiwa na chuo hiki huko kwenye vyuo wanavyoenda na pesa hizo zitarudishwa St. Joseph!
Cha kujiuliza hapa wadau wa elimu ni hiki
1.TCU wamefuta vyuo hivi kwa sababu vilikua vinatoa Elimu isiyo na Ubora wa chuo kikuu, inawezekanaje wanafunzi watakiwe kuilipia tena wakati sio elimu stahiki?
2.Iwapo wanafunzi watashindwa kulipa watakataliwa kupokelewa huko vyuo wanapokwenda?
3.Wanafunzi wamepotezewa muda na fedha zao kwa kupewa elimu isiyo stahiki, je, St. Joseph watawalipa fidia wanafunzi?
4.Wazazi wa wanafunzi watakubali kulipa ada iliyokua imebaki wakidaiwa katika chuo kilichofungwa?
5.Wanafunzi wa vyuo hivyo wamelazimika kuuza vitu vyao kwa hasara ili kuhama, je st. Joseph itawafidia gharama hizo?
6.Ni halali wanafunzi kukilipa chuo ambacho kimefungwa na TCU kwa tatizo la kutoa elimu duni?
7.Kuna urafiki gani kati ya TCU na chuo hiki mpaka iamuliwe kwamba wanafunzi walipe ada za nyuma ambazo wanadaiwa ili hali walikua wakipewa elimu isiyo stahiki?
 
Hayo yote hapo mkuu ni sahihi lakn kwa tz ni ngumu xana!.
 
Huyu mgaya ndo jipu kabisa maana ni wao ndo walisajili vyuo bila kukidhi vigezo na ndo leo wanaovifuta.
Mgaya wewe,ungekuwa somalia,nigeria na falme za kiarabu..(........................)?.
Unachezea maisha ya watanzani kwa tamaaaa yenu?????.
 
Back
Top Bottom