Urafiki na huyu mke wa mtu uko hatiani

Urafiki na huyu mke wa mtu uko hatiani

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
37,287
Reaction score
55,902
Kuna dada mmoja nilisoma naye darasa moja miaka mingi iliyopita, tulikuwa hatuna mahusiano yoyote...zaidi ya hisia zake na zangu kuwa zinawasiliana tu. Wiki tatu hivi zilizopita, nilipokea simu kutoka kwake tukasalimiana na kujuliana hali, pamoja na kuniambia jitihada alizotumia kupata namba yangu. Yeye alishaolewa na anafamilia yake zaidi ya miaka 10. Ilitokea wamehama hama kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine kutokana na mazingira ya kazi. Ndani ya wiki tatu hizi tumewasiliana sana, naye anatumia nguvu nyingi sana kunipigia simu, kutuma sms n.k

Juzi, ndipo akaamua kuniambia changamoto alizonazo kwenye ndoa; mumewe amebadilika, akirudi nyumbani anamjibu kwa ukali, hakuna masikilizano, matumizi hatoi, mzee anawajali watoto tu, amekuwa hana thamani ndani ya nyumba zaidi ya kuonekana kama beki 3.

Nilijaribu kumpa ushauri wa hapa na pale, lakini naona uelekeo wake naye anatafuta pa kupunguzia msongo wa mawazo. Najaribu kufikiria huu ukaribu huu unaojisogeza, unaweza kusababisha kula tunda kimasihara, lakini hofu yangu nisije kuwa kikwazo kwenye familia yake au yangu. Na nikikata mawasiliano naye pale anaponipigia nahisi nitakuwa sijamtendea haki.

Wakuu mnanishauriji kwenye hili jambo?
 
ukimpa upenyo tu ndio unaharibu familia yake. yaani atahama mpaka kimwili kwako. kuwa tu casual but dont let her in
Mkuu,kweli hili nimeliona ingawa analazimisha tuweze kuonana; kinachonisaidia kwa sasa tupo mikoa tofauti
 
Mkuu unataka ushauri gani hapa?
 
Ukifanikiwa kuonana nae hakikisha una kilainishi mkuu itakusaidia
 
Haya mambo mengine madogo madogo ni ya kumalizana wenyewe tu huko huko kimya kimya! Mpaka uje uombe ushauri humu jukwaani kweli!!

Unadhani hata sisi wanaume wenzako hatukutani nayo? Tunakutana nayo sana tu! Ila huwa tunayamaliza kiutu uzima.
 
Linda ndoa yako. Inaonekana na wewe unapenda huo ukaribu. Show her (kwa vitendo) kuwa wewe siyo muhuni. La sivyo you will obviously sleep with her and ultimately destroy the two marriages, very very soon. Utakufa.
 
Usisahau kuleta mrejesho kwenye ule uzi wa kula tunda kimasiara.
 
Mkuu tunakusubiri kwenye uzi wa kula tunda masihara
 
Sasa hivi kuna wimbi kubwa sana la wanandoa kulipizana visasi,tena kwa kuchepuka. Ushauri wangu kwa mleta mada msisitize huyo dada atafute msaada wa kiroho kuhusu ndoa yake,na Mungu atakurudishia fadhila wewe na familia yako. Mkuu usimkwepe pengine wewe ndiyo umeandaliwa kusaidia hiyo ndoa,do your best and God will do the rest. Kila la Kheri
 
Back
Top Bottom