Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,786
Nchi nzima kuna Timu mbili tu Yanga na Simba, hata kama Yanga/ Simba wakienda kucheza Mkoani tuseme labda Mbeya dhidi ya Timu ya Mbeya Uwanja utajaa wapenzi wa Yanga/Simba badala ya timu ya Mkoa wa Mbeya hii ni ajabu sana haitokei sehemu nyingine yoyote ile Dunia hii na inaonyesha jinsi tusivyoelewa kuhusu hii Dunia kwamba tupo tupo tu!
Dunia nzima ukisikia Klabu ya Mpira maana yake ni kwamba Washabiki wa Timu hiyo ni wenyeji wa hilo eneo, lkn haiwezekani mtu amezaliwa na kukulia Tunduru, Kigoma au sijui Muheza lkn yeye ni shabiki wa kufa wa Simba/Yanga za Dar huu ni ujuha!
Sasa cha kustaajabisha zaidi Wabunge wetu wakiongozwa na Zito Kabwe &Co. ambao ndiyo wanaopaswa kuwa mfano wa kuigwa nao pia ni mashabiki na Wanachama wa Timu za Yanga na Simba, kwani Zito Kigoma hakuna football Club? Ni kwa nini wewe na wenzako ni mashabiki wa Yanga/Simba? Kwani ninyi hapa Dar ni kwenu?
Sasa naelewa kwanini Brazili walivyokuja kucheza dhidi ya Timu yetu ya Taifa Watanzania walikuwa wanaishangilia Brazili badala ya Timu yetu ya Taifa, huu ni zaidi ya ujuha, na inaonyesha jinsi gani tusivyo hata elewa kama tunafahamu tunapokwenda, tunawezaje kujenga Nchi na kuendelea kwa kushindana na Mataifa mengine kwa tabia kama hii?
Simba!
Yanga!