Upungufu wa noti za mia tano

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,973
27,205
Wakuu poleni na harakati za kutafuta rizki!!huku kitaani sijui niseme ni ukosefu au ni mzunguko wa hizi noti yaani sa hivi hizi noti za sh.500 zimekuwa adimu sana kiasi kwamba ukinunua kitu cha mia tano ukatoa elfu ankuuliza kaka/dad huna mia tano!!!kama huna anakuamvia basi chenji ya mia tano sina..zinasumbua sana tafuta kwanza chenji!!!!
 
Noti za miatano hazitengenezwi tena, sasa hivi kuna sarafu za mia tano.
Hizi sarafu za 500 watu hawataki kuzichuchua toka benki.
Mkuu huu utafiti umeufanya lini na kwa benki ipi? Kwa nini watu hawataki kuchukua hizi sarafu?
 
Mkuu huu utafiti umeufanya lini na kwa benki ipi? Kwa nini watu hawataki kuchukua hizi sarafu?

We upo nchi gani kwani,bank mbona walishatangaza hayo ya wenye mabenki kutokuchukua sarafu za Mia tano wanapoenda benk kuu,na yakwamba noti za jero hazitotolewa tena,zitatumika za coin
 
Nahusika, jamaa mmoja ameleta benki sarafu za miatano, jumla yake 1000,000/= akitaka chenji. Alikataliwa kwa kuambiwa ndani zipo milioni nane wameambiwa wazisambaze na BOT ila wateja hawazitaki.

Kama una shida na sarafu za mia tano nenda benki yoyote na kiasi ulichonacho cha kubadilishiwa, utapewa.
 
Ngoja niende maana mtaani chenji za jero ni adimu sana!!
 
Back
Top Bottom