Upumbavu wetu uko dhahiri machoni kwetu

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Leo ningependa tujadili kitu kimoja ambacho nimekipata kwa jitihada kubwa, katika kutafakari na kusoma, katika kufanya jitihada kujua mambo na katika kufungua milango ya ufahamu wa ubongo wangu, nikaona ni bora na kitu chenye thamani, kuwashirikisha. Ili kile kitu ambacho nakifahamu mpate kukifahamu na nyie pia na kipate kuwaongoza katika maisha ya yenu ya kila siku katika kipindi hiki kifupi cha uwepo wetu duniani.

Na ufahamu huu usibaki katika kizazi hiki tu bali pia upate kuwaongoza wengine watakaokuja katika vizazi vingine. Na ndio maana mimi imekuwa jukumu langu la kila siku kutafuta maarifa kadiri ya uwezo wangu kwa kutafakari na kusoma na kutoa maarifa hayo kwa watu wengine bure kabisa ili maarifa haya yapate kuwasaidia wengi zaidi kuongoza maisha yao.

Leo ningependa kuzungumzia kitu kimoja ambacho ni cha muhimu sana na ndio msingi wa maisha yetu hapa duniani na maisha yetu yanategemea sana hiko. Kufanikiwa kwetu au kutokufanikiwa kwetu kunategemea sana mambo haya ya kimsingi lakini pia amani yetu na furaha yetu.

Binadamu tunayemwona ana mwili, ambao unamtambulisha kama binadamu, na kumtofautisha mtu mmoja na mwingine. Na kumtofautisha pia yeye na wanyama na hata ndege. Maisha yake yote huyu binadamu anayaendesha kupitia mwili. Kupitia mwili wake ndio anajenga dunia tuliyonayo juu ya ardhi hii ambayo inampatia mahitaji yake ya kila siku kama mbuzi. Tofauti tu sisi tuna akili ya kupanda na kulima wao wanapata majani bila kuhangaika.

Mwili ni nyenzo inayotumiwa na binadamu kufanikisha malengo ya nguvu isiyoonekana iwe nguvu hiyo watu huitumia kwa kuijua au kwa kutoijua, lakini nguvu hiyo ipo ndani ya binadamu.

Nguvu hii ndio iliyounda dunia na kuongoza matukio yote yanayotokea duniani bila nguvu hii binadamu hawezi kuendelea. Mwili ni nyenzo tu ambayo hutumika kufanikisha malengo ya binadamu, lakini ndani yake kuna kitu kikubwa zaidi. Nguvu hii ambayo iko ndani ya binadamu hufanya kazi katika pande mbili inaweza kumsaidia binadamu akaishi maisha mazuri yenye maendeleo na furaha au kumharibu maisha yake inategemea sana ni jinsi gani ataitumia. Binadamu ana nguvu kubwa sana iko ndani yake na maendeleo yake na amani yake inategemea sana anaitumiaje.

Binadamu hawaifahamu nguvu hii lakini wanayo na wanaishi nayo na ndio inayowafanya watembee na waishi. Kwa watu walio wengi nguvu hii imedorora ndani yao. Pengine hawajajisumbua kutafuta nguvu hii. Binadamu ni zaidi ya mwili ni mkuu kuliko mwili wake mwenyewe, kwasababu kuna aliye mkuu ndani yake.

Kwasababu kuna Mungu ndani yake anayeadhibu na kutukuza. Hamjui kwamba nyinyi ni watoto wa Mungu na roho ya Mungu iko ndani yenu? Hamjui kwamba mkimfanya uovu mnamsononesha aliye ndani yenu? Ni nani ana uwezo wa kupona akilaaniwa na Mungu pasipo Mungu mwenyewe kumponya?

Mwisho wa siku kwa kumpinga Mungu tunaonekana wapuuzi, upumbavu wetu uko dhahiri machoni kwetu. Kwa kufuata vitu visivyo na faida kwetu vyenye kutuangamiza.

Baadae ya binadamu inategemea sana mawazo yake na matendo yake. Kwasababu nguvu ambayo iko ndani yake inategemea sana jinsi gani anatenda na kuwaza, na inaunda kutokana na mawazo na matendo ya binadamu. Inaunda kutokana na mbegu iliyopandwa. Ni muhimu tukajua binadamu atavuna alichopanda. Binadamu ni zao la matendo yake mwenyewe. Mungu hakuumba dunia nzuri tumeiharibu wenyewe na kuirarua ?

Je binadamu anaweza kuwa mwenye akili kuliko muumba wake? Unaweza kumdanganya Mungu? Au unajidanganya mwenyewe? Na mwisho wa siku unakuwa mpumbavu. Nadhani ni busara kumtii mwenye mamlaka.
 
Back
Top Bottom