Upotoshwaji juu ya mama wa kambo

Upotoshwaji juu ya mama wa kambo

Hawa mama wa Kambo wa sasa kidogo wameelimika! Wewe tuulize sisi tuliolelewa na mama wa kambo Malimbukeni....miaka ya 90,kurudi nyuma huko...
Nakubali kwa sasa haki za watoto na ustawi wa jamii vimepunguza ukatili kwa watoto ila miaka ya nyuma hali ilikuwa mbaya zaidi.
 
Wakuu mimi ni miongoni mwa binadamu nilielelewa kwenye mikono ya MAMA wa kambo. MAMA yangu yule nathubutu kusema alikuwa zaidi ya MAMA wakunizaa, ni MAMA alienipigania na kunilea katika misingi na malezi imara na bora na kujikuta nasahau uwepo wa MAMA mzazi.

Nilihisi labda baba ndio wakufkia na mama yule ndio mzazi mana MAMA wakambo yule alipitia misukosuko mingi toka kwa mzee kwa kuwa upande wangu. Nakumbauka niliwahi kukosea (nilichelewa kurudi nyumbani) mzee pamoja na kunipiga saana alinifunga chini ya nguzo ya kitanda alicho kilalia, MAMA yule (Mungu amlipe kila la kheri ) alivizia mzee kalala akanifungua akanionesha alipoficha chakula kisha akaingia uvunguni akawa ana furukuta ili mzee akiamka ajue me ndo npo uvunguni na MAMA yupo uwani labda.

Na kipindi nipo bwenini (5&6) nilikuwa nikirudi nyumbani likizo mzee ananipokea vyema ila soon karibuni na kurudi shuleni mzee anakuwa mkali ko hata siku yakurudi shule tofauti na Ada hapakuwa na chochote nachopata toka kwa mzee lakini MAMA yule alijitahidi kukimbia huku na kule nakutafta chochote chakunipa niende nacho na wakati mwingine alifanya kwa kujificha mzee asijue (atanikangia kuku, samaki, nakunipa vijisenti) Pia nilipokuwa kinda kuna huduma zingine kama kuniinika (wazazi tu ndo mnaelewa nikisema kumuinika mtoto) kunitoa funza na kuwa na Mimi kila wakati.

Lengo la kukumbuka malezi haya nikutaka kupinga dhana iliyowekwa kwenye jamii kuwa MAMA wakambo ni special kwa mateso, manyanyaso ,uchoyo, gubu na uchonganishi Kati ya baba na mwanae, hali ambayo imepelekea watoto wanaolelewa na mama wakambo kuwa viburi, majeuri, wavivu na watovu wa nidhamu kwa sababu MAMA zao wa kambo wanawaogopa hata kuwakalipia wanapokosea mana wakifanya hivyo huonekana labda kwa kuwa sio wanao wa kuzaa eti hawawajulii uchungu na jamii kuwaona tofauti. Ivi mtoto hata kama unamjulia uchungu ndo humpigi wala humsemi?

Natambua uwepo wa MAMA wa kambo wachache wakorofi na pia natambua uwepo wa MAMA na Baba wazazi ambao ni wakatili, kwahiyo sio kila baya wabebeshe wazazi wa kambo.

Kama nawewe umepitia malezi kama yangu, tupe stori yako tubadlishe dhana iliyowekwa kwenye jamii juu ya mama wa kambo.

@MAMAwakambonimama

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeolewa? Kama bado njooo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimelelewa na mama wa kambo 3 ..nimeanza kuishi na mama wa kambo nikiwa na miaka 7.. Miaka 3 baadae baba aliacha akaoa mwingine,,yule wa kwanza hakuwa mbaya ,,,labda alikuwa kipindi nipo mdogo sana,,,alizaa nae watoto 2 , ,,waliachana na baba ,,baadae aliondoka na mtoto mmoja,,mwingine alimwacha pale kwa baba,, mama wa pili alikaa na baba kwa miaka 2 naye alipata mtoto mmoja ,,, baadae baba akawa Mara harudi Mara week hatumuoni,,pale NYUMBANI nilibaki Mimi,,na ndugu yangu mtoto wa mama yangu yule wa kwnza,,,,huyu mama wa pili nae hakuwa mbaya, alikuwa akitupenda tu..sana hakuwa na shida... Siku moja baba alirudi akatuchukuwa mimi na mdogo wangu ,,,akatupeleka mahali Fulani,,si mbali sana na NYUMBANI,, kufika tukapokelewa vizuri sana,,akatwambiya kuanzia Leo mtaishi hapa,,,na hyu ndy mama YENU mpya,,,kipindi hicho nipo darasa la 5 .. HAPO NDY MAISHA HALISI YA MAMA WA KAMBO NIKAYAPATA...pale NYUMBANI Tulikuta yule mama ana watoto wake 2 WASICHANA wakubwa tu zaidi yetu..na tayari walikuwa wameshazalishwa,,,baada ya miezi Kama 2 yule mama yangu wa kambo wa pili nae akaja kumleta MWANAE pale kwa baba ,,,akamtelekeza pale,, yule mama hajarudi kutafuta MWANAE hadi Leo...hyo ILIKUWA mwaka 1988....mdogo wangu alikuwa na mwaka mmoja tu...BASI maisha yalikuwa ya taabu sana pale,,,nyumbani, Kwanza KUTUMWA BILA KIPIMO...Kanunuwe mkaa,,dk kumi unarudishwa tena GENGENI kanunuwe mafuta , hujakaa sawa tena nenda kanunuwe chumvi,,,na ukisema utoke ukacheze ukirudi hakuna chakula,,,MTEMBEZI HULA MIGUU YAKE...HUYU MAMA NI HATARI SANA,,,,kulikuwa na house girl lakini nikiwepo Mimi yeye hatumwi...sometimes NARUDI nataka niende tuition naambiwa NIENDE MASHINE,, KUKOBOA MAHINDI..nikifika nakuta foleni kubwa sana,,kuna mashine ILIKUWA pale TRAVETINE MAGOMENI..basi nikishakoboa NARUDI HOME wanapeta mahindi NARUDI KUSAGA TENA. ,..mimi natoka MBALI KUFATA MASHINE...ilikuwa ni UMBALI MREFU SANA,,,,kwa kifupi ILIKUWA ni kama kunifanya nisiende tuition...mdogo wangu akijisaidia basi haoshwi hadi nirudi mimi SHULE,, baba yangu hakuwahi kunipiga hata Kofi,,lakini kwa mama huyu ilikuwa ni makofi kila siku,,maana kila siku kesi za kusingiziwa,,,CHOO CHENYEWE MLANGO WA GUNIA,,,MTU ANAOGA ukipita anasema mwanao ananichungulia CHOONI,,CHAKULA kwenye kisahani cha chai,,kwa kweli huyu mama alikuwa MIYAYUSHO SANA,,,nikipofika STD 7 ..MUNGU ALIJAALIA NILICHAGULIWA KUJIUNGA NA AZANIA SEC SCHOOL...aisee,,yule mama ilimuuma sana,,na pale ilikuwa tunaishi kwenye nyumba ya yule mama,,lilikuwa banda Fulani bovu,,baba aliitengeneza ikawa inatizamika,,,sijuwi alipatwa na NINI MZEE wangu,, yule mama akamwambiya baba yangu hataki Mimi niishi pale tena ,,aondoke yeye ,au niondoke Mimi,, basi baba akaniondoa kwa shingo upande,, akanipeleka kwa mjomba wake niishi....kwakweli story ni ndefu sana...naomba niishie hapa MKUU... nitaleta tena maisha ya kwa mjomba wa baba SIKU ingine..LAKINI kwa kifupi mama wa kambo kumpata aliyekuwa BORA NI BAHATI SANA,,WENGI wao wana pretend.... KUTENGENEZA MAPENZI BAINA YAKE NA MUME,, ,mwisho wa siku mama anatia sumu kwa baba ili awachukie watoto wake... Nakusihi kama una UWEZO Lea wanao PEKE YAKO NA HOUSE GIRL,, ukipata MWANAMKE malizana nae HUKO HUKO NJE..au mpangie sehem ingine,,nakuhakikishia UTAKUWA LULU KWA WATOTO WAKO....kukaribisha mama wa kambo ni KUTOA SADAKA MAPENZI YAKO NA WATOTO WAKO..na hata JITAHIDI KUISHI NA MKEO VYEMA ili mlee watoto wenu pamoja....hata huko kwa mjomba wa baba pia nilipatwa na VISANGA VINGI SANA , LAKINI VILINIFANYA NIWE STRONG BOY...na KUINGIA kwenye maisha ya UBAHARIA HADI SASA.... hii ni TRUE STORY OF MY LIFE....

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana , na mara nyingi watoto wao huwa mbulula tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wala simlaumu MZEE,,, ni kulewa na MAPENZI , au PENGINE alifanyiwa mambo ya kiswahili... ,,miaka miwili baadae wakaachana na yule mama,,,MZEE AKAWA ANAISHI KIVYAKE....na hakutoka na kitu kwa yule mama,,..NOW NAAMINI PENGINE ALIMFANYIA NGUVU ZA GIZA...baada ya kutoka pale NYUMBANI nilikuwa na MAHUSIANO mazuri sana na baba yngu...alikufa mwaka 2003 mikononi mwangu...hospital

Sent using Jamii Forums mobile app
Daa pole sana, bora alimalizia maisha yake mkiwa vizuri,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo watu wanapenda sana kujumuisha mambo (generalization). Kwasababu labda aliteswa na mama wa kambo basi atasema wamama wa kambo wote wabaya.

Tabia ya mtu mmoja sio jumuishi. Watu wako tofauti. Kuna mama wazazi wengine ni aheri hata mama wa kambo.
Kuna wakati mwingine mama anakuwa mzuri ila watoto mwenyewe sasa na akijua huyu si mama yake daa kiburi dharau, kuna wengine hufundishwa na mama yake kabisa uwe unamjibu vibaya, kuna mmoja baada ya kuachana na mmewe naye kuoa mke mwingine akawa anapita pale eti wewe house girl wa watoto wangu vipi. sasa hapo unategemea nini watoto wako watapokea nini hapo!

Na ndicho kinachochafua taswira ya mama wakambo .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo lipo kwenye Jamii imeshazoeleka ivyo kuwa mama wa kambo ni mtu mmbaya lakini Kuna mama wa kambo wenye mioyo yenye huruma Kama mama wa mleta mada.

Mama angu mdogo aliolewa kwenye familia ambayo tayari alikuta watoto Tena Ni wadogo mkubwa alikuwa na miaka mitano mdogo miaka mitatu..Mama yule aliwalea wale watoto Kama wake na mapenzi yote..lakini aliyoyapitia kwenye kulea wale watoto Ni mateso kutoka kwa mtoto mkubwa ambaye ni wa kike akishirikiana na mama mkubwa wa wale watoto..juzi tu hapo baada ya wale watoto kupatwa na janga yule mkubwa ndiyo kaanza elewana na kumuheshimu Mama yao wa kambo.
 
Kuna wakati mwingine mama anakuwa mzuri ila watoto mwenyewe sasa na akijua huyu si mama yake daa kiburi dharau, kuna wengine hufundishwa na mama yake kabisa uwe unamjibu vibaya, kuna mmoja baada ya kuachana na mmewe naye kuoa mke mwingine akawa anapita pale eti wewe house girl wa watoto wangu vipi. sasa hapo unategemea nini watoto wako watapokea nini hapo!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa siunaona mama mzazi hapo ndio anataka kuwa chanzo cha wanawe kuteseka kisa chokochoko tu.
 
Tatizo lipo kwenye Jamii imeshazoeleka ivyo kuwa mama wa kambo ni mtu mmbaya lakini Kuna mama wa kambo wenye mioyo yenye huruma Kama mama wa mleta mada.

Mama angu mdogo aliolewa kwenye familia ambayo tayari alikuta watoto Tena Ni wadogo mkubwa alikuwa na miaka mitano mdogo miaka mitatu..Mama yule aliwalea wale watoto Kama wake na mapenzi yote..lakini aliyoyapitia kwenye kulea wale watoto Ni mateso kutoka kwa mtoto mkubwa ambaye ni wa kike akishirikiana na mama mkubwa wa wale watoto..juzi tu hapo baada ya wale watoto kupatwa na janga yule mkubwa ndiyo kaanza elewana na kumuheshimu Mama yao wa kambo.
Na ndio lengo la Uzi huu. Niltaka jamii itambue mchango wa MAMA wa kambo katika malezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu mimi ni miongoni mwa binadamu nilielelewa kwenye mikono ya MAMA wa kambo. MAMA yangu yule nathubutu kusema alikuwa zaidi ya MAMA wakunizaa, ni MAMA alienipigania na kunilea katika misingi na malezi imara na bora na kujikuta nasahau uwepo wa MAMA mzazi.

Nilihisi labda baba ndio wakufkia na mama yule ndio mzazi mana MAMA wakambo yule alipitia misukosuko mingi toka kwa mzee kwa kuwa upande wangu. Nakumbauka niliwahi kukosea (nilichelewa kurudi nyumbani) mzee pamoja na kunipiga saana alinifunga chini ya nguzo ya kitanda alicho kilalia, MAMA yule (Mungu amlipe kila la kheri ) alivizia mzee kalala akanifungua akanionesha alipoficha chakula kisha akaingia uvunguni akawa ana furukuta ili mzee akiamka ajue me ndo npo uvunguni na MAMA yupo uwani labda.

Na kipindi nipo bwenini (5&6) nilikuwa nikirudi nyumbani likizo mzee ananipokea vyema ila soon karibuni na kurudi shuleni mzee anakuwa mkali ko hata siku yakurudi shule tofauti na Ada hapakuwa na chochote nachopata toka kwa mzee lakini MAMA yule alijitahidi kukimbia huku na kule nakutafta chochote chakunipa niende nacho na wakati mwingine alifanya kwa kujificha mzee asijue (atanikangia kuku, samaki, nakunipa vijisenti) Pia nilipokuwa kinda kuna huduma zingine kama kuniinika (wazazi tu ndo mnaelewa nikisema kumuinika mtoto) kunitoa funza na kuwa na Mimi kila wakati.

Lengo la kukumbuka malezi haya nikutaka kupinga dhana iliyowekwa kwenye jamii kuwa MAMA wakambo ni special kwa mateso, manyanyaso ,uchoyo, gubu na uchonganishi Kati ya baba na mwanae, hali ambayo imepelekea watoto wanaolelewa na mama wakambo kuwa viburi, majeuri, wavivu na watovu wa nidhamu kwa sababu MAMA zao wa kambo wanawaogopa hata kuwakalipia wanapokosea mana wakifanya hivyo huonekana labda kwa kuwa sio wanao wa kuzaa eti hawawajulii uchungu na jamii kuwaona tofauti. Ivi mtoto hata kama unamjulia uchungu ndo humpigi wala humsemi?

Natambua uwepo wa MAMA wa kambo wachache wakorofi na pia natambua uwepo wa MAMA na Baba wazazi ambao ni wakatili, kwahiyo sio kila baya wabebeshe wazazi wa kambo.

Kama nawewe umepitia malezi kama yangu, tupe stori yako tubadlishe dhana iliyowekwa kwenye jamii juu ya mama wa kambo.

@MAMAwakambonimama

Sent using Jamii Forums mobile app
mwaka 84 dingi alikua anaoa mke mwingine,wakati huo mlezi wangu ni bibi mkewe babu.kisha tukaanza maisha ya kifamilia mimi dingi na mkewe mpya,na muda si mrefu na sis akazaliwa.kipindi hiki ubaya na wema havikupishana sana ktk mizani sababu ya utoto.miaka kadhaa tukiwa sumbawanga mji wenye baridi njombe imesingiziwa,ndio mizani ikakaa sawa.na nikajua huyu ni mtu mwema,nakumbuka sauti yake akitufukuza tusimfate anapowasindikiza wageni lkn hatusikii.kisha wakati anarudi tunaungana nae huku akitupigia stori.nakumbuka baba akiwa hayupo alivyohangaika na mguu uliovimba kwa kuchomwa na msumari,nakumbuka ktkt kotaz za pale jangwani zilizo karibu na msitu wa wilayani huku mvua kubwa kabisa ikinyesha nimejificha bustanini namuona akiwa ameroa anapita vibaraza vya nyumba nyingine,huku akiniita,nakumbuka barazani kwetu kulikua na meza.mbovu.hilo lilikua chimbo lake la kunifichia chakula.kisha nakumbuka wakati anafariki agakhan anamwachia maagizo dada yake ,akimwambia dada wanangu.kuna mwaka nilikwenda arusha likizo nikakaa na mama mzazi mwezi tu.akilini ikaingia hisia nikiambiwa nichague namchagua wa kambo.alikua mtu mwema hata baba alipotangulia mapenzi hayakupungua.kama alikua na makosa meeeeeeengi kwa mungu,basi malezi aliyonilea yanatosha kumpa msamaha huko aliko.aliitwa mama mimi,sio mama mwanae wa kumzaa.eeh mola mlezi.mmiliki wa viumbe.muhurumie yule mama,alinihurumia sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hyo inategemea roho ya mtu, ni kweli wamama wa kambo wengine wamejaliwa roho nzuri had unaweza usijue kama sio mama mzazi.

Kuna mama aliolewa akakuta watoto wa huyo baba wakubwa kiasi, aliwalea kama watoto wake kwa kuwapa upendo wa mama hadi watoto wakawa watu wazima wanajitegemea. Bahati mbaya yule mama hakufanikiwa kupata mtoto kwa mda wote alioolewa hapo.
Last yr mwishoni yule baba alifariki, ndugu wakaanza vimbwanga na kutaka yule mama aondoke kwenye nyumba ya ndugu yao kwa kisingizo kua hawezi kurithi mali hana mtoto (yule mzee alikua tajiri so aliacha mali nyingi tu) wale watoto ndio walikua watetezi wake, walikua tayari kugombana na ndugu zao kwa ajili ya yule mama hadi mwisho wa siku ndugu ikabd wawe wapole wakamuachia yule mama kila kitu.

Nikakumbuka ule msemo wa "Wema Hauozi"
 
Mimi nimelelewa na mama wa kambo 3 ..nimeanza kuishi na mama wa kambo nikiwa na miaka 7.. Miaka 3 baadae baba aliacha akaoa mwingine,,yule wa kwanza hakuwa mbaya ,,,labda alikuwa kipindi nipo mdogo sana,,,alizaa nae watoto 2 , ,,waliachana na baba ,,baadae aliondoka na mtoto mmoja,,mwingine alimwacha pale kwa baba,, mama wa pili alikaa na baba kwa miaka 2 naye alipata mtoto mmoja ,,, baadae baba akawa Mara harudi Mara week hatumuoni,,pale NYUMBANI nilibaki Mimi,,na ndugu yangu mtoto wa mama yangu yule wa kwnza,,,,huyu mama wa pili nae hakuwa mbaya, alikuwa akitupenda tu..sana hakuwa na shida... Siku moja baba alirudi akatuchukuwa mimi na mdogo wangu ,,,akatupeleka mahali Fulani,,si mbali sana na NYUMBANI,, kufika tukapokelewa vizuri sana,,akatwambiya kuanzia Leo mtaishi hapa,,,na hyu ndy mama YENU mpya,,,kipindi hicho nipo darasa la 5 .. HAPO NDY MAISHA HALISI YA MAMA WA KAMBO NIKAYAPATA...pale NYUMBANI Tulikuta yule mama ana watoto wake 2 WASICHANA wakubwa tu zaidi yetu..na tayari walikuwa wameshazalishwa,,,baada ya miezi Kama 2 yule mama yangu wa kambo wa pili nae akaja kumleta MWANAE pale kwa baba ,,,akamtelekeza pale,, yule mama hajarudi kutafuta MWANAE hadi Leo...hyo ILIKUWA mwaka 1988....mdogo wangu alikuwa na mwaka mmoja tu...BASI maisha yalikuwa ya taabu sana pale,,,nyumbani, Kwanza KUTUMWA BILA KIPIMO...Kanunuwe mkaa,,dk kumi unarudishwa tena GENGENI kanunuwe mafuta , hujakaa sawa tena nenda kanunuwe chumvi,,,na ukisema utoke ukacheze ukirudi hakuna chakula,,,MTEMBEZI HULA MIGUU YAKE...HUYU MAMA NI HATARI SANA,,,,kulikuwa na house girl lakini nikiwepo Mimi yeye hatumwi...sometimes NARUDI nataka niende tuition naambiwa NIENDE MASHINE,, KUKOBOA MAHINDI..nikifika nakuta foleni kubwa sana,,kuna mashine ILIKUWA pale TRAVETINE MAGOMENI..basi nikishakoboa NARUDI HOME wanapeta mahindi NARUDI KUSAGA TENA. ,..mimi natoka MBALI KUFATA MASHINE...ilikuwa ni UMBALI MREFU SANA,,,,kwa kifupi ILIKUWA ni kama kunifanya nisiende tuition...mdogo wangu akijisaidia basi haoshwi hadi nirudi mimi SHULE,, baba yangu hakuwahi kunipiga hata Kofi,,lakini kwa mama huyu ilikuwa ni makofi kila siku,,maana kila siku kesi za kusingiziwa,,,CHOO CHENYEWE MLANGO WA GUNIA,,,MTU ANAOGA ukipita anasema mwanao ananichungulia CHOONI,,CHAKULA kwenye kisahani cha chai,,kwa kweli huyu mama alikuwa MIYAYUSHO SANA,,,nikipofika STD 7 ..MUNGU ALIJAALIA NILICHAGULIWA KUJIUNGA NA AZANIA SEC SCHOOL...aisee,,yule mama ilimuuma sana,,na pale ilikuwa tunaishi kwenye nyumba ya yule mama,,lilikuwa banda Fulani bovu,,baba aliitengeneza ikawa inatizamika,,,sijuwi alipatwa na NINI MZEE wangu,, yule mama akamwambiya baba yangu hataki Mimi niishi pale tena ,,aondoke yeye ,au niondoke Mimi,, basi baba akaniondoa kwa shingo upande,, akanipeleka kwa mjomba wake niishi....kwakweli story ni ndefu sana...naomba niishie hapa MKUU... nitaleta tena maisha ya kwa mjomba wa baba SIKU ingine..LAKINI kwa kifupi mama wa kambo kumpata aliyekuwa BORA NI BAHATI SANA,,WENGI wao wana pretend.... KUTENGENEZA MAPENZI BAINA YAKE NA MUME,, ,mwisho wa siku mama anatia sumu kwa baba ili awachukie watoto wake... Nakusihi kama una UWEZO Lea wanao PEKE YAKO NA HOUSE GIRL,, ukipata MWANAMKE malizana nae HUKO HUKO NJE..au mpangie sehem ingine,,nakuhakikishia UTAKUWA LULU KWA WATOTO WAKO....kukaribisha mama wa kambo ni KUTOA SADAKA MAPENZI YAKO NA WATOTO WAKO..na hata JITAHIDI KUISHI NA MKEO VYEMA ili mlee watoto wenu pamoja....hata huko kwa mjomba wa baba pia nilipatwa na VISANGA VINGI SANA , LAKINI VILINIFANYA NIWE STRONG BOY...na KUINGIA kwenye maisha ya UBAHARIA HADI SASA.... hii ni TRUE STORY OF MY LIFE....

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh! Story yako ipo serious kidogo ila kuna kitu chakujifunza na kikubwa ni kwamba Baba ndio chanzo cha mateso ya mama wa kambo kwa watoto. Mana kama baba kaolewa na kabeba na wanae kapeleka unahisi atakuwa na sauti apo.? Lakini pia hata mzee hakuwa fair mana kashindana na wanawake wawili ( japo mama yako hujamzungumzia huenda na yy walishindana) ko mpaka hapo mzee ndo chanzo cha yote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom