Cheef Baroka
JF-Expert Member
- Apr 28, 2019
- 490
- 1,019
Wakuu mimi ni miongoni mwa binadamu nilielelewa kwenye mikono ya MAMA wa kambo. MAMA yangu yule nathubutu kusema alikuwa zaidi ya MAMA wakunizaa, ni MAMA alienipigania na kunilea katika misingi na malezi imara na bora na kujikuta nasahau uwepo wa MAMA mzazi.
Nilihisi labda baba ndio wakufkia na mama yule ndio mzazi mana MAMA wakambo yule alipitia misukosuko mingi toka kwa mzee kwa kuwa upande wangu. Nakumbauka niliwahi kukosea (nilichelewa kurudi nyumbani) mzee pamoja na kunipiga saana alinifunga chini ya nguzo ya kitanda alicho kilalia, MAMA yule (Mungu amlipe kila la kheri ) alivizia mzee kalala akanifungua akanionesha alipoficha chakula kisha akaingia uvunguni akawa ana furukuta ili mzee akiamka ajue me ndo npo uvunguni na MAMA yupo uwani labda.
Na kipindi nipo bwenini (5&6) nilikuwa nikirudi nyumbani likizo mzee ananipokea vyema ila soon karibuni na kurudi shuleni mzee anakuwa mkali ko hata siku yakurudi shule tofauti na Ada hapakuwa na chochote nachopata toka kwa mzee lakini MAMA yule alijitahidi kukimbia huku na kule nakutafta chochote chakunipa niende nacho na wakati mwingine alifanya kwa kujificha mzee asijue (atanikangia kuku, samaki, nakunipa vijisenti) Pia nilipokuwa kinda kuna huduma zingine kama kuniinika (wazazi tu ndo mnaelewa nikisema kumuinika mtoto) kunitoa funza na kuwa na Mimi kila wakati.
Lengo la kukumbuka malezi haya nikutaka kupinga dhana iliyowekwa kwenye jamii kuwa MAMA wakambo ni special kwa mateso, manyanyaso ,uchoyo, gubu na uchonganishi Kati ya baba na mwanae, hali ambayo imepelekea watoto wanaolelewa na mama wakambo kuwa viburi, majeuri, wavivu na watovu wa nidhamu kwa sababu MAMA zao wa kambo wanawaogopa hata kuwakalipia wanapokosea mana wakifanya hivyo huonekana labda kwa kuwa sio wanao wa kuzaa eti hawawajulii uchungu na jamii kuwaona tofauti. Ivi mtoto hata kama unamjulia uchungu ndo humpigi wala humsemi?
Natambua uwepo wa MAMA wa kambo wachache wakorofi na pia natambua uwepo wa MAMA na Baba wazazi ambao ni wakatili, kwahiyo sio kila baya wabebeshe wazazi wa kambo.
Kama nawewe umepitia malezi kama yangu, tupe stori yako tubadlishe dhana iliyowekwa kwenye jamii juu ya mama wa kambo.
@MAMAwakambonimama
Sent using Jamii Forums mobile app