Upotoshaji wa Habari! Nani alaumiwe?

Mkuu, wa kulaumiwa hapa ni Mengi au Mhariri wa Gazeti ambaye amesomea uandishi na akawa kinara wa upuuzi? Same things are happening kwenye gazeti la Majira, labda mkuu hujasoma vema wanavyojichanganya Majira. Habari moja inarudiwarudiwa mara kadhaa huku ikionesha wazi kuna target binafsi aidha za kuchafuana ama kujipendekeza kwa watu flani. Mhariri wa Majira na wa Alasiri wanatakiwa kujua kuwa kadiri wanavyoruhusu upuuzi wa namna hii ndivyo wanavyopelekea watanzania kuona kuwa magazeti haya ni ya kizushi

Yapo mengi haya magazeti. Lakini mbona unalisahau na TANZANIA DAIMA.
 
Wait a minute, hivi Mengi ndo mhariri wa gazeti hilo? Sikujua mkuu.

On the other hand, kukiwa na habari ambayo inaenda kombo katika RAI, Mtanzania, Dimba, Taifa, Dimba n.k tumlaumu Rostam?

Watu twende mbali zaidi, tuwabana wahariri wanaoweza kununulika kwa maneno ama vijisenti kadhaa waache kuwa chanzo cha uzushi katika sekta ya habari kwani ni wizi wa wazi wa fedha za wananchi wanaonunua magazeti yao na ni uchochezi wa kutafuta heading ya kuuza gazeti ilhali content iliyo ndani yake siyo!

In this case... naanzisha Thread, special.
 
Mkuu wangu Heshima mbele,

Upotosahji wa habari Tanzania ulianza mwishoni mwa mwaka 2004, na ulianzishwa rasmi na kundi la kisiasa la Mtandao kwa kuanza kuwanunua waandishi na magazeti yetu, since then hatujawahi ku-recover as a nation,

Wananchi huiga tabia za viongozi wao, na walionunua habari, yaani Mtandao sasa wako kwenye power, eti wakulaumiwa hapa ni nani kama hoja yako ni kweli, maana hata hoja yako bado ni debatable kama ina ukweli!
 
Ukweli ni kwamba magazeti mengi tu ya bongo yana mapungufu ya kutoa habari zilizofanyiwa utafiti na uchambuzi wa kina. Mengi yana mtazamo wa kuwa wa kuongeza mapato (turnover ya magazeti) kwa kuweka vichwa vya habari vyenye mvuto na vyenye kumwacha mnunuzi mtarajiwa njia panda kama siyo kupandwa na hasira mara tu anapotoa Shs 400 au 500 kununua gazeti husika. Hili ni tatizo mojawapo ambalo wahariri wa habari na wamiliki wake kutupa kando usanifu na kuzingatia kujenga himaya kupitia 'turnover' ya siku ya gazeti. Nafikiri hii fani imekosa watu waliobobea ambao wanashughulikia 'quality assurance'.
 
Kwa wale mnaotaka kumtetea Mkapa kwa nguvu zote, muwe mnatafuta hoja znito basi maana hizi zingine mnajishusha hadhi na yeye pia!
 
Mkuu,

Taifa lilianza kupoteza waandishi makini baada ya waandishi kutaka kutukuzwa na kupenda masiha ya juu kuliko kile wanchokipata.Waligundua kwamba wanaweza kuwa matajiri kwa kuwatumia wale wanowapamba kila siku na ndicho kianendelea mpaka leo.Leo sio ajabu mtu kumsifia Mbowe a Lowassa na kumponda Wangwe kwa kuwa anatofautiana na yule anayempenda.Tumeona hapa hapa JF kipindi cha kumsimamisha wangwe watu makini wanaondelea kumtukuza mtu na chama na walijitahidi sana kuspin mambo ya uongo kuhusu ndugu yaangu wa kemakorere(hili linaniuma sana)

Waandishi wamekuwa wakimsifia mtu tu kuliko kusifia yale anayoyafanya kw aumakini,Ukiangalia Gazeti moja la kila siku limekuwa likiandika Habari zinazohusu chama kimoja cha Upinzani na kuhakikisha kinampaamba mwenyekiti wake.Imesaidia kuwabomoa watu wachafu na hilo ni lengo mojawapo la uandishi.Mie sitaki kuamini kwamba hili lilianza 2004 na watu wa Mtandao bali limeanza pale tulipoacha kujali maslahi ya taifa

Hiyo imeendelee hata hapa Jamvini,kumukuwwapo watuambo wanaandika kwa sababu wanapenda flani awe hivyo alivyo na asiguswe,tumejawa na hisisa za wale walio wakubwa zetu.tumenyeyekea vyama vyetu kuliko Maslahi ya Taifa.

Mie naweza kusema upotoshaji wa habari ulianza pale tulipoanza kuwa mashabiki wa habari zisizo na msingi,tulipoaanza kuamini kwamba ukiandika jambo linalomhusu flani utaheshimika na kupata Pesa.Kuna kipindi hapa Mzee mwanakijiji aliwahi kuleta habari ya kaanzi kwamba Mhe. Ngeleja ana undugu wa kindoa na Mhe Lowassa kwa lengo ambalo sijui lilikuwa ni nini,ila tulimuelewesha kwa kumueleza ukweli.Mie nafikiri tuendele kurekebishana na kusaidiana pale tunapokosea au kukosea

Ila naamini hatujachelewa,sidhani kama kuwa Tajiri ni ufumbuzi wa kila kitu,sidhani kama kusifia chama na kumtetea mtu kwamba hakufeli shule naweza leta maana,Hata kama mtu amefukuzwa na mapanga tusimjadili na tumuache aje ajitetee Mwenyewe.Tumeacha vyama kumiliki Media na hili ndilo jambo ambalo linatupoza na kutufanya tuwe mhayawani

Tulishapotea njia muda mrefu,tumekubali kufungwa bao la kisigino,waliltumia udhaifu wetu kutumaliza,Jf sasa tupo kama hatupo na tunawategemea hao walete habari,tumeacha uchunguzi wa kina na tumeendekeza kuandamana sisi kwa sisis kwa maneno yasiyo na msingi,vita kati yetu ndiyo inachochoea haya yote ya upotoshaji wa habari
 
1. Hivi gazeti likiandika upuuzi wakulaamiwa ni mwekezaji/mmliki au mhariri/mwandishi? Mfano... mmoja wa mwekezaji/mmliki wa mwananchi ni Aghakan ambaye hata hajui gazeti linaandikwa nini yeye anachoangalia ni je bottom line kwenye mahesabu inaonyesha kiasi gani.?.. bottom line ni mstari kwenye hesabu za makampuni unaonyesha profit after tax. Mengi pia, Rostam, na Mliki wa Majira wote... siku zote waangalia zaidi huo mstari... na wakati mwingine wanachukua muda mrefu bila kusoma magazeti yao...

Mkuu, una uhakika kwamba hawa mabwana wakubwa wanaangalia faida tu kwenye magazeti yao? Jaribu kutafuta taarifa kutoka vyombo vyao utabaini kuwa, kama si wote, wengi wao wanainfluence edirtoria content.

Tukiacha hilo....
Kama ilivyoelezwa hapo juu, your comments are debetable if they are true na ni kwa sababu they are too general in a sense kwamba upotoshaji wa habari unaweza kufanyika katika level yoyote ya hizo ulizozitaja.
Wapo wamiliki ambao wanadedicate kiandikwe nini kuhusu jambo fulani. wapo wamiliki ambao wametoa policies kwa wahariri wao kwa mba linapotokea jambo linalohusu kitu fulani, mrengo wa vyombo vyake vya habari ni huu na hakuna kubadili unless umechoka kufanya kazi hapo.
Habari inaweza kupotoshwa na mwandishi au mhariri.
lakini kubwa zaidi, habari inaweza kuwa sahihi, lakini ikapotoshwa na msomaji kwa kutotaka kuamini kilichaondikwa badala yake akataka kuamini anachokiamini yeye hata kama kilichoandikwa ndio ukweli wenyewe
 
Ukweli ni kwamba magazeti mengi tu ya bongo yana mapungufu ya kutoa habari zilizofanyiwa utafiti na uchambuzi wa kina. Mengi yana mtazamo wa kuwa wa kuongeza mapato (turnover ya magazeti) kwa kuweka vichwa vya habari vyenye mvuto na vyenye kumwacha mnunuzi mtarajiwa njia panda kama siyo kupandwa na hasira mara tu anapotoa Shs 400 au 500 kununua gazeti husika. Hili ni tatizo mojawapo ambalo wahariri wa habari na wamiliki wake kutupa kando usanifu na kuzingatia kujenga himaya kupitia 'turnover' ya siku ya gazeti. Nafikiri hii fani imekosa watu waliobobea ambao wanashughulikia 'quality assurance'.

Orkesumet Nakusalimu, SUBHAI.
Naomba kukupinga kwa hilo nililowekea rangi nyekundu, kwanza tukubali kuwa habari hizo ndizo zinazouzika, habari zipo na zinafanyiwa uchunguzi vizuri ila sasa inapofika suala la marketing(kutengeza soko) ndipo tatizo linapojitokeza, ni vipi tutaliuza gazeti na hatuna ubunifu wowote wa kuliunda soko ndipo waandishi na wahariri wanapochukuwa njiamkato(shortcut) kwamba kutokana na waliowengi wa WaTanzania ni wa vipato duni maisha magumu hawamudu burudani, njia mmbadala ni burudani ya vituko kashfa vioja mapenzi ngono nk vinawekwa magazetini basi yanakimbiliwa magazeti kama njugu.
Unajua kuwa Mwanadamu anapokuwa na machungu/mazonge ya maisha halafu unampelekea habari za wengine wanaoteseka ama kuharibikiwa inakuwa ni sehemu ya tulizo ama nafuu ya kujiona kwamba hayuko pekee katika matatizo anajiliwaza, hivyo ndivyo tulivyo wengi wa waTanzania.
 
suala la mmiliki na mhariri halina tofauti na mwajiri na mwajiriwa! Tukiangalia kwenye sekta nyingine, kwa mfano mahakama, serikali ndio mwajiri wa Majaji na hata mahakimu, lakini inapofika kwenye masuala ya utendaji, tumeona Majaji wanaihukumu serikali (serikali inashindwa kesi!). Inapofikia kwenye suala la miiko ya kazi, hakuna mambo ya mwajiri na mwajiriwa!

Kwa hiyo tunaporudi kwenye sekta ya habari, mambo ni tofauti kabisa, tunaona mwajiriwa (mhariri) anamlamba miguu mwajiri (mmiliki)! Kisa, apate kuishi, ama apate maisha bora! Hii inaendekezwa na wahariri wenyewe na wala si mmiliki, tumeona wahariri wakihama chombo kimoja kwenda kingine, kwasababu ya kunyimwa uhuru wa mawazo na ki-fikra!

Mtindo wa kulamba miguu, ulemaza wahariri wetu, na hata uwezo wao wa kupembua mambo unafifia, na taaluma hii sasa inafifia!

FMES,

You are very right! Haya mambo yameanzishwa na wana-mtandao, mapema kabisa wakati wa mchakato wa chama! Sisi wasomaji wazuri, tulianza kushangaa kuliko wahariri wameanza kunukuu hata magazeti ya enzi za TANU!! Kwanini kipindi hiki ndio tunaambiwa habari za HIZBU!!! Je habari hizi zilikuwa zinahitajika kwaajili ya nini kipindi hicho?? utapata jibu, kuna mtu alikuwa anatekeleza kazi yake ya "kulamba" mguu wa mwajiri!

Na hili limeendelea mpaka sasa, ni jukumu la baraza la wahariri kukemea na kuhakikisha wanasimamia miiko yao ya kazi. Sisi kama wasomaji wametuongezea mzigo wa kusoma habari nyingi zaidi ili kugundua ukweli! Tumefika sehemu ambapo hakuna kuamini chombo kimoja cha habari, lazima upitie vyombo vinne hata visita ili kujua ukweli wa taarifa moja tu! Na hii ni mbaya kwa suala zima la ustawi wa sekta ya habari Tanzania!
 
Mkuu Field Marshall na Think Big.

Sawa walioanzisha ni wana-Mtandao.. tumejua, tusonge mbele basi, tunaomba tusahau maana wanamtandao sio wenye nchi wenyewe, nchi ni ya kwetu sote ... hatuwezi kuongelea historia forever otherwise, tutakuwa kama Zanzibar ambapo madoa tangu ya uchaguzi wa 1957 bado yanaathiriki watu ambao hata hawakuwepo wakati huo.

Tunahitaji ku-change and we need responsible journalism like yesterday.
 
Tunahitaji Mapinduzi ya Utamaduni!

a new Cultural Revolution

The good thing is WE at JAMII FORUMS we can INFLUENCE and DRIVE that critical and important change.

Let us try our level best to be part of the SOLUTION and not part of the PROBLEM.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
2. Hivi JF hapa watu wanapoweka pumba, wa kulaumia ni JF management au mwekezaji/mtoa pumba zake?

3. Hivi ni lini tutatoka kwenye kujadili watu ili tuingie kwenye kujadili hoja (issues) mifumo (systems, legal frame work), sera(policies), maendeleo (development challenges), uchumi, uwekezaji, elimu, mazingira... etc.

Chonde chonde Watanzania wenzangu tukemee uandishi usio makini maana ni Sumu kubwa sana ya maendeleo yetu kama taifa.

Mungu ibariki Tanzania
Ahsanteni kwa kunisoma.

Kasheshe,

Mbona Marshall Plan ya Mchungaji hujachangia kitu na huko hakuna kutajana majina?
 
Mkuu Invicible ni makampuni ya IPP Media yanayoongoza kuandika habari zozote zenye lengo la kumbabua BWM, ushahidi uko wazi na pia hata yale ambayo Mengi ana hisa agenda ni hiyhiyo!!! Soma This day au Kulikoni , Nenda the Guardian, Nipashe,Acha Umbea na hata ya michezo, Ni Lete Raha lililoendesha kampeni ya kupinga Uwanja mpya usiitwe kwa jina la Mkapa mpaka wakathubutu kupendekeza uitwe Jakaya M.Kikwete, tunayaangalia magazeti haya kwa macho ya fadhaa maana sasa hata Pimbi anatambua mchezo unaofanyika.

Ninakutaka ufanye uchunguzi wako, IPP Media wanavyoziripoti habari za viongozi wa Umma wa Tz inapofika Mkapa tatizo kwelikweli na ndio maana kuna siku nilihoji JF iweje hawa jamaa wa IPP Media habari iwe ni Mkapa pale inapozungumzia yale wanayoona na mabaya yake?!! Lakini inapokuja dunia na umma ku acknowledge mchango wako they don't want to be part of it?!!!! Kumbuka kilichotokea National Stadium(The New Arena) , kwa makusudi IPP walianza kampeni za kuwaonyesha viongozi wa sasa kila mara lakini wale wachina wakaamua kuiwasha ile Runinga pale ndani ikimuonyesha Ben Netanyahu Mkapa uwanja uliripuka kama kuna goli limeingia kimiani, wao hawakuonyesha hicho kitu live siku ile mpaka siku ya pili tuliposoma baadhi ya magazeti kuwa wananchi walisahau machungu ya game mara baada ya kuonyeshwa mzee Netanyahu akikagua uwanja wakati wa mapumziko.

Ninaanza kuamini kuwa ushirika wa Msuya na Mengi na harakati za kujipendekeza kwao kwa utawala mpya ni chanzo cha yote yanayompata Mkapa, hakukosea kuwa wagomvi wake ni pamoja na wale aliwanyima mamlaka zama za utawala wake.

Invicible, Mengi anao mkono juu ya haya yanayotendwa na waajiriwa wake dhidi ya Ben Netanyahu, usipoteze muda wako kumtetea huyu tajiri kwani umma unamuangalia kwa jicho la kisirani kwa mahubiri yake na matendo yake, tulisha hoji iweje huyu afananishwe na Martin Luther King Jr, tuliongea mengi humu JF.

Mzee Mramba alichosema ni sahihi kabisa na wala hakulenga kumponda mtu wala chama chake bali ni kujiuliza kama Mtz, ameongea kwa ufasaha ,kwa dhati ya moyo wake na zaidi ametoa changamoto. Muandishi anapoamua kupotosha ,Muhariri anapokubaliana na Mmiliki anapokaa kimya bila kuchukua hatua za makusudi kurejesha imani na heshima ya mali zake unataka tusimuhoji?!!!

Mkuu black and white IPP Media ni tatizo kwa maendeleo ya habari Tz, tunamlaumu sana Rostam why?? Ni pale tunapoona media zake zinapotosha umma, why not Mengi? Ni mungu huyu au?
Alichotaka ktk kipindi cha Mkapa na kukikosa sasa amekipata kwa JK, tunamuona yuko karibu naye sana ingawaje jamii haipendezwi na hali hiyo lakini maamuzi ya Rais na tunayaheshimu, mzee wake Msuya naye kasogezwa basi inatosha kwake ,ajenge nchi na siyo malumbano yaso na hoja.

Hofu yake nini kwa Mkapa ambaye sasa si Rais wa nchi au anataka nini toka kwa huyu mzee? Issue hii Mkuu invisible inawakera wananchi wengi sana na kwa dhati ninaamini inaipotosha nchi maana umma hautaki kukubaliana na huu mchezo na muda unakwenda wakati mambo ya muhimu hayazungumzwi na tunamjadili mtu tena kwa pesa za nchi yetu.

Imetosha wakuu, sasa wahariri jaribuni kuheshimu taaluma zenu na mkumbuke tu kuwa mnayemkejeli aliwashawatabiri kuwa uwezo wenu ni mdogo sana ktk kuchambua mambo na mmeamua kumthibitishia kuwa hamnazo, Shame on you!!!!!!

Mkuu Invicible mpaka sasa ktk ugumu huu wa kipato kuna wakati bado huwa najitahidi kununua Mwanahalisi, Raia Mwema,Rai na Tz Daima Jtano-Jpili maana kidogo hapo ninalo la kujifunza, hata kama wanamuandika Ben Netanyahu hawa jamaa wako reasonable kwa msomaji wao.

Mkuu ni maoni yangu juu ya thread hii na IPP Media, ruksa kupingana kwa hoja.
Mungu awabariki sana.
 
Kigazeti kama Alasiri kimejaa ushabiki na umbea kwa wingi. Ninaangalia vichwa vya habari zinazoongoza kila siku. Inatia kichefu chefu.

Gazeti pekee lililodumu kwa miaka mingi na hadhi yake ikabakia ni Mwananchi.
 
Mkuu Quassim, ni ukweli usopingika kwamba magazeti mengi yamekosa umakini katika habari zao. Habari nyingi wanazotoa ni zinakosa expert opinion na zaidi zinaelezea tu event in a general picture. Mfano Majira ya tarehe 14 Aug 08..Kichaa aliyeuwa wenzake asomewa mashtaka uchi..lakini ukisoma habari hii utaona kuwa haina substance yeyote kwa mtu ambaye ni analytical angependa kuisoma. kwa mfano aina ya ugonjwa wa akili mtu huyu alikuwa akisumbuliwa nao, je ilikuwa sawa kuwekwa pamoja na wagonjwa wengine etc! Angalia pia habari hata za burudani...Simba yailaza Polisi Moro, ni habari ambayo haina umakini hata kidogo! Na tatizo hili lipo hasa kwenye magazeti ya kila siku kama majira, mtanzania, nipashe ndo kabisa! Kwa mifano hiyo utaweza nielewa nanimaanisha kitu gani.
 
Mkuu Invicible ni makampuni ya IPP Media yanayoongoza kuandika habari zozote zenye lengo la kumbabua BWM, ushahidi uko wazi na pia hata yale ambayo Mengi ana hisa agenda ni hiyhiyo!!! Soma This day au Kulikoni , Nenda the Guardian, Nipashe,Acha Umbea na hata ya michezo, Ni Lete Raha lililoendesha kampeni ya kupinga Uwanja mpya usiitwe kwa jina la Mkapa mpaka wakathubutu kupendekeza uitwe Jakaya M.Kikwete, tunayaangalia magazeti haya kwa macho ya fadhaa maana sasa hata Pimbi anatambua mchezo unaofanyika.

Ninakutaka ufanye uchunguzi wako, IPP Media wanavyoziripoti habari za viongozi wa Umma wa Tz inapofika Mkapa tatizo kwelikweli na ndio maana kuna siku nilihoji JF iweje hawa jamaa wa IPP Media habari iwe ni Mkapa pale inapozungumzia yale wanayoona na mabaya yake?!! Lakini inapokuja dunia na umma ku acknowledge mchango wako they don't want to be part of it?!!!! Kumbuka kilichotokea National Stadium(The New Arena) , kwa makusudi IPP walianza kampeni za kuwaonyesha viongozi wa sasa kila mara lakini wale wachina wakaamua kuiwasha ile Runinga pale ndani ikimuonyesha Ben Netanyahu Mkapa uwanja uliripuka kama kuna goli limeingia kimiani, wao hawakuonyesha hicho kitu live siku ile mpaka siku ya pili tuliposoma baadhi ya magazeti kuwa wananchi walisahau machungu ya game mara baada ya kuonyeshwa mzee Netanyahu akikagua uwanja wakati wa mapumziko.

Ninaanza kuamini kuwa ushirika wa Msuya na Mengi na harakati za kujipendekeza kwao kwa utawala mpya ni chanzo cha yote yanayompata Mkapa, hakukosea kuwa wagomvi wake ni pamoja na wale aliwanyima mamlaka zama za utawala wake.

Invicible, Mengi anao mkono juu ya haya yanayotendwa na waajiriwa wake dhidi ya Ben Netanyahu, usipoteze muda wako kumtetea huyu tajiri kwani umma unamuangalia kwa jicho la kisirani kwa mahubiri yake na matendo yake, tulisha hoji iweje huyu afananishwe na Martin Luther King Jr, tuliongea mengi humu JF.

Mzee Mramba alichosema ni sahihi kabisa na wala hakulenga kumponda mtu wala chama chake bali ni kujiuliza kama Mtz, ameongea kwa ufasaha ,kwa dhati ya moyo wake na zaidi ametoa changamoto. Muandishi anapoamua kupotosha ,Muhariri anapokubaliana na Mmiliki anapokaa kimya bila kuchukua hatua za makusudi kurejesha imani na heshima ya mali zake unataka tusimuhoji?!!!

Mkuu black and white IPP Media ni tatizo kwa maendeleo ya habari Tz, tunamlaumu sana Rostam why?? Ni pale tunapoona media zake zinapotosha umma, why not Mengi? Ni mungu huyu au?
Alichotaka ktk kipindi cha Mkapa na kukikosa sasa amekipata kwa JK, tunamuona yuko karibu naye sana ingawaje jamii haipendezwi na hali hiyo lakini maamuzi ya Rais na tunayaheshimu, mzee wake Msuya naye kasogezwa basi inatosha kwake ,ajenge nchi na siyo malumbano yaso na hoja.

Hofu yake nini kwa Mkapa ambaye sasa si Rais wa nchi au anataka nini toka kwa huyu mzee? Issue hii Mkuu invisible inawakera wananchi wengi sana na kwa dhati ninaamini inaipotosha nchi maana umma hautaki kukubaliana na huu mchezo na muda unakwenda wakati mambo ya muhimu hayazungumzwi na tunamjadili mtu tena kwa pesa za nchi yetu.

Imetosha wakuu, sasa wahariri jaribuni kuheshimu taaluma zenu na mkumbuke tu kuwa mnayemkejeli aliwashawatabiri kuwa uwezo wenu ni mdogo sana ktk kuchambua mambo na mmeamua kumthibitishia kuwa hamnazo, Shame on you!!!!!!

Mkuu Invicible mpaka sasa ktk ugumu huu wa kipato kuna wakati bado huwa najitahidi kununua Mwanahalisi, Raia Mwema,Rai na Tz Daima Jtano-Jpili maana kidogo hapo ninalo la kujifunza, hata kama wanamuandika Ben Netanyahu hawa jamaa wako reasonable kwa msomaji wao.

Mkuu ni maoni yangu juu ya thread hii na IPP Media, ruksa kupingana kwa hoja.
Mungu awabariki sana.

TaSAVAli Mkuu FDR jr
Nahisi ulilenga kumjibu Invisible; na sio Invincible. I am really invincible. No bulls#¤%&it!
 
Back
Top Bottom