Upotoshaji wa Habari! Nani alaumiwe?

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,695
785
Ndugu Watanzania wazalendo wenzangu.

Tumefika pahali ambapo taifa linapotoshwa sana kwa kiasi ambacho tusipokuwa makini tutazalisha taifa la walalamikaji, watu wa michapo... wajadili watu tu, tusiojadili hoja... wapenda udaku, wapenda kosoa tu bila kutoa solutions... lakini yote haya huletwa zaidi na jinsi jamii inavyopotoshwa na media mbalimbali etc.

Nachelea kuuliza yafuatayo:-

1. Hivi gazeti likiandika upuuzi wakulaamiwa ni mwekezaji/mmliki au mhariri/mwandishi? Mfano... mmoja wa mwekezaji/mmliki wa mwananchi ni Aghakan ambaye hata hajui gazeti linaandikwa nini yeye anachoangalia ni je bottom line kwenye mahesabu inaonyesha kiasi gani.?.. bottom line ni mstari kwenye hesabu za makampuni unaonyesha profit after tax. Mengi pia, Rostam, na Mliki wa Majira wote... siku zote waangalia zaidi huo mstari... na wakati mwingine wanachukua muda mrefu bila kusoma magazeti yao...
Lakini tumependa kuwashambulia wamiliki as if na sisi vichaa vile.

2. Hivi JF hapa watu wanapoweka pumba, wa kulaumia ni JF management au mwekezaji/mtoa pumba zake?

3. Hivi ni lini tutatoka kwenye kujadili watu ili tuingie kwenye kujadili hoja (issues) mifumo (systems, legal frame work), sera(policies), maendeleo (development challenges), uchumi, uwekezaji, elimu, mazingira... etc.

4. Kwanini waTanzania tunakubali kurudishwa nyuma na waandishi uchara ambao wametufanya tutumie muda mwingi kujadili, Uchawi bungeni, mto aliyekula kichwa cha mtoto mwingine..., Wangwe kapigwa Risasi, Mbowe kaokolewa vs hajaokolewa, Zanzibar ni nchi vs Sio nchi, hivi hizi ndio vipa umbele vyetu kwa sasa?

5. Angalia mfano mzuri wa heading za JF: zaidi ya 60% vichwa vya habari vina majina ya Watu.... kuliko hoja, issues ...shame on us?Chonde chonde Watanzania wenzangu tukemee uandishi usio makini maana ni Sumu kubwa sana ya maendeleo yetu kama taifa.

Mungu ibariki Tanzania
Ahsanteni kwa kunisoma.

BongoTz said:
This is what you call journalism? Hebu compare hii headline iliyokuwa leo kwenye gazeti la Alasiri na utumbo ulioandikwa ndani...

Mramba amlipua Mkapa!

2008-08-13 15:47:06
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Katiaka kile ambacho pengine hakikutazamiwa kutokea, Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Tatu ya Rais Benjamin Mkapa na ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rombo, Mheshimiwa Basil Mramba, amemlipua kiaina Rais Mstaafu Mkapa kwa kuiponda Serikali yake kuhusu sera ya viwanda.

Mheshimiwa Mramba amesema Serikali hiyo ya awamu ya tatu ( iliyokuwa ikiongozwa na Rais Mkapa), kamwe haikuwahi kutekeleza sera ya viwanda.

Akizungumza bungeni jana wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Mheshimiwa Mramba akazidi kueleza kuwa kwa kasi iliyokuwepo katika serikali ya awamu ya tatu, nchi ingechukua muda mrefu sana kuwa na viwanda.

``...Nina tatizo. Najua watu watauliza, si (nawe) ulikuwepo. Lakini wacha niseme,`` ndivyo alivyoanza kueleza Mheshimiwa Mramba kabla ya kuchangia zaidi...

Hebu nisaidieni ndugu wanachi: Mramba kamlipuaje Mkapa ukisoma hiyo article yote? Na kwanini hakuzungumza chochote kuhusu serikali ya awamu ya pili ambayo pia haikufanya chochote ktk kutekeleza sera ya viwanda?

What's going here people?

I personally think, this is an excellent example of clear personal vendatta that has existed for so long between vibaraka kama vile Mramba, CCM ya Kikwete, Media (IPP/TBC1/Majira/Rai) aimed at scapegoating Mr.Clean.
 
Kuhusu awamu ya Pili na Viwanda , wa kumuuliza ni Mramba sio Mwandishi
 
Waandishi wa bongo wa magazeti hasa yale ya Kiswahili yako hivyoo... although mengine yanahakikisha yanaingiza kwa namna ambayo sio rahisi kuona...

Mramba alichosema awamu tatu (yaani ya pili, ya tatu, na ya nne), ndio maana alikua akisema only wakati wa nyenyere ndio kulikuwa na sera ya viwanda...

Sasa mwandishi akaamua... kufanya vibwanga vyake... na hilo ndilo linalotokea hapa nchini kwetu.. hata waandishi makini kama akina M. M. Mwanakijiji kuna time... wanakuwa biased... especially wakati wa kujadili chama tukufu, cherefu... sahihi kama CHADEMA.
 
I am jus finished to read the thread Mkapa ni mtu safi...Period!Then nakutana na hii hapa!!Ma brain got alerted dat kuna wa2 wako very sensitive bout Mr.Clean!They ll do anything to maintain his cleaness,wateva it ll cost em.
 
mwenye gazeti akiwa reginald mengi kuna maajabu unategemea hapo???????
Mkuu, wa kulaumiwa hapa ni Mengi au Mhariri wa Gazeti ambaye amesomea uandishi na akawa kinara wa upuuzi? Same things are happening kwenye gazeti la Majira, labda mkuu hujasoma vema wanavyojichanganya Majira. Habari moja inarudiwarudiwa mara kadhaa huku ikionesha wazi kuna target binafsi aidha za kuchafuana ama kujipendekeza kwa watu flani. Mhariri wa Majira na wa Alasiri wanatakiwa kujua kuwa kadiri wanavyoruhusu upuuzi wa namna hii ndivyo wanavyopelekea watanzania kuona kuwa magazeti haya ni ya kizushi
 
Mengi lazima awe na uchungu na chenkapa baada ya kumwekea kiwingu asiweze kununua Kilimanjaro (now kempiski) hotel na kuwapatia foreigners.
Naona anamalizia hasira zake taratibu kupitia magezeti yake.
 
Invisible... unanitoa machozi ninapokumbuka majira ya enzi zile..... za akina Nyaronyo... na wengineo. Hivi ni nini kimetokea kwenye Gazeti la majira limeshuka hadhi namna hii??? Naomba anayemjua mhariri mkuu wa majira kwa sasa aniwekee jina lake hapa!!! Ameliua na kulizika majira...
 
Mengi lazima awe na uchungu na chenkapa baada ya kumwekea kiwingu asiweze kununua Kilimanjaro (now kempiski) hotel na kuwapatia foreigners.
Naona anamalizia hasira zake taratibu kupitia magezeti yake.
Wait a minute, hivi Mengi ndo mhariri wa gazeti hilo? Sikujua mkuu.

On the other hand, kukiwa na habari ambayo inaenda kombo katika RAI, Mtanzania, Dimba, Taifa, Dimba n.k tumlaumu Rostam?

Watu twende mbali zaidi, tuwabana wahariri wanaoweza kununulika kwa maneno ama vijisenti kadhaa waache kuwa chanzo cha uzushi katika sekta ya habari kwani ni wizi wa wazi wa fedha za wananchi wanaonunua magazeti yao na ni uchochezi wa kutafuta heading ya kuuza gazeti ilhali content iliyo ndani yake siyo!
 
Invisible... unanitoa machozi ninapokumbuka majira ya enzi zile..... za akina Nyaronyo... na wengineo. Hivi ni nini kimetokea kwenye Gazeti la majira limeshuka hadhi namna hii??? Naomba anayemjua mhariri mkuu wa majira kwa sasa aniwekee jina lake hapa!!! Ameliua na kulizika majira...
Macho,

Wahariri wetu wamekuwa chanzo cha kupotea ladha ya habari. Huyu mhariri wa Majira analimaliza gazeti hivihivi. Senti kidogo wanazopokea na kuanza kuvurunda kwa kuandika habari za kiushabiki wakiweka kando maslahi ya taifa kando basi zinapoteza hadhi ya magazeti husika.

Ni kweli maisha ni magumu lakini heshima kwa fani zetu ni muhimu sana. Ukiangalia magazeti kadhaa kwa Tanzania yamekuwa yakiandika habari ambazo kwa mtu mwepesi kushtukia anaona habari zenyewe ni za kiushabiki. Majira lilikuwa gazeti credible, wanalimaliza taratibu. Tukiwa wa kwanza kuwabebesha lawama wamiliki wa vyombo hivyo tunakosea, wahariri wakuu wa magazeti haya ndo wa kubeba lawama. Same applies kwenye Television sector, kama quality ya broadcasting na programs zao hazikidhi haja basi wahusika wabanwe na walaumiwe moja kwa moja na kama kuna kulazimishwa na wamiliki basi wafanye uungwana kama uliofanywa na baadhi wa kuachia ngazi na kuanika ukweli tu ili jamii itambue nini pumba na nini mchele!
 
IPP media kwa ujumla wako na ajenda kuhusu awamu ya tatu. nina shaka kubwa wahariri wanatumika vibaya na kuidhalilisha fani yao. magazeti mengi kwa sasa yanakera na yanawafanya watanzania wengi kuwa mabegwe kiholela. Lazima tuwe analytical kwamba third term govt what we expected it to do and what has been DONE. Majungu yamewakaa hata watu ambao wanataka kuiaminisha jamii wao ni waana.
 
Jamani; haka ni kagazeti kanatoka mchana na kanauzika kwa shida kidogo. Hivyo ni lazima kawe na vichwa vya habari vyenye "mvuto" kidogo. Watanzania tu wavivu sana kusoma. Magazeti yanauzika kwa taabu!
 
IPP media kwa ujumla wako na ajenda kuhusu awamu ya tatu. nina shaka kubwa wahariri wanatumika vibaya na kuidhalilisha fani yao. magazeti mengi kwa sasa yanakera na yanawafanya watanzania wengi kuwa mabegwe kiholela. Lazima tuwe analytical kwamba third term govt what we expected it to do and what has been DONE. Majungu yamewakaa hata watu ambao wanataka kuiaminisha jamii wao ni waana.

Nyauba, unachosema ni kweli. Juzi tu kulikuwa na headline nyingine ya kipumbavu kwenye hayohayo magazeti ya Mengi " Jakaya afanya kweli," lakini ndani yake ilikuwa ni kichekesho. Ukisoma kipande chote (hapo chini), unabaki ukijiuliza: Hivi, huyu Kikwete kafanya kweli ipi wakati mafisadi wakubwa bado wanapeta mitaani kama hawana akili nzuri!

JK afanya kweli

2008-08-09 14:52:15
Na Mwandishi Wetu, Songea

Tahadhari ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Jakaya Kikwete kuwa Serikali yake haitakuwa na msamaha kwa viongozi na watumishi watakaofanya ufisadi kwa kutumia pesa za umma kwa manufaa yao binafsi, imeanza kuliza vigogo baada ya vijana wa kazi kufanya kweli na kumsweka jela kigogo mmoja.

Hatua hiyo imekuja baada ya vijana wa JK kuvalia njuga sakata la kigogo huyo, hadi kupata ushahidi wa kutosha juu ya namna jamaa huyo alivyolamba mapesa ya umma.

Kigogo huyo aliyeswekwa jela ni Mhasibu wa Shule ya Sekondari Mbinga mkoani hapa aitwaye Omari Millanzi, 56.

Mapesa hayo yaliangukia mikononi mwa kigogo huyo baada ya kutumwa na ofisi ya Hazina ili yafanye kazi ya kuboresha elimu.

Hata hivyo kigogo huyo alizinyaka pesa hizo na kuzikandamizia kwenye mambo yake mwenyewe hadi aliposhtukiwa na kuburuzwa kortini.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Ruvuma, Baptist Mhelela ndiye aliyesikiliza kesi juu ya sakata hilo na baadaye kumuona Millanzi ana hatia katika makosa 60 aliyoshtakiwa.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mhelela alisema kuwa kwa kuzingatia ombi la Mwendesha Mashtaka aliyetaka adhabu kali itolewe kwa mshtakiwa, na kwa kuzingatia vilevile kuwa mshtakiwa amekutwa na hatia ya makosa hayo yote, mahakama imeamua kumfunga jela mshtakiwa huyo kwa miaka mitatu kwa kila kosa, katika mashtaka 30 ya awali, hivyo kutakiwa atumikie jela kwa miaka 90.

Aidha, Hakimu Mhelela akasema kwa makosa mengine 30, kila kosa litampasa mshtakiwa atumikie jela kwa miaka mitano, hivyo jumla kuwa miaka mingine 150.

Jumla kuu ya kipindi cha adhabu za mshtakiwa huyo kilipaswa kuwa miaka 240 jela.

Hata hivyo Hakimu Mhelela alisema kwakuwa adhabu zote zitatumikiwa kwa pamoja, mshtakiwa atakwenda jela miaka mitano.
Pia Hakimu huyo akaamuru mshtakiwa alipe kiasi chote cha pesa alizoiba kwa mwajiri wake ambazo ni Sh. Milioni 24.1, mara tu baada ya kumaliza adhabu yake ya kifungo.

Kabla ya hukumu hiyo, upande wa mashtaka ukioongozwa na Inspekta George Omary, ulidai kuwa katika kipindi cha mwezi Januari na Julai mwaka 1998, mshtakiwa Millanzi aligushi nyaraka mbalimbali za Serikali na kuiba pesa hizo, kaisi cha Sh. Milioni 24.1.

Alipotakiwa kujitetea, ndipo mshtakiwa Millanzi alipomlilia hakimu na kumtaka ampunguzie adhabu akidai kuwa ana umri mkubwa na kuwa vilevile, ana familia inayomtegemea.

Mara kwa mara, Rais Kikwete amekuwa akisisitiza juu ya nidhamu ya matumizi mazuri ya pesa za umma na kuonya kuwa yeyote atakayekiuka taratibu, atachukuliwa hatua kali za kisheria.

SOURCE: Alasiri
 
Mkuu, wa kulaumiwa hapa ni Mengi au Mhariri wa Gazeti ambaye amesomea uandishi na akawa kinara wa upuuzi? Same things are happening kwenye gazeti la Majira, labda mkuu hujasoma vema wanavyojichanganya Majira. Habari moja inarudiwarudiwa mara kadhaa huku ikionesha wazi kuna target binafsi aidha za kuchafuana ama kujipendekeza kwa watu flani. Mhariri wa Majira na wa Alasiri wanatakiwa kujua kuwa kadiri wanavyoruhusu upuuzi wa namna hii ndivyo wanavyopelekea watanzania kuona kuwa magazeti haya ni ya kizushi

Mkuu naungana na wewe kabisa kwani Mengi ndio Mhariri?Hata kama anawatumia Wahariri wake kuchafua wengine kwa nini hao wahariri wawe so cheap to humiliate their own proffession kwa kuchafulia wengine?The right people to be blamed hapa ni wahariri ambao wameruhusu umaskini wao kuwafanya vibaraka wa matajiri!
 
This is what you call journalism? Hebu compare hii headline iliyokuwa leo kwenye gazeti la Alasiri na utumbo ulioandikwa ndani...

Mramba amlipua Mkapa!

2008-08-13 15:47:06
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Katiaka kile ambacho pengine hakikutazamiwa kutokea, Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Tatu ya Rais Benjamin Mkapa na ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rombo, Mheshimiwa Basil Mramba, amemlipua kiaina Rais Mstaafu Mkapa kwa kuiponda Serikali yake kuhusu sera ya viwanda.

Mheshimiwa Mramba amesema Serikali hiyo ya awamu ya tatu ( iliyokuwa ikiongozwa na Rais Mkapa), kamwe haikuwahi kutekeleza sera ya viwanda.

Akizungumza bungeni jana wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Mheshimiwa Mramba akazidi kueleza kuwa kwa kasi iliyokuwepo katika serikali ya awamu ya tatu, nchi ingechukua muda mrefu sana kuwa na viwanda.

``...Nina tatizo. Najua watu watauliza, si (nawe) ulikuwepo. Lakini wacha niseme,`` ndivyo alivyoanza kueleza Mheshimiwa Mramba kabla ya kuchangia zaidi...

Hebu nisaidieni ndugu wanachi: Mramba kamlipuaje Mkapa ukisoma hiyo article yote? Na kwanini hakuzungumza chochote kuhusu serikali ya awamu ya pili ambayo pia haikufanya chochote ktk kutekeleza sera ya viwanda?

What's going here people?

I personally think, this is an excellent example of clear personal vendatta that has existed for so long between vibaraka kama vile Mramba, CCM ya Kikwete, Media (IPP/TBC1/Majira/Rai) aimed at scapegoating Mr.Clean.

Mara nyingi tunawalaumu waandishi wa habari kwa jinsi habari zinavyosomeka. Watu ambao hawako 'newsroom' si rahisi kujua ni nini mwandishi wa habari aliandika na nini mhariri aliondoa au kuongeza.

Habari inapofika 'newsroom', inapaswa kwanza kupitiwa na mhariri wa habari (au msaidizi wake - senior reporter) na kwa kawaida huwa haina kichwa cha habari. News editor anaweza kuwasiliana na mwandishi ili kufanyia kazi tena ili iwe 'balanced' na akiridhika nayo huipeleka kwa sub-editor.

Huyu ndiye anayeipitia na kuisanifu huku akitafuta nini ni 'news' katika habari ile. Wakati mwingine, sub-editor, anaiandika upya kabisa na kutafuta ni paragraph ipi inaonekana kuwa 'introduction' na ipi iwe 'conclusion'. Pia tukumbuke kuwa baadhi ya vyanzo vya habari vinaficha ukweli wenyewe na kutoa tu 'secondary facts'. Mfano, unaweza kuona raia akipata kipigo cha polisi kituoni, ukienda kuuliza kulikoni, utaambiwa hakuna aliyepata kipigo na kuna vyanzo vingi tu vinaficha habari muhimu.

Hii ndiyo hali halisi wanayokumbana nayo waandishi wa habari, ambao kwa bahati mbaya wanalipwa kidogo sana.

Wakati mwingine, sub-editor anaweza kupata 'introduction' katikati ya habari yenyewe au mwishoni kabisa. Na huyu ndiye anayeweka kichwa cha habari.

Newsrooms ambazo zina wahariri wa kutosha, sub-editor akimaliza kupitia story huipeleka kwa chief-sub, ambaye anaweza kuiruhusu iende kama ilivyo au anaweza kupata maoni kutoka kwa mhariri mkuu.

Wakati huo habari hii siyo ya mwandishi tena, bali ya mhariri mkuu. Vymbo vingine vina 'revise editor', ambaye yeye ni mtaalam wa lugha (grammar, syntax, semantics, etc) na anapitia habari zote kurekebisha lugha au kuondoa makosa ambayo wahariri hawakuyaona au waliyafanya wao wenyewe.

Kwa hiyo, magazeti yanayosomeka vizuri, mara nyingi yana watu wote hawa na yale yenye shida ya lugha au habari makini - ina maana hawana watu wote muhimu na hivyo hulazimika kufanya tu kile wanachoweza - yaani kutoa gazeti. Katika mazingira haya, utakuta mwajiri au mwenye chombo cha habari husika ameshaelezwa tatizo lakini mengine kipaumbele chake siyo kuboresha taaluma au kuinua kipato cha wafanyakazi wake bali kupata faida.

Kwa bahati mbaya, baadhi ya wahariri wanashabikia mtazamo wa chama au watu fulani na hivyo wanaweza kuongeza kitu ambacho mwandishi hakukiandika kabisa. Baadhi yao wanalipwa hela nyngi tu au wanasaidiwa kwa namna moja au nyingine kwa kufanya hivyo na kwa vile hakuna asiyetaka hela - hii ndiyo inayoathiri taaluma ya uandishi wa habari na siyo elimu ya chuo kikuu kama wengine wanavyodhani.

In fact, uandishi wa habari hauhitaji elimu ya juu sana - ila unahitaji uwezo wa kutafuta na kupata habari (journalistic skills & analytical mind), kuilewa, kuifanyia kazi na kuitoa kwa lugha inayoeleweka kwa wasomaji na kulinda maadili ya kazi (ethics za uandishi: kutoa habari ya kweli na inayojenga jamii, kuandika bila kuegemea upande, kutoiba kazi ya wengine na kuifanya yako na kama ukitoa kazi ya mtu mwingine kusema ni kazi yake na ameruhusu uitumie, etc).

Kwa hiyo basi, ni maslahi binafsi au ushabiki wa kulipwa hela na shinikizo la waajiri au wamiliki wa vyombo vya habari unaoharibu taaluma ya uandishi wa habari (wakiwemo waandishi makanjanja).

Katika baadhi ya newsrooms, wahariri wanalazimishwa kutoa habari na waajiri au wamiliki wa vyombo hivyo kwa kuambiwa - habari hiyo isitoke kwenye gazeti langu kama inavyosema au ondoa hiyo, weka hii na tunawafahamu. Wapiga debe wanapatikana kwenye 'newsrooms' pia. Ni kitu cha kusikitisha lakini baadhi ya waajiri au wamiliki wa vyombo vya habari wanapenda hivyo.

Kwa hiyo, waandishi wa habari wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana ni inabidi tuwatie moyo kwelikweli. Ila wale walio na maslahi binafsi, hao inabidi tuwakosowe na kuwalaani kwa nguvu zote.
 
"especially wakati wa kujadili chama tukufu, cherefu... sahihi kama CHADEMA".

Nimeguswa sana na maneno hayo juu, kuna maswali mengi ambayo bado sijawa na uhakika na majibu ninayo fikiri kuwa yaweza kuwa sahihi. tutafika!
 
Jamani IPP wana magazeti machache ya Udaku ..... nafikiri ni lile "Acha Umbea " tu.. sasa kwa jinsi soko la magazeti hapa Bongo lilivyotawaliwa na Ununuzi mkubwa wa magazeti ya Udaku kuliko yale yaliyo serious naona ikabidi Alasiri lisimame hapo kati kati .... Udaku kama si udaku vile: Ndivyo nionavyo
 
Kasheshe! naomba nikupongeze kwa sentesi zako za mwisho maana zina kila aina ya ukweli kwa upande wangu na nimejitahidi sana kuwa nauliza majibu bila mafanikio nadhani ni vizuri pia kuyafanyia kazi hayo uliyoaandika katika msatari wa mwisho. Bravoo KASHESHE
 
Heshima zenu Wakuu,
Kwanza naona hapa hana mambo mengi ila muhimu ni kuwa Mleta mada hakukerwa moja kwa moja cha tofauti iliyomo kwenye habari na kichwa cha habari yenyewe ila ninachokiona ni "Mr. Clean asichafuliwe" pili kawalaumu sana mwandishi habari wakati katika soko la magazeti hapa nchini bila habari za namna hiyo haliuziki gazeti. WaTanzania hatupendi kusoma habari tunapenda udaku na umbeya, tunapenda habari za kimapenzi na ngono, habari za kuumbuana, hizo ndio zenye soko, hivyo waandishi wanajitahidi kulisha soko kulingana na mahitaji, hili linanisikitisha mno.
Maadili yetu wanadamu wa enzi hizi yameporomoka sana kiasi kwamba hali inatisha, tunapenda uharamia zaidi ya uhalalia naombeni tubadilike sasa.
Hali ngumu ya kiuchumi inatufanya tuwe na machungu na chuki ndani ya roho zetu na wengi wetu hatumudu kwenda kwenye burudani ajili ya kujiliwaza na kuondosha mazonge sasa panapotokea jambo lolote basi hapo ndipo pa kutolea machungu na kujifariji, ikiwa ni kumuumbua mtu ama habari za kushangaza inachukuwa nafasi ya burudani. hii ni hali mbaya na ngumu kupata tiba.
 
alichoongea mramba, kichwa cha habari na kilichoandikwa sioni tatizo!!!! serikali ya mkapa ilichemka kwenye viwanda in short
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom