Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,939
- 46,690
Kumekuwepo na upotoshaji kwamba Marekani imesitisha au imekosa pesa za kuendelea kuifadhili Ukraine katika vita yake dhidi ya uvamizi wa Urusi.
Ukweli ni kwamba Marekani haijakosa pesa za kuipa Ukraine angalau Serikali kuu ya Biden. Kinachoendela ni kwamba chama cha Republicans kimekuwa ndio chama chenye wabunge wengi tangu January mwaka huu baada ya kushinda uchaguzi wa bunge November mwaka jana na hivyo kukifanya kukalia kiti cha spika wa bunge la House of Representatives. Pia uchaguzi huo uliingiza wabunge wengi wenye mahaba zaidi kwa Trump maarufu kama MAGA.
Katika siasa za Marekani Spika ni mtu mwenye nguvu sana hasa katika bajeti kwa sababu ni yeye tu mwenye uwezo wa kupeleka muswaada wowote wa bajeti au matumizi ya nchi bungeni ujadiliwe na kupigiwa kura. Spika wa sasa kutoka chama cha Republicans na mrengo wa MAGA amekataa kupeleka bungeni muswaada wowote wa msaada kwa ajili Ukraine upigiwe kura kwa sababu kundi la wabunge wenye "loyalty" kubwa kwa Trump(MAGA) hawataki kabasa Ukraine ipatiwe pesa na ni watu wanaomuhusudu Putin kwa kiasi fulani.
Kinachoendela sasa ni Republicans ambao hawapendi sana wahamiaji wanataka Muswaada wao wa sera za mpaka upitishwe na Biden ndipo nao wapitishe Muswaada wa pesa za Ukraine. Hapo ndipo mkwamo wa msaada kwa Ukraine ulipokwamia kwa sababu kila upande unaona mwaswaada wa mwenzake haufai na hauna maslahi kwao.