Upotoshaji kuhusu kusitishwa kwa msaada wa US kwa Ukraine

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,660
46,337
Kumekuwepo na upotoshaji kwamba Marekani imesitisha au imekosa pesa za kuendelea kuifadhili Ukraine katika vita yake dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Ukweli ni kwamba Marekani haijakosa pesa za kuipa Ukraine angalau Serikali kuu ya Biden. Kinachoendela ni kwamba chama cha Republicans kimekuwa ndio chama chenye wabunge wengi tangu January mwaka huu baada ya kushinda uchaguzi wa bunge November mwaka jana na hivyo kukifanya kukalia kiti cha spika wa bunge la House of Representatives. Pia uchaguzi huo uliingiza wabunge wengi wenye mahaba zaidi kwa Trump maarufu kama MAGA.

Katika siasa za Marekani Spika ni mtu mwenye nguvu sana hasa katika bajeti kwa sababu ni yeye tu mwenye uwezo wa kupeleka muswaada wowote wa bajeti au matumizi ya nchi bungeni ujadiliwe na kupigiwa kura. Spika wa sasa kutoka chama cha Republicans na mrengo wa MAGA amekataa kupeleka bungeni muswaada wowote wa msaada kwa ajili Ukraine upigiwe kura kwa sababu kundi la wabunge wenye "loyalty" kubwa kwa Trump(MAGA) hawataki kabasa Ukraine ipatiwe pesa na ni watu wanaomuhusudu Putin kwa kiasi fulani.

Kinachoendela sasa ni Republicans ambao hawapendi sana wahamiaji wanataka Muswaada wao wa sera za mpaka upitishwe na Biden ndipo nao wapitishe Muswaada wa pesa za Ukraine. Hapo ndipo mkwamo wa msaada kwa Ukraine ulipokwamia kwa sababu kila upande unaona mwaswaada wa mwenzake haufai na hauna maslahi kwao.
 
Kwa namna yeyote ile, Ukraine haiwezi shinda hii vita , wananchi wa US nao wana akili wanaona kodi zao zinazotumwa kwenda Ukraine zinaweza kuboresha maisha yao hapo US.

Mwisho Ukraine kasaidiwa na haitoshinda hii vita, na hii wajuzi walisema toka vita inaanza, kupigana na Russia sio mchezo, upumbavu wa kudanganyana Russia ana silaha hafifu za kizamani yako wapi sasa.
 
Kwa namna yeyote ile, Ukraine haiwezi shinda hii vita , wananchi wa US nao wana akili wanaona kodi zao zinazotumwa kwenda Ukraine zinaweza kuboresha maisha yao hapo US...
Kura mbalimbali za maoni Marekani zinaonyesha theluthi mbili ya raia wa Marekani wangependelea nchi yao iendelee kuipa Ukraine msaada katika vita yake dhidi ya Urusi.
 
Kwa namna yeyote ile, Ukraine haiwezi shinda hii vita , wananchi wa US nao wana akili wanaona kodi zao zinazotumwa kwenda Ukraine zinaweza kuboresha maisha yao hapo US...
Kodi za wa USA ni ndogo mno ukilinganisha na upolaji wa majeshi yao!

Wa USA hawawezi kulalamikia kodi hata kidogo, maana wanajua, zinazokuwa ni misaada, ni za upolaji tupu
 
Katika nchi kama Tanzania na zingine za kiimla kama za kiarabu, Russia, Iran na China ndio watu wanashangaa mambo kama hayo kwa sababu mabunge yao ni mihuri tu ya kupitisha miswada ya serikali zao za kidikteta.
 
Back
Top Bottom