Upotevu wa maadili kwenye siasa ni kioo cha jamii ya leo hii

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Dunia ya utandawazi, ni tofauti na ile ya enzi zile za nyuma, wakati wa vita baridi, wakati wa chama kimoja cha siasa. Dunia ile kwa sababu ya ukosefu wa maendeleo kwa maana ya teknolojia, iliweka mipaka ya uelewa miongoni mwa watu. Mtu akisikia Russia au China alijenga picha za ajabu ndani ya mawazo yake, akadhania kwamba ni sehemu ambazo watu wake wanaishi maisha ambayo ni tofauti kabisa na ya nchini mwetu.

Kuibuka kwa teknolojia za kisasa, kumeenda sambamba na uhuru wa taasisi za kisiasa. Wakati wa chama kimoja, kauli za viongozi zinazotolewa, hazingeweza kupata mtu wa kuzikosoa. Leo hii wakati wa vyama vingi, wakati utitiri wa radio na vyama vya kijamii, kinachotamkwa na kiongozi kinakosolewa ndani ya saa 24. Kila mtu anaweza kuongea akasikika, kila mtu anaweza akamtukana mtu na akasikika pia.

Binafsi sifurahishwi na matusi yanayoandikwa kwenye mabango ya kisiasa, iwe Zanzibar iwe Bara, zifurahishwi na jinsi ambavyo watu wanavyoutumia vibaya uhuru mkubwa wa habari. Uhuru usiokuwa na mipaka, huzaa aina fulani ya uendawazimu katika jamii.

Upotevu wa maadili kwenye siasa za nchi hii, ni kitu kinachokwenda sambamba na upotevu wa maadili katika jamii nzima. Naisikitia nchi yangu, kila ninaposhuhudia watu wanajisahau na kujiona kama vile wapo juu ya kila kitu. Tuwe huru katika kuwakilisha hisia zetu na malengo yetu lakini tukumbuke kuwa uhuru unaozidi mipaka ni mtego mbaya kwetu pia.
 
Back
Top Bottom