Uporoto amewini

Hodi hooodi uwanjani, (mbuta!, alaf wanaendeleaje tena?)

Enewi, we mpotee mzazi, au siyo....

Ha ha ha.... Hicho kipaji bana... Mie hata kujaribu siwezi
 
Mkuu kumbushia zile

Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli, Iwafae masihani

Baada ya hapo mambo yatafloo!

Akatamka mgonjwa, ninaumwa kweli kweli,
Hata kama ni kuchanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa, (Baada ya hapo nilitoroka class)
 
kweli kajaiba ulipenda,cheusi mangala akakutenda
wahenga walishanena,lakini wewe hukupendwa
mpende akupendae ,hasokupenda achana nae
na usipoangalia tena utatendwa na zaidi ya kutendwa.


Uporoto si umwache,cheusi mangala ampakate?
mbona wewe ulikuwa wake na tena ukampa mate?
sasa kwanini umfate fate,na kshikshi zimpate?
yeye kesha sema anawake,tabu ya nini upate?

si kila ufatapo nyuki utapata utamu
wengine hupata manundu ,huku wakivuja damu.
sasa wewe wataka makuu na si tena utamu
ntamwambia uporoto aje akupe hatam.

si kama nakucheka kwa yalokufika
lakini napenda kukueleza,na upende kusikika,
watu wakishapendana ni ngumu kuachanika
waombee maisha mema ,huko walikofika.
 
Nitawaletea translation ya kiingereza ya haya mashairi for future use nyie naomba muendelee
 


asante babu yangu,kwa itikio ombi langu,
ipo shwari roho yangu,baada ya kupata mkungu,
tapalilia shamba langu,babu ule ndizi zangu
katu hutolala njaa,kukulinda itakua kazi yangu.

japo tupo wengiwengi,mi ntakua kiziwanda
afrodenzi ndo mpishi,mi kazi ya kuandaa
wiselady kucota maji,maty kuni kusenya
katu hutolala njaa,kukulinda itakua kazi yangu.
 
The Following User Says Thank You to Asprin For This Useful Post:

Kimey (Today)​
 
 

hodi hodi uwanjani,
shosti pearl nakusalimu kisha naomba kuteta nawe,
hapo penye blue,penzi langu na Uporoto panalihatarisha,
Uporoto alinikuta 'sijui lolote' akanifundisha kila kitu,
leo hii ukisema Kaishaijabutege alinipa mate si Uporoto atadhani nilikua nilimdanganyanilipomwambia kuwa sijui hata mate yanaliwaje?
be carefuly shosti,nikiharibu penzi langu na Uporoto sijui kama nitapata jengine kama hili ktk dunia hii.
 

Cheusie nakushauri urudi darasani kujifunza ushairi:A S kiss:
 

Ushindwe na ulegee, uongo kunizushia,
Kwa tuo nielezee, wapi kaniingilia?
Birungi nipotezee, popobawa nakemea,
Birungi wewe Mhaya, Kiswahili kwako shida.
 

Wewe ni dawa ya homa, utawaweza vimwana?,
Nakuonea huruma, ni kifupi chako kina,
Kijogoo nanguruma, dozi natoa pana,
Kijogoo nimenona, niachie kina mama.
 
ah ah ah lol
chesui nimekupata,uporoto kakamata
na hakika anakipata ,kile anachokitaka,
katu kasha mate hakupata,wala mda wa kukupakata
na kama mate angepata ,si asingekuacha?

kwa uporoto uliena,bila kujua la kutenda
nae kama mlengwa,alikuonyesha vya kutenda
nawe bila kalenda ukamuacha akatenda
na sasa kesha kupenda,huna budi kupendeka
 
si hivi nipo?haujaniona wewe wajidai tuu uyoo pengine hujui ushadodewa ulijua ntakataa nini ha hahahah lol?

Toto la kiarabu,
Umejaa ustaarabu
Wapatikana kwa tabu,
Sema neno unitibu,
Uwe wangu muhibu,
Karibu.
 

:A S kiss::A S kiss::A S kiss:
 
Duh!!..........Ngoja niwaachie malenga wetu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…