Uporoto amewini

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
chukua vyote NIACHIE Uporoto01.:angel:

Kwa hiyo yake saini, Cheusi kanisaliti,
Nimeshindwa ushindani, Uporoto ni smati,
Mangala wake mwandani, si yangu hiyo bahati,
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.

Afrodenzi jamani, nawe mfariji Mati,
Preta ukiwa kundini, nijuzeni mikakati,
Cheusi mkuwadini, Poroto apigwe buti,
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.

Uporoto huna dini, si kiumbe ni ngongoti,
Iweje unifitini, unipore langu titi?
Nitalala mang'amuni, labda nile vitoti,
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.

Wapendwa nawaageni, nimeshapigwa kibuti,
Uporoto amewini, leo anafanya pati,
Cheusi kanipiga pini, nakoma simfuati,
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.

Kaditama niahuni, nimekwaa kizingiti,
Cheusi kenda mitini, na kivulanache njiti,
JF nishaurini, nilizushe valangati?
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.
 
yote ni mipango yake maulana,
sikujua kama utasurender mapema namna hii maana nilishatekwa na hizi tungo zako,
hata hivyo bado unayo nafasi maalum moyoni mwangu na utakuwa wangu daima.
 
Duh! hii nilikuwa sijaiona jamaa kapinda kanitungia mpaka shairi ? kashai we kiboko usikate tamaa wako wengi hata hapa JF utatoka tu au labda ujaribu kwa miss Judith naona mtatongozana kimashairi zaidi nakutakia kila la heri.:yo:
 
mie sinilesema
hawa watu smart sana..
hachukui muda kashamwaga maneno...
duuhh hiii hatari..

mie najaribu kuandika poem ya kipenzi ambae namtafuta..
nimeanza kuandika mwaka 2009..
lakini ndo mistari 3 tu..
mmmmhhh labda ndo maan simpati
hahahah lol

Kashaijabutenge nakuvulia kofia tena..
Uporoto kazi kwako dear
maneno matamu hayo
na sifa umemwagiwa tena
hii wiki yako dear..
na kitamu zaidi bibie Cheusi karudi.
mmhhhh weekend hii twakuja kwako dear
 
yote ni mipango yake maulana,
sikujua kama utasurender mapema namna hii maana nilishatekwa na hizi tungo zako,
hata hivyo bado unayo nafasi maalum moyoni mwangu na utakuwa wangu daima.

Lipi lako nichukue, na lipi niliamini?,
Uporoto uko nae, wamtaja hadharani,
Ili mie nirudie, ibadilishe saini, (chukua vyote NIACHIE Uporoto01.:angel:)
Umtusi umatini, ndipo nikurudie.
 
mie sinilesema
hawa watu smart sana..
hachukui muda kashamwaga maneno...
duuhh hiii hatari..

mie najaribu kuandika poem ya kipenzi ambae namtafuta..
nimeanza kuandika mwaka 2009..
lakini ndo mistari 3 tu..
mmmmhhh labda ndo maan simpati
hahahah lol

Kashaijabutenge nakuvulia kofia tena..
Uporoto kazi kwako dear
maneno matamu hayo
na sifa umemwagiwa tena
hii wiki yako dear..
na kitamu zaidi bibie Cheusi karudi.
mmhhhh weekend hii twakuja kwako dear

Nambie Afrodenzi, nirushe yangu ndoana?
Nasumbuka na mapenzi, nipate wangu kimwana,
Mwingine nimpe tenzi, Cheusi tumeachana,
Afrodenzi kimwana, likubali langu penzi.
 
chukua vyote NIACHIE Uporoto01.:angel:

Kwa hiyo yake saini, Cheusi kanisaliti,
Nimeshindwa ushindani, Uporoto ni smati,
Mangala wake mwandani, si yangu hiyo bahati,
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.

Afrodenzi jamani, nawe mfariji Mati,
Preta ukiwa kundini, nijuzeni mikakati,
Cheusi mkuwadini, Poroto apigwe buti,
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.

Uporoto huna dini, si kiumbe ni ngongoti,
Iweje unifitini, unipore langu titi?
Nitalala mang'amuni, labda nile vitoti,
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.

Wapendwa nawaageni, nimeshapigwa kibuti,
Uporoto amewini, leo anafanya pati,
Cheusi kanipiga pini, nakoma simfuati,
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.

Kaditama niahuni, nimekwaa kizingiti,
Cheusi kenda mitini, na kivulanache njiti,
JF nishaurini, nilizushe valangati?
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.

Kashaija ndugu yangu, nakugea zangu pole,
Ulienda wanguwangu, ukajikwaa kidole,
Alichokipanga Mungu, kiwezi kuwa kipele,
Jaribu tena kwingine, Cheusi kwako haramu.

Ila onyo nakugea, Siguse jukuu wangu,
Usije tena kulia, Nikiwarudisha kwangu,
Wajukuu nimelea, wanitunze peke yangu,
Jaribu tena kwingine, Cheusi kwako haramu.

Afrodenzi angalia, simuweke mawindoni,
Maty wala Roselia, na mwanajamiiwani,
Waisiledi achia, na wengineo sebuleni,
Jaribu tena kwingine, Cheusi haramu kwako.

Dada zangu nakwachia, ukiwaweza chukua.
Preta nakuzawadia, Nyamayao naye pia,
LD kiwezea, Lili Flawa Fukuzia,
Mahari ulete kwanza, Babu ninazipokea
 
Nambie Afrodenzi, nirushe yangu ndoana?
Nasumbuka na mapenzi, nipate wangu kimwana,
Mwingine nimpe tenzi, Cheusi tumeachana,
Afrodenzi kimwana, likubali langu penzi.

Nilikukanya mapema, hautaki kusikia?
Usilete lelemama, utakuja kujutia,
utakipata kihama, jukuu ukimendea,
Ninakutahadharisha, wajukuu usiguse.
 
hili foramu jamani halikosi vimbwanga,
kila nikizama ndani nabaki nazimiaga
utasikia fumanizi na kule mtu katengwa
kashaija we jasiri kumwaga mwenzi hadharani.

ulipoanza mfukuzia hukumtungia shairi
mkala kwa kuibia sasa wasema umeghairi
uporoto kakuingilia au hauna umahiri
kashaija we jasiri kumwaga mwenzi hadharani,

aspirin babu nilinde nami niwe kijukuu,
utakula vilivyo na shibe kwani sina makuu
tena busara unipe niwaepuke fataki wakuu
kashaija we jasiri kumwaga mwenzi hadharani
 
aspirin babu nilinde nami niwe kijukuu,
utakula vilivyo na shibe kwani sina makuu
tena busara unipe niwaepuke fataki wakuu
kashaija we jasiri kumwaga mwenzi hadharani

Birungi karibu kwangu, ulinzi ni yangu fani,
Amenijalia Mungu, Hebu toka mashakani,
Utakula na wanangu, ukiingia kambini,
Ombi lako mesikia, Birungi jukuu wangu.

Thenksi nimekugongea, ili upate amini,
Kuwa nimekupokea, hapa kwangu kibandani,
Njoo upate tulia, kashaija sikuwini,
Ila usijisahau, babu akalala njaa.
 
Hodi hooodi uwanjani, (mbuta!, alaf wanaendeleaje tena?)

Enewi, we mpotee mzazi, au siyo....
 
Hodi hooodi uwanjani, (mbuta!, alaf wanaendeleaje tena?)

Enewi, we mpotee mzazi, au siyo....

Mkuu kumbushia zile

Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli, Iwafae masihani

Baada ya hapo mambo yatafloo!
 
Back
Top Bottom