Upo uwezekano wa mtoto mchanga kubadilika na kuwa albino kutoka katika hali ya kawaida ya mwili aliyozaliwa nayo

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Hali hii nimeishuhudia kutoka kwa mtoto wa jirani yangu. Alizaliwa akiwa wa kawaida tu, lakini baada ya mwaka ngozi yake ilibadilika taratibu na kuwa ya albino totally ikifuatiwa na mabadiliko katika macho

Kisayansi hii imekaa vipi?
 
HABARI

KUNA UWEZEKANO wa vitu kadhaa ambavyo Vinaweza vikawa vilitokea kulingana na Swali ulilouliza na ntavielezea kwa Mujibu wa swali lako hapo chini baada ya maelezo ya utangulizi....

Japo Nitapenda kuanza kwa Kusema kuwa Mpaka sasa hakuna Uwezekano Wowote kwa Mtu kuzaliwa Akiwa kawaida na kubadilika baadae kuwa albino...

Kwanza Muhimu kujiuliza Ualbino ni nini?
Ualbino ni Matatizo au Wengine huita ugonjwa wa kurithi Unaotokana na Mwili kukosa madini ya Melanini (Melanocytes) hivyo kufanya Mwili wa muathirika kuwa mweupe ukiambatana na Matatizo mbalimbali yanayoathiriwa na madini hayo ikiwemo macho,Nywele na Ngozi..

Kwa maelezo uliotaja ulimaanisha mtoto huenda ana albinism iitwayo Oculocutaneous albinism (Albinism inayohusisha macho na ngozi na ndo common sana) Sasa ili mtoto mtoto azaliwe na ualbino huo Lazima arithi vinasaba kamili "recessive Gene" za Albinism kutoka kwa wazazi wake wote wawili (Ambao wote Lazima wawe wame beba Gene hizo za ualbino "carries for Albinism genes")..

MAJIBU YA SWALI LAKO..

1.Kwanza
Kulingana na Scenario Uliotoa, kama Wazazi walikuwa na Vinasaba "Recessive gene" Za albinism ni Kwa asilimia kubwa sana huenda mtoto alikuwa na Ualbino ila wahusika wali "overlook" dalili mbalimbali za Ualbino kwa mtoto akiwa mdogo,
Wazazi Wengi sana sana wanaozalia majumbani Hushindwa kugundua Dalili hizi mapema na Hugundua dalili hizi pindi mtoto amekuwa mkubwa,Na Hapa Ndo huja changamoto kama ulizoelezea Kwenye uzi wako...

2.Pili mtoto anaweza Akawa na Congenital Vitiligo (Neonatal Vitiligo)
Unaweza ukaita unavyotaka wewe Congenital vitiligo au Neonatal vitiligo au Paediatric vitiligo...😉

(Congenital maana yake -a kuzaliwa .......Neonatal -a kuzaliwa -a utoto...... na paediatric maana yake -ya utoto)
Vitiligo ni ugonjwa Wa ngozi Ambao unasababisha Ngozi ya mwili Kuwa nyeupe Sana Kutokana na kuvunjwa au kuharibiwa kwa Madini Au pigmant za Melanocytes (ambazo ndo hutoa Rangi ya ngozi)..

Vitiligo pia inaweza ikaathiri Mpaka "Mucus Membranes" Tishu zilizo katika macho,Ulimi na pua hivyo kuathiri utendaji kazi wake....
japo mpaka sasa haijulikani hasa Nini husababisha Vitiligo kutokea japo inaaminika kuwa huenda hutokea kutokana na Kile huitwa "Auto immune disorder" yaani Mwili kuzalisha Antibodies nyingi ambazo huenda kushambulia Tishu zake.

Mtu mwenye Vitiligo huanza kuonekana na Kubadilika kwa Rangi na kuwa mweupe kusiko kawaida katika baadhi ya sehemu za mwili mikononi, miguuni ,Tumboni kichwani mgongoni na sehemu zingine na baadae husambaa mwili mzima,Na hata huanza kugusa nywele na kuonekana nyeupe...

NB:Vitiligo sio Sawa na Albinism Na wala Albinism sio sawa na Vitiligo Japo huwenda Kuna wakati Zinaweza zikafanana kwa baadhi kimuonekano

SASA NINI KIFANYIKE...

Mshauri Jirani yako kumpeleka mtoto Hospitali Ili kupata uhakika ikiwemo kufanya vipimo Vya vinasaba ili kupata uhakika Wa Hizi condotion mbili..

Japo magonjwa yote hayana Shida wala sio magonjwa ya kuambukizwa ila kama ni Albino apate ushauri mzuri jinsi ya kumuhudumia

Asante

Cc: Melki the Storyteller
 
Back
Top Bottom