Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,851
- 7,767
Kiongozi Mkuu wa upinzani na chama chake cha Sierra Leone peoples party wametangazwa washindi wa marudio ya kura za urais.
Julius Maada Bio ameshinda kwa asilimia 51 dhidi ya 48 ya Samora Kamara wa chama tawala cha All peoples Congress. Bwana Bio aliwahi kuwa kiongozi wa mapinduzi wa kijeshi wa nchi hii ya Africa magharibi january 1996 ambapo mwaka huohuo March 1996 aliruhusu uchaguzi kufanyika bila yeye kugombea huku wakati huo akiwa kijana Mbichi kabisa.
Alimpindua rafiki yake kijana mdogo kabisa Valentine Strasser huku kipindi hicho yeye akiwa makamu wa Rais. Valentine Strasser ameipindua serikali mwaka 1992 akiwa ni kijana mwanajeshi wa miaka 25 huku akiwa na cheo cha chini sana jeshini cha private na baadaye kujipa captain baada ya kutwaa madaraka. Maisha yake yalikuwa ya anasa sana na nchi iliingia kwenye umaskini na mdodoro wa kiuchumi ambapo rais mteule wa sasa alimpindua.
Valentine Strasser kwa sasa ni miongoni mwa marais wastaafu wanaoishi maisha magumu sana duniani huku akiishi nyumbani kwa mama yake akiomba msaada kwa ndugu na anakunywa pombe za kienyeji. Nyumba hii yadaiwa ni duni mno na mama aliridhi kutoka kwa marehemu mumewe.
Marais waliofuatia hawakumwonea huruma kwani alipora Mali nyingi na almasi ya nchi kipindi chake lakini hakujenga hata nyumba ya kuishi na pesa zote alikula na wanawake na alikuwa na safari nyingi nje ya nchi kwa ajili ya starehe. Wasieraleone walimchukia sana hadi alipopinduliwa na rafiki yake Bio. Mawaziri wake ni matajiri mno akiwepo Bio lakini yeye hakujua umihimu wa kuwekeza kipindi hicho kutokana na hela zake nyingi za uporaji lakini pia cha ajabu kutokana na anasa hakuoa na hana familia hadi Leo. Pia alitoa maelekezo watu wengi wauliwe hasa waliompinga kutokana na utawala wake mbovu.
Rais wa chama tawala ndugu Ernest Bai Koroma amemaliza mhula wake wa miaka 10 na anaondoka huku chama chake kikishindwa uchaguzi.
Nitazidi kuja na updates hadi kuapishwa kwake.
Rais Julius Maada Bio ameshaapishwa kuwa Rais wa Sierra Leone huku mgombea wa chama tawala Samora Kamara akipinga ushindi wake na ajiandaa kuchukua hatua za kisheria.