Upinzani wamtaka Sumaye...

Upinzani wamtaka Sumaye...

Status
Not open for further replies.
Joined
Jan 22, 2014
Posts
12
Reaction score
3
CHADEMA wamtaka Sumaye kuchukua nafasi ya Lowassa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kipo katika mazungumzo na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, katika harakati za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Chadema kumkibilia Sumaye inafuatia hali ya afya ya mgombea urais wa UKAWA, Edward Lowassa ambae inadaiwa kadri siku zinavyozidi kwenda mbele na hali yake inazidi kuwa dhoofu.

“Sumaye ni chaguo namba mbili iwapo mgombea wetu anatishindwa au kuishia njiani, basi mara moja muungano wetu uendelee na mapambano ya kuchukua nchi,” alisema mmoja wa viongoz wakuu wa UKAWA.

Hali ya afya ya viongozi wa UKAWA imeingiwa hofu kufuatia hali ya afya ya Lowassa, hatua ambayo imefanya vikao vya siri kufanyika usiku kwa zaidi ya siku nne sasa kutafuta mbadala wake.

Imedhihilisha kuwa Lowassa mbali na afya yake lakini hataweza mtiti wa uchaguzi unaotarajiwa kufungua panzi Jumamosi ijayo kwa vyama vyote kuanza kampeni.

Hivi karinu kumekuwa na uvumi ya Sumaye kuhamia Chadema, lakini waziri mkuu huyo mstaafu amekuwa kimya bila ya kusema lolote.

Hata hivyo wiki iliyopita kauli ya kumkaribisha Sumaye kujiunga na Chadema ilitolewa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, muda mfupi baada ya Sumaye kumaliza hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kanisa la Lole la Usharika wa Mwika, Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Hatua ya Mbowe kumkaribisha Sumaye kujiunga na Chadema inafuatia kauli aliyoitoa Waziri Mkuu huyo mstaafu wiki iliyopita kwamba mahasimu wake kisiasa ‘wanampakazia’ kwamba yeye ni maskini wa kutupwa, hivyo hana uwezo wa kuwapa fedha wanaomuunga mkono katika kupinga rushwa ya uchaguzi, ufisadi na aina nyingine ya uovu kwa jamii ya Watanzania.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu mstaafu (Sumaye), kama nilivyokwisha tangulia kukuomba radhi, huko ulipo ni pagumu, karibu kwetu kwa sababu sisi tunakemea rushwa wazi wazi, tena bila ya kificho, tumekemea rushwa siyo leo, siyo jana. Tuko tayari kufanya kazi na wewe kwa sababu unakemea rushwa, tunakupongeza na karibu sana,” alisema Mbowe mbele ya viongozi mbalimbali wa kisiasa na dini akiwamo Mkuu wa Kanisa hilo nchini, Askofu Dk. Alex Malasusa.

Mbowe alisema kwamba maneno aliyozungumza Sumaye ameyatafakari kwa kina na kujiuliza maswali mengi kwa kuwa maneno hayo siyo mepesi sana kuyasikia hasa kwa viongozi ambao wamekuwa na mamlaka ya kikatiba kuwaongoza Watanzania.

Alisema kuwa hoja ya rushwa inayotolewa na Sumaye, ni ya msingi sana na haki katika taifa la Tanzania ni bidhaa adimu na kwamba wanaotetea haki wengi wao huipata kwa gharama ya maisha yao.

“Kwa watu ambao tuko katika active politics (siasa hai), tunaona namna siasa zinavyobadilika na kuwa ni mambo ya kutishia uhai wa watu. Wenzetu viongozi wa Kanisa mtusaidie kuomba ili tusije tukajenga misingi ya kulipasua taifa hili kwa itikadi ya vyama vya siasa,” alisema na kuongeza:

“Haya ni mambo ya kupita na Mheshimiwa Sumaye siasa ni kazi ya kupita kesho CCM inaweza isiwapo na Chadema ikawapo…njoo sasa Chadema.
 
CCM mwaka huu mtakuja na kila aina ya propaganda lakini watanzania wamekwishawaelewa! Hamtafanikiwa!
 
Breaking News:CHADEMA wamtaka Sumaye kuchukua nafasi ya Lowassa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kipo katika mazungumzo na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, katika harakati za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Chadema kumkibilia Sumaye inafuatia hali ya afya ya mgombea urais wa UKAWA, Edward Lowassa ambae inadaiwa kadri siku zinavyozidi kwenda mbele na hali yake inazidi kuwa dhoofu.
“Sumkaye ni chaguo namba mbili iwapo mgombea wetu anatishindwa au kuishia njiani, basi mara moja muungano wetu uendelee na mapambano ya kuchukua nchi,” alisema mmoja wa viongoz wakuu wa UKAWA.
Hali ya afya ya viongozi wa UKAWA imeingiwa hofu kufuatia hali ya afya ya Lowassa, hatua ambayo imefanya vikao vya siri kufanyika usiku kwa zaidi ya siku nne sasa kutafuta mbadala wake.
Imedhihilisha kuwa Lowassa mbali na afya yake lakini hataweza mtiti wa uchaguzi unaotarajiwa kufungua panzi Jumamosi ijayo kwa vyama vyote kuanza kampeni.
Hivi karinu kumekuwa na uvumi ya Sumaye kuhamia Chadema, lakini waziri mkuu huyo mstaafu amekuwa kimya bila ya kusema lolote.
Hata hivyo wiki iliyopita kauli ya kumkaribisha Sumaye kujiunga na Chadema ilitolewa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, muda mfupi baada ya Sumaye kumaliza hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kanisa la Lole la Usharika wa Mwika, Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Hatua ya Mbowe kumkaribisha Sumaye kujiunga na Chadema inafuatia kauli aliyoitoa Waziri Mkuu huyo mstaafu wiki iliyopita kwamba mahasimu wake kisiasa ‘wanampakazia’ kwamba yeye ni maskini wa kutupwa, hivyo hana uwezo wa kuwapa fedha wanaomuunga mkono katika kupinga rushwa ya uchaguzi, ufisadi na aina nyingine ya uovu kwa jamii ya Watanzania.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu mstaafu (Sumaye), kama nilivyokwisha tangulia kukuomba radhi, huko ulipo ni pagumu, karibu kwetu kwa sababu sisi tunakemea rushwa wazi wazi, tena bila ya kificho, tumekemea rushwa siyo leo, siyo jana. Tuko tayari kufanya kazi na wewe kwa sababu unakemea rushwa, tunakupongeza na karibu sana,” alisema Mbowe mbele ya viongozi mbalimbali wa kisiasa na dini akiwamo Mkuu wa Kanisa hilo nchini, Askofu Dk. Alex Malasusa.

Mbowe alisema kwamba maneno aliyozungumza Sumaye ameyatafakari kwa kina na kujiuliza maswali mengi kwa kuwa maneno hayo siyo mepesi sana kuyasikia hasa kwa viongozi ambao wamekuwa na mamlaka ya kikatiba kuwaongoza Watanzania.

Alisema kuwa hoja ya rushwa inayotolewa na Sumaye, ni ya msingi sana na haki katika taifa la Tanzania ni bidhaa adimu na kwamba wanaotetea haki wengi wao huipata kwa gharama ya maisha yao. “Kwa watu ambao tuko katika active politics (siasa hai), tunaona namna siasa zinavyobadilika na kuwa ni mambo ya kutishia uhai wa watu. Wenzetu viongozi wa Kanisa mtusaidie kuomba ili tusije tukajenga misingi ya kulipasua taifa hili kwa itikadi ya vyama vya siasa,” alisema na kuongeza:
“Haya ni mambo ya kupita na Mheshimiwa Sumaye siasa ni kazi ya kupita kesho CCM inaweza isiwapo na Chadema ikawapo…njoo sasa Chadema.”

Bado sana hujawa na nguvu ya ushawishi wa jambo!
 
Damu ni nzito kuliko maji, Tamaa mbele mauti nyuma. Leo saa sita mchana, Waziri Mkuu wa awamu ya tatu, FREDRICK TLUWAY SUMAYE atatangaza rasmi kujiunga na chama cha CHADEMA, uamuzi alioufikia baada ya kukutana na EDWARD NGOYAI LOWASSA na kumhakikishia kuwa lazima ashinde na asiposhinda DAMU ITAMWAGIKA.
Pamoja na Tamaa ya Madaraka aliyonayo Sumaye na ukweli kwamba wanatoka Kanda moja na Lowassa kuwa miongoni mwa sababu za Sumaye kuamua kuhamia CHADEMA kwa kivuli kwamba anamfuata Lowassa, PIA ATAKUWA AMEFIKIA UAMUZI HUO ILI KUJISALIMISHA MAPEMA KWA LOWASSA KWA VILE YEYE(SUMAYE) ni miongoni mwa watu WALIOMPIGA SANA LOWASSA KUWA NI FISADI. SUMAYE ameamua kuweka silaha chini na kujisalimisha.
Sumaye ana lipi jipya atakalowaongezea CHADEMA zaidi ya sifa ya Uwaziri Mkuu Mstaafu tu?
Kila la heri SUMAYE huko uwendako, ila uangalie usiende kuwa kero kwa wenye chama kama walivyokero akina ESTER BULAYA, MKONGORO MAHANGA, SAIDI MKUMBA, KAFULI n.k.

Tamaa Mbele Mauti NYUMA.
 
Invisible na Moderator kuna watu mnawafuga sana na pia kuacha waaandike hata uzushi na Maneno ya hovyo,mleta mada anaandika uchochezi,chuki na uvunjivu wa Amani na sio mara moja lakini ni sawa tu!!!

Anaweza kuweka source na kuthibitisha huo UMWAGAJI DAMU??!!

Aliyeua watu Zanzibar hadi wengine wakawa wakimbizi Mombasa ni Lowassa??!!

Mwembechai ni Lowassa??!!

Mauaji ya Mwangosi ni Lowassa?!!
 
Last edited by a moderator:
Ndo unaleta habari au majungu?? Mbona nyinyi hamsemi chama kimekuwa cha mwenyekiti na familia yake!? Wengine ni vyambo tu humo ndani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom