Upinzani waanza kumdai mrithi wa Prof. Muhongo

Upinzani waanza kumdai mrithi wa Prof. Muhongo

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
upload_2017-8-4_10-31-21.jpeg

Mbunge wa Jimbo la Kibamba, ambae ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, akiongea katika mkutano wa hadhara Jumatano 2/8/2017 eneo la Goba mwisho katika Jimbo la Kibamba, amemtaka Rais Magufuli ateue Waziri wa Nishati na Madini ili aongoze majadiliano kuhusu madini.

“Ni muda mrefu umepita Rais hajateua Waziri wa Nishati na Madini, ambaye ndiye anayestahili kuongoza majadiliano kuhusu madini, badala yake anamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kuongoza majadiliano kuhusu masuala ya madini, Ameamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kwa sababu alikuwa kwenye tume ya mabadiliko ya Katiba, nae amekataa kuendeleza mabadiliko ya katiba mpya” amesema Mnyika.

Amesema Serikali makini isingeanza na makinikia huku madini yanaendelea kuchimbwa na kutoka, wakati kuna makampuni mengine yanaendelea na uchimbaji, na kampuni inayoingoza kwa uzalishaji ni kampuni ya Geita Gold mine (GGM) na inaendelea na uchimbaji hakuna ufuatiliaji wala majadiliano yeyote yanayoendelea, huku Taifa likielekezwa kwenye majadiliano kuhusu makinikia badala yafanyike majadiliano kuhusu madini kwa upana wake.
 
Ameshasema hapangiwi kazi...!!! Kama vip kamshike sharubh
 
Siku hizi hata mawaziri hawana kazi kwanza..miradi yote inazinduliwa na raisi mwenyewe.kifupi mawaziri wamekuwa vibogoyo
 
Halafu utasikia jinsi watavyolalamika akishateuliwa huyo waziri, Utadhani wanaliahidiwa kuwa atatoka chadema.
 
Waziri wa nishati na madini yupo. Nchi za kidikteta raisi huwa pia waziri wa wizara anazotaka yeye.
 
View attachment 557729

Mbunge wa Jimbo la Kibamba, ambae ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, akiongea katika mkutano wa hadhara Jumatano 2/8/2017 eneo la Goba mwisho katika Jimbo la Kibamba, amemtaka Rais Magufuli ateue Waziri wa Nishati na Madini ili aongoze majadiliano kuhusu madini.

“Ni muda mrefu umepita Rais hajateua Waziri wa Nishati na Madini, ambaye ndiye anayestahili kuongoza majadiliano kuhusu madini, badala yake anamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kuongoza majadiliano kuhusu masuala ya madini, Ameamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kwa sababu alikuwa kwenye tume ya mabadiliko ya Katiba, nae amekataa kuendeleza mabadiliko ya katiba mpya” amesema Mnyika.

Amesema Serikali makini isingeanza na makinikia huku madini yanaendelea kuchimbwa na kutoka, wakati kuna makampuni mengine yanaendelea na uchimbaji, na kampuni inayoingoza kwa uzalishaji ni kampuni ya Geita Gold mine (GGM) na inaendelea na uchimbaji hakuna ufuatiliaji wala majadiliano yeyote yanayoendelea, huku Taifa likielekezwa kwenye majadiliano kuhusu makinikia badala yafanyike majadiliano kuhusu madini kwa upana wake.
Teh!😀 Teh!😀 Teh!😀 cheki CHADEMA wanavyo tapatapa kutafuta agenda ya kudumu
Wanagusa gusa kila kitu, na vyote vinawashinda
Mara ajenda ya kupinga udikitekta, Mara ajenda ya kuwapigania waislamu, Mara uchumi, Mara rasilimali za taifa
 
Wapi mnyikaaa, enzi zile ulikuwa ukishusha nondo mpk napata uchungu kwa uzalendo na nchi yangu, leo hii umekuwa kituko hata hoja ya msingi huna alimradi tu umeambiwa uko kimya sn. Una hofu ukisogea runingani watakudai ushahidi ulonao wa kutosha wa yule fisadi.
 
Chadema wana kazi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo kazi ya upinzani ndugu yangu, kutafuta loop holes. Kimsingi wizara inatakiwa iwe na waziri. Kwanini Rais hateui waziri kwenye wizara ya nishati? Kuepuka kuonekana anazidi kujirundikia madaraka, (Kama ambavyo tayari anafanya), angemteua waziri ili hata kama atampa commands anazotaka yeye lakini ijulikane. Kwa wenye akili tayari watajua kuwa, rais ana kinga ya kutoshtakiwa, na moja kato ya wizara zenye kizungumkuti mojawapo ni hiyo ya nishati na madini, nyingine ni utalii na mali asili. Rais anapoamua kutoteua waziri ni a strtegic move ili afanye maamuzi ambayo yakija kuhojiwa mbele ya safari ionekane waziri hakuwepo, Rais ndiye alifanya. Kama alifanya Rais then mnamfanyaje? Ana kinga! Hata very soon huko utalii na mali asili nako atadaka mtu na hatateua then atakuwa tayari wizara zote nyeti ziko ofisini kwake. Tayari nishati ipo, utumishi na seriakli za mitaa ipo kwake, bado mali asili na utalii. Chadema kama chama cha upinzani, kiko sahihi kudai maana, aliyeko karibu na wananchi na wabunge ni waziri siyo Rais. JPM aliyomfanyia JK wakati anamwambia Kafulila komaa, kuhusu swala la Escrow, yatamtesa sana, na anaogopa yatammaliza hata yeye. Siku zote muosha huoshwa. Tatu, waziri ni mbunge sawa na mbunge mwingine. Kwahiyo wanapodai kuwateuliwa kwa waziri, ni sawa na wanataka mbunge mwenzao (tene miongoni mwao maana mkuu alishamaliza kuteua wake) awe waziri, ni nani? na ana msimamo gani? Si kazi rahisi sana. Mwisho, kati ya mambo mkuu anayahitaji kuliko kingine chochote sasa hivi ni pesa, tena cash siyo ahadi za kwenye makaratasi. Wizara hii ina pesa na yeye amesema tumeibiwa sana kupitia wizara hii. Ni ngumu sana kuteua mtu kwenye wizara yenye mshikemshike ambao ni mbichi. Angependa kuumaliza aweke pesa mfukoni au ajue inaingia kiasi gani ili akimteua waziri ajue hatapigwa panga. Lakini yoote haya hufanyika kwenye sehemu ambayo utawala wa sheria na good governance kuna mushkeli.
 
mIMI NADAHANI KATIBA INAMRUHUSU KUJIPA HUO UWAZIRI, ANEJIPA TU AHTA ULE UJAI MKUU ANGEJIPA PIA JAPO KATIBA HAIRUHUSU.
 
Nadhani bado anatafuta mtu sahihi, tuvute subira.
 
Back
Top Bottom