Upinzani wa Tanzania haujawahi kufanikiwa katika jambo lolote lile dhidi ya dola, nini tatizo?

Hv kwann viongoz wa africa n walaf wa madaraka?.....hawaheshm demokrasia kabsaa.....lakn kinachoangusha upinzan n uwoga na ujinga wa watu.....uwoga kwakuwa watz hawana hata ushrkiano wanaish tu kwakuwa bado wako hai....na ujinga kwakuwa watu weng hawajaelemika haswa kuhusu masuala ya kiukomboz.....CCM itatawala kwa mabav kwa miaka ming sana tz....
Mkuu Kabla Hujasema Afrika Kuna Ulafi Wa Madaraka Hebu Jiulize,

- Kama Madaraka Ya Chama Cha Siasa Ni Matamu Sana Mpaka Mtu Anakatalia Madarakani

- Leo Unashangaa Mtu Kukatalia Madarakani Kinchi ?

- Vipi Kuhusu Utamu Wa Ikulu Si Ataigeuza Nyumba Ya Familia
 
SABABU ZA KUSHINDWA KWA UPINZANI TANZANIA.

- Vyama Vya Upinzani Tanzania Ni Kama Kampuni Au Kampuni Binafsi Za Watu, Wanazitumia Kupiga Pesa Kutoka Kwa Serikali Ya CCM Na Wazungu

- Kama Wewe Sio Ndugu, Kabila Au Kutoka Eneo Fulani Hupati Faida Yoyote Hata Kama Utapigana Kwa Damu Kupigania Chama, Unless Uwe Na Maslahi Fulani Kisiasa Kwao Ref. Tundu Lissu Na Lowassa

- Upinzani Hawana Raslimali Watu Wa Maana Unaoweza Kuwaona Kama Watu Wa Serikali Mbadala Zaidi Ya Kuendesha Vyama Vyama Vyao Kijasiriamali Jasiriamali

- Yaani Ili Kuonesha Kuwa Upinzani Hakuna Watu, Mtu Ambaye Ndani Ya CCM Anaonekana Hafai Kabisa - Mtu Huyo Ni Hot Cake Ndani Ya Upinzani, Yaani Ganda La Muwa La Jana - Chungu Kaona Kivuno

- Vyama Hazina Ushirikishi Wa Watu Wote Kama Ilivyo CCM Kama Dini, Kabila, Mikoa,kanda Nk

- Kutokuwa Wakweli, Kuwa Na Unafiki Uliokubuhu.

Haya Ni Machache Tu Ya Kwanini, Upinzani Tanzania Ni Majanga - Yaani Ni Bora Tuwe Na CCM Mlemavu Wa Mguu Mmoja Kuliko Upinzani Ambao Ni Kiwete Kabisa.[/QUOTE
Yote uliyoorodhesha hapa hayana hata punje ya ukweli!
 
Ulichokisema Na Kukiamini Ni Kweli Na Ndio Maana Upinzani Tanzania Hautakaa Ufanikiwe Kama Unaamini Kama Wewe

- Siku Wakibadili Fikra Na Kufanya Tofauti , Utayaona Mabadiliko
 
Sisi tu waoga mmno! Tunapenda kuishi kuliko kuriski maisha tukitiahiwa tunatishika, tumejaaa unafiki tu!
 
Hivi haiwezekani kani kwenda mahakamani kudai
Tume huru ya uchaguzi
Na katiba mpya?!

Wanasheria tuelimisheni kwenye hili
 
GSam naona akili yako matope matupu,hata Tanzania ni lini wapinzani wamewahi kushika dola halafu wakashindwa kuongoza? Nchi zote maskini za Afrika hazijawa tayari kwa mfumo wa vyama vingi.Wapinzani wote katika Afrika wanaonekana kama ni maadui katika serikali zilizoko madarakani ndio maana kila kukicha wanasakamwa tu.Angalia katika nchi zilizoendelea ambako vyama pinzani na vilivyoko madarakani wanavyopokezana kutawala.Huwezi kusikia chama kilichoko madarakani kinanyanyasa vyama vingine ambavyo haviko madarakani.Vyama pinzani vikipewa fursa ya kuongoza haviwezi kushindwa kwani hawa wanaongoza wao dawa ya kufanikiwa kutawala waliipatia wapi ambako wapinzani hawawezi kuipata???.
Umesema kweli! Ukweli bado tuna safari ndefu sana. Kuna tatizo pande nyingi kuanzia kwa wapiga kura, walioko madarakani, wanaosimamia kura; nakdhalika. Ukisoma baadhi ya michango humu, ambayo inatoka kwa hao wapiga kura unaweza kuelewa kuwa wengi wetu tunapiga kura bila kuelewa ni kwanini tunapiga kura! Nadhani kuna tatizo la uelewa, na hili ndilo linachangia CCM kuendelea kuwa madarakani. Sio kweli, hata chembe, kwamba CCM ipo madarakani kwa sababu ya udhaifu wa upinzani, bali ni kwa sababu ya udhaifu wa wapiga kura.

Tumeona juzi wenzetu kule Ghana. Hawa waliishabadilika kitambo, tume iko huru na wapiga kura na taasisi nyingine haziruhusu upuuzi wa "magoli ya mkono"! Hii yetu ni nchi ya ajabu kidogo, watu wazima wanashangilia kuona kiongozi anasimama kutamba kwamba "hata kwa goli la mkono" lazima washinde, huku pembeni unamsikia mwingine akizungumza tena ndani ya Bunge kwamba "hatuiachii nchi kwa makaratasi"!

Sasa kujadili hoja hii inahitaji kuangalia mambo kadhaa. Lakini lililo muhimu kwangu ni kwamba tatizo kubwa zaidi liko kwa aina ya wapiga kura tuliopo hapa nchini. Wengi wetu hatujui thamani ya kura. Na tunaowapigia kura wanalifahamu hili, japo kidogo kidogo kuna mabadiliko ambayo yanawashtua wapenda kuongoza. Na ndio maana unaona leo kuna maamuzi yanatolewa kwa lengo la kuwafurahisha wapiga kura hata kama yana athari kubwa za kiuchumi, kijamii, mahusiano ya kimataifa; nakadhalika. Ref suala la wamachinga na wachimbaji wa madini.

Hata hivyo, kwamba wapinzani hawajahi kufanikiwa katika jambo lolote dhidi ya dola ni hoja ya ajabu kidogo, labda kama aliyeileta haishi hapa nchini tangu awamu ya pili ya uongozi wa serikali. Najaribu kufikiri hivyo kwa kuwa, mambo mengi yamefanywa na upinzani yakaitikisa serikali na matokeo yake yanaonekana. Na kwa kuwa mtoa mada anaonekana kuguswa na utendaji wa awamu hii ya serikali, ni muhimu afahamu kuwa kama kuna mambo yanafanywa na serikali yakamfurahisha yeye na familia yake, ajue ni kwa sababu ya uwepo wa upinzani imara hapa nchini! Unapokuwa na upinzani dhaifu huwezi kuona kiongozi mkuu wa serikali anakesha usiku kucha bila kulala akichunguza majina ya wateuliwa!
 
Huenda hata wenzetu Uganda wakaja kufanikiwa katika harakati zao dhidi ya dola mapema zaidi kwa kuangalia kuliko Tanzania.

Mbali na upinzani wa Tanzania kuwepo kwa takribani miaka 24 sasa, haujawahi kufanikiwa katika jambo lolote lile ulilopigania dhidi ya dola. Achilia mbali kumbukumbu kuwa upinzani wa Tanzania umekuwa katika harakati nyingi kwa muda mrefu kupita nchi nyingi za ukanda huu.

Kenya walianza wakaweza, na sasa pengine ndilo taifa lenye demokrasia pana zaidi baada ya mataifa kama Ghana na Afrika kusini. Wenzetu Uganda, DRC, Burundi wanaonekana kuwa ni wapinzani thabiti kuliko sisi Tanzania.

Je, ndani ya upinzani wa Tanzania kumepandikizwa virusi? Hata katiba na tume huru tu ya uchaguzi wameshindwa kudai kweli? Wanaonekana kuwa na dira kwa sasa? Waweke wapi uthabiti na waanze na lipi? Kina nani wawe msitari wa mbele?

Mbowe na viongozi wengine wa upinzani waelewe kuwa mengi ya wanayodai hawatapewa kama pipi. Ni lazima wao walale kwanza rumande tena isiyo ya kitoto.Wapewe virungu vya kutosha bila kukata tamaa na wapitie msoto kama wenzao kina Raila na wengine! Wakiogopa hilo basi wasubiri kizazi chenye uthubutu kije kufanya hayo ila wasitarajie badiliko lolote bila kutoka jasho tena jasho litakaloonekana hata na mtoto mchanga aliyezaliwa leo!!
Uhuru wetu wenyewe hatujatolea damu wakati wengine tunajua walichopitia
 
Sisi tu waoga mmno! Tunapenda kuishi kuliko kuriski maisha tukitiahiwa tunatishika, tumejaaa unafiki tu!
Sisi Sio Waoga Ila Tunachagua Vita Za Kupigana, Hatuko Tayari Kupigania

- Katiba Mpya

- Bunge Live

- Mikutano Ya Kisiasa

- Kata Funua, Ukuta

Hayo Yote Ni Mahitaji Ya Wanasiasa Ambao Wanawaza Uchaguzi 24/7 Ili Wapate Madaraka Wapate Pesa Wapeleke Ndugu, Watoto Na Mademu Zao Dubai

- Sasa Ni Watanzania Gani Wajinga Waumie Kwa Faida Ya Mtu Fulani ?
 
SABABU ZA KUSHINDWA KWA UPINZANI TANZANIA.

- Vyama Vya Upinzani Tanzania Ni Kama Kampuni Au Kampuni Binafsi Za Watu, Wanazitummia Kupiga Pesa Kutoka Kwa Serikali Ya CCM Na Wazungu

- Kama Wewe Sio Ndugu, Kabila Au Kutoka Eneo Fulani Hupati Faida Yoyote Hata Kama Utapigana Kwa Damu Kupigania Chama, Unless Uwe Na Maslahi Fulani Kisiasa Kwao Ref. Tundu Lissu Na Lowassa

- Upinzani Hawana Raslimali Watu Wa Maana Unaoweza Kuwaona Kama Watu Wa Serikali Mbadala Zaidi Ya Kuendesha Vyama Vyama Vyao Kijasiriamali Jasiriamali

- Yaani Ili Kuonesha Kuwa Upinzani Hakuna Watu, Mtu Ambaye Ndani Ya CCM Anaonekana Hafai Kabisa - Mtu Huyo Ni Hot Cake Ndani Ya Upinzani, Yaani Ganda La Muwa La Jana - Chungu Kaona Kivuno

- Vyama Hazina Ushirikishi Wa Watu Wote Kama Ilivyo CCM Kama Dini, Kabila, Mikoa,kanda Nk

- Kutokuwa Wakweli, Kuwa Na Unafiki Uliokubuhu.

Haya Ni Machache Tu Ya Kwanini, Upinzani Tanzania Ni Majanga - Yaani Ni Bora Tuwe Na CCM Mlemavu Wa Mguu Mmoja Kuliko Upinzani Ambao Ni Kiwete Kabisa.
Hivi haiwezekani kani kwenda mahakamani kudai
Tume huru ya uchaguzi
Na katiba mpya?!

Wanasheria tuelimisheni kwenye hili

ww sijawahi kukuona ila nima hakika ww utakuwa ni mzee. hizi propaganda za kizee.
 
SABABU ZA KUSHINDWA KWA UPINZANI TANZANIA.

- Vyama Vya Upinzani Tanzania Ni Kama Kampuni Au Kampuni Binafsi Za Watu, Wanazitumia Kupiga Pesa Kutoka Kwa Serikali Ya CCM Na Wazungu

- Kama Wewe Sio Ndugu, Kabila Au Kutoka Eneo Fulani Hupati Faida Yoyote Hata Kama Utapigana Kwa Damu Kupigania Chama, Unless Uwe Na Maslahi Fulani Kisiasa Kwao Ref. Tundu Lissu Na Lowassa

- Upinzani Hawana Raslimali Watu Wa Maana Unaoweza Kuwaona Kama Watu Wa Serikali Mbadala Zaidi Ya Kuendesha Vyama Vyama Vyao Kijasiriamali Jasiriamali

- Yaani Ili Kuonesha Kuwa Upinzani Hakuna Watu, Mtu Ambaye Ndani Ya CCM Anaonekana Hafai Kabisa - Mtu Huyo Ni Hot Cake Ndani Ya Upinzani, Yaani Ganda La Muwa La Jana - Chungu Kaona Kivuno

- Vyama Hazina Ushirikishi Wa Watu Wote Kama Ilivyo CCM Kama Dini, Kabila, Mikoa,kanda Nk

- Kutokuwa Wakweli, Kuwa Na Unafiki Uliokubuhu.

Haya Ni Machache Tu Ya Kwanini, Upinzani Tanzania Ni Majanga - Yaani Ni Bora Tuwe Na CCM Mlemavu Wa Mguu Mmoja Kuliko Upinzani Ambao Ni Kiwete Kabisa.
safi sana kiongozi umeeleza vyema pia jambo lengine upinzani wana tamaa ya madaraka mtu amekua mwenyekiti tangu chama kinaanzishwa mpaka sasa ina maana hakuna watu wengine wenye sifa na vigezo ili kushika uenyekiti mpaka awe yeye kila siku,
ukanda nadhani umesha elezea,siyo watu wenye dhamira ya kweli bali wapo hapo kwaajili ya kupata fedha tu
 
Back
Top Bottom