Upinzani unaleta maendeleo...

Upinzani unaleta maendeleo...

Ba'mdgo

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2012
Posts
230
Reaction score
46
Naamini mtakubaliana nami kuwa kila penye upinzani kuna maendeleo yawe ni ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kitamaduni. Ukifuatilia hili ninalosema pengine hapa kwetu tanzania au nchi za wenzetu utagunduwa hilo, nijaribu kutoa mifano angalo kwa kiasi kidogo kusupport ninachoamini.Angalia nchi kama Marekani na Uingereza ambako upinzani ni kubwa sana wa kisiasa na angalia mafanikio ya nchi hizo.Ukija hapa kwetu Tanzania, angalia mikoa au sehemu ambayo imethubutu kuwepo kwa upinzani wa kisiasa angalia mafanikio ya sehemu hizo nilinganisha na mikoa/ sehemu bado wamekuwa waoga au wagumu kukaribisha upinzani katika maeneo yao utakubaliana nami kwa hilo; mfano ya mikoa ambayo upinzani umepenya, Mwanza, mbeya, arusha, iringa, kilimanjaro na mikoa mingine ninayoamini maendeleo yatatinga katka mikoa yao kwa kasi baada ya kuimarika kwa upinzani ni kigoma, na shinyanga.....hata wanyewe wanakuambia kigoma ya leo sio hile ya zamaniHapo linganisha na mikoa ambayo upinzani kama aupo, mfano.. Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga, Songea.HUU NI UKWELI MTUPU, JARIBU KUANGALIA KWA TANZANIA WAKATI UPINZANI UJAIMARIKA KAMA SASA MAMBO LALIKUWA YANAENDA KIOLELA, KIUBABE, KUTOFUATA SHERIA NA UFISIDI MKUBWA, JAPO YAJAISHA ILA KIDOGO WAPINZANI WANAIBANA AU KUIKUMBUSHA SERIKALI YALE YASIYOENDA SAWA
 
Ni kweli kabisa, hakuna maendeleo pasipokuwa na ushindani. Mfano mzuri ni huyu spika wa bunge letu Anna Makinda huenda angesifiwa kama akina Adam Sapii Mkwawa kama kusingekuwa na upinzani. Lakini fursa ya upinzani imempa fursa ya kukutana uso kwa uso na THE DON HIMSELF,,,, Tundu Lissu...

Tuwape nafasi wapinzani wachukue nchi 2015 tupime ewezo wao, wakichemsha 2020 tunawapiga chini, ndio maana ya maendeleo.

Ushindani ni muhimu sana kwa maendeleo, ikumbushe wakati mitandao ya simu inaanza wakati Tritel wanauza bonge la mshindi la analojia kwa laki 6 lakini leo hii unapata mchina ya dijitali kwa elfu 20 tu. Tuanchane na ANALOJIA CCM tuhamie DIJITALI CHADEMA
 
Ni kweli kabisa, hakuna maendeleo pasipokuwa na ushindani. Mfano mzuri ni huyu spika wa bunge letu Anna Makinda huenda angesifiwa kama akina Adam Sapii Mkwawa kama kusingekuwa na upinzani. Lakini fursa ya upinzani imempa fursa ya kukutana uso kwa uso na THE DON HIMSELF,,,, Tundu Lissu...Tuwape nafasi wapinzani wachukue nchi 2015 tupime ewezo wao, wakichemsha 2020 tunawapiga chini, ndio maana ya maendeleo. Ushindani ni muhimu sana kwa maendeleo, ikumbushe wakati mitandao ya simu inaanza wakati Tritel wanauza bonge la mshindi la analojia kwa laki 6 lakini leo hii unapata mchina ya dijitali kwa elfu 20 tu. Tuanchane na ANALOJIA CCM tuhamie DIJITALI CHADEMA
Laine ya simu ilikuwa sh 15,000.. sasa 500/=
 
Back
Top Bottom