Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,742
- 40,874
Njia sahihi ya upinzani nchini kuweza kuzuia au kusahihisha yale yote yanayofanywa na Rais Magufuli sasa hivi ni wao kujiandaa na hatimaye kuja na mtu wao ambaye atakuwa Rais na atabeba ajenda zao.
Haitoshi tu kusema Magufuli amefanya hili vibaya au hili anafanya siyo sahihi na kuwa ni baya kwa nchi na wakati huo huo bado watu wanasubiria Rais huyo huyo na chama chake watatue matatizo ambayo upinzani umekuwa unalalamikia. Hatari yake ni kuwa upinzani ni kama umekubali kuwa "wakosoaji wakuu" wa utawala wa sasa kwa ajili tu ya kuwa wakosoaji wakuu.
Kwamba, wao hawana nia, uwezo wala mipango ya hatimaye kuunda serikali na hivyo basi wamekubali kuendelea kutoa mawazo ya kushindana na walioko madarakkani. Hili tunaliona Bungeni na nje ya Bunge; na sasa imekuwa ni kama ndugu zetu wanataka kuridhika kuonekana wamerudi kwenye miaka ya baada ya uchaguzi wa 2005. Kwamba, kazi yao ni kuibua kashfa, kupinga serikali na kushindana na Rais aliyeko madarakani. kwamba, wao waonekane ndio wenye kuthubutu kutoa maneno makali tu na kuonesha wana hasira sana na uzalendo.
Hili sina tatizo nalo kwani inawezekana wakawa wanaona mambo mengi vizuri zaidi bila kuwa na hofu ya kumuudhi kiongozi wao wa chama.
Hata hivyo, binafsi naamini kuwa tatizo hili la upinzani litawasumbua sana hadi pale watakapoamua kujioangalia kimkakati (strategic self-reflection) na wajiulize kama haya yote yanawasaidia ama kupata mgombea mzuri wa Urais mwaka 2020 na kama haya yote yanawasaidia kupata wagombea wazuri kwa serikali za Mitaa 2019 na uchaguzi wa wabunge 2020.
Hata iliyopo ni kuwa wanaweza kujikuta wanarudi tena wabunge wale wale wa upinzani (na nyongeza y a wachache) au wanaweza kujikuta wakapoteza hata kidogo kilichop na hivyo hivyo kufikia 2020 bado watakuwa wanaendelea na ajenda yao ya ukosoaji na siyo uongozi.
Nikiangalia naona makosa mengine makubwa yanayofanywa sasa na ndugu zetu hawa yanaathari zaidi kwa upinzani kuliko kwa Magufuli na kwa hakika inaonekana hayataidhoofisha CCM. Kwa wale ambao tunajua tatizo letu kubwa la kiutawala nchini limekuwa ni sera za CCM kuendelea kukazia haya mambo mengine bila kuidhoofisha CCM siyo njia sahihi ya kuweza kupata wagombea bora wa nafasi mbalimbali za uongozi.
Maswali yafuatayo yanahitaji kutafakariwa na kutafutiwa majibu:
Sasa hivi ni mwaka 2017 mwezi Juni na imebakia miaka kama mitatu kamili tu kabla ya Bunge kuvunjwa kupisha Uchaguzi Mkuu wa 2020. Je, muda huu unatosha kuweza kumpata, kumuandaa na kumjenga mgombea Urais wa upinzani (hapa namaanisha zaidi CHADEMA)?
Je, haja ya upinzani kuweza kushirikiana inahitaji kusubiri hadi muda gani ili iweze kufanyiwa kazi. Wengi tunakumbuka jinsi gani wakati wa joto la uchaguzi la 2015 jinsi gani CHADEMA na washirika wake walivyojikuta wanachukua maamuzi ambayo yamewagharimu imani ya wananchi wengi kwao. Kuanzia suala la kumpata mgombea wao wa Urais, Mgombea mwenza, na hata masuala ya kiutawala ambayo mengi hayakuwa wazi wakati wote wa kampeni. Je, kosa hili litarudiwa tena?
Je, inawezekana kwa mara nyingine tena upinzani unasubiri na kutafuta mgombea wake wa Urais ambaye atatoka CCM na siyo aliye ndani yake tayari? Na kama mtu huyu yupo CCM, anasubiriwa nini kabla ya kujiunga na upinzani au itasubiriwa aonekane akikatwa jina lake tena? Inawezekana mgombea fulani kijana akaamua kuja upinzani kutoka CCM ili kuipa CHADEMA mgombea anayekubalika na wana CCM vile vile?
Je, njia sahihi ya kujijenga kuelekea 2020 ni ipi bila kujiweka wenyewe matatizoni au kupunguzi nafasi ya kujikuta kwenye matatizo?
Yapo na maswali mengine ambayo yanahitaji majibu hasa kwa vile kutoyauliza ni jambo jingine linaloweza kutishia upinzani zaidi sasa hivi.