Upinzani Tanzania umenunuliwa rasmi

Upinzani Tanzania umenunuliwa rasmi

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
7,341
Reaction score
18,102
Rais Samia jikite kufungua na kuanzisha miradi, jikite kupambana na mfumuko wa bei, jikite kuhamasisha viwanda .
Viwanda ndiyo vitanunua mazao ya wakulima ,viwanda ndiyo vitazalisha ajira nyingi sana.
Huwezi kupeleka nchi uchumi wa kati kwa kukutana na Mbowe mara kwa mara.
Juzi Prof Lipumba amenukuliwa akisema Rais Samia atashinda kwa kishindo mwaka 2025!!
Zito Kabwe ndiyo hivyo tena amekuwa kasuku wa ccm kila siku ni kusifia tu.
James Mbatia ndiyo hivyo tena kutwa kusifia mama anaupiga mwingi.

Inasikitisha sana chadema kununuliwa, Lisu na Lema huko wanakolelewa wamekuwa kama misukule hawajui washike lipi waache lipi maana mwenyekiti wao hatabiliki, muda wowote anabadili gia angani kama alivyofanya mwaka 2015 kwa kununuliwa na Lowasa.
Mbowe alipotoka tu jela akakimbilia Ikulu kwenda kunywa chai badala ya kuwashukuru kwanza waliompigania!!.

Sasa tumaini pekee liliobaki kwa wapenda mabadiliko na ulinzi wa kweli wa rasilimali za nchi yetu ni UMOJA PARTY.
Mungu ibariki Umoja party ipate usajili haraka .
 
Ni fursa nzuri kwa Pro JPM wajipange kuandaa mgombea makini.
 
Mama anafikiria ushindi wa mezani. Ameshindwa kutafuta ushindi wa kuwatumikia watanzania. Anajua ameshafeli. Hata kina JK aliowaamini kwa sasa hawasikiki tena. Kinana ndio anazidi kudhiifika. Karma kitu mbaya sana. K
 
CHADEMA wakiaandaa maandamano mnawaita chama Cha fujo. Wakikaa kwenye mazungumzo mnasema wamenunuliwa. Ebu tushauri wafanyeje ili uridhike.
Hawa huwa wanaipenda sana serikali ikiwa na mtu dhaifu, maana wanaipeleka wapendavyo.
 
Elewa kwamba huyu ni mtanzania mwenye mila na desturi za ki-Zanzibari. Subiri muda wake uishe labda ataingia mwenye haiba ya bara ndo tutaweza kurudi uchumi wa kati. Kwa sasa utasikia maneno laini tu kama royal tour, uchumi wa kidijiti, uchumi wa buluu, kufungua nchi( wakati ilikuwa uchumi wa kati) n.k
 
CHADEMA wakiaandaa maandamano mnawaita chama Cha fujo. Wakikaa kwenye mazungumzo mnasema wamenunuliwa. Ebu tushauri wafanyeje ili uridhike.
Wakaze buti, naona wamekubali walishikwa pabaya.

Mwananchi ambae haijui SIASA bora asiijue na asiifatilie kabisa maana ni mchezo wa ajabu sana, huwezi kuelewa wala kuamini kama vyama pinzani wanatupigania sisi wananchi au maslahi yao. Tuishi tu hivyo hivyo maana hakuna namna tena.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli usemavyo. Lakini naomba utoe ushauri wafanyeje.
 
CHADEMA wakiaandaa maandamano mnawaita chama Cha fujo. Wakikaa kwenye mazungumzo mnasema wamenunuliwa. Ebu tushauri wafanyeje ili uridhike.
Hii mijitu ya CCM, haiwezi kuisha kupiga propaganda, kwao kila kitu ni kibaya.

Imagine Kila leo hawaishi kumwandama Mbowe kuwa ni Mwenyekiti wa kudumu wa Chadema, kwa huyo ang'atuke.

Lakini hata siku moja huwezi wasikia wakimwambia Augustine Mrema, wa TLP, ambaye amekigeuza hicho chama kama "his own property" ang'atuke!🥺
 
wanasiasa ni Kama KINYONGA.
huu urafiki wa Samia na chadema tuombe Mungu tufike 2025.
 
Kama yule Mfanyabiashara ya utumwa alishindwa kuinunua CHADEMA kwa fedha za mikopo, hakuna atakayeweza. Samia ana mapungufu yake tena mengi lakini kwa hili anafanya lililomshinda yule mwenye Roho ya kutu.
Hivi zile hela za project ya kununua wapinzani zilienda wapi? Au wameachiwa wajane zake ndo maana wanasumbue humu.
 
Back
Top Bottom