Upinzani nchini

Pamoja na kwamba wamezuiliwa bado mi naamini kulikua na njia mbadala wa kudeal na hayo makatazo kwa njia ya amani na watawala wakawaelewa kuliko njia walizotumia za kutukana na kukejeli.

Ivi kweli Leo hii wewe mbunge wa chadema au mwanachama kamati kuu ya act wazalendo ukamkejeli mbowe au zito kabwe tuone kama atakuacha salama Basi vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa watawala.

Kwa hiyo njia ya halali haikua ya kukejeli na kutukana.Hiyo ni sawa na enzi zile tulivyokua mashuleni tukidai kubadilshiwa vyakula hauwezi kufikisha ujumbe huo kwa kumtukana mkuu wa shule kwenye school baraza hata Kama hoja yako inamashiko lahasha kwa sababu hawezi kukusikiliza Zaid zaidi atakutimua shule kwa utovu wa nidhamu.
 
Hivi na wewe ujiona umetoa maoni!
 
Hawajapewa muda wa kufanya hayo what next.................
 
Kwani mkuu CCM wanatumwa na mabwana zao wepi hao?
Akili yako inakomea kwenye vyama. Wenye upeo wanafikiri zaidi ya hapo, kwakuwa wanaotumika kutimiliza azma za mabwana nilio wataja, hawako kwenye vyama pekee, hata nje ya vyama; na kwa maana hiyo, sisi tunawapima kwa matendo yao. Wanaweza kuwa ndani ya vyama vyote vya siasa, taasisi za kidini, vyama vya kiharakati, vyama vya kitaaluma, taasisi za serikali n.k

Ni mara chache taasisi kusajiliwa ikijipambanua kuwa ni kuwadi au kibaraka wa mabwana hao, bali nia hiyo hujificha kwenye malengo mazuri yaliyo andikwa. Ili uwabaini, lazima uchunguze kauli zao, matendo yao, mienendo na tabia zao, n.k

Hivyo kwa kiwango kikubwa, viongozi katika vyama (upinzani) japo si wote, ila walio wengi na viongozi wakubwa, wameonesha pasi na shaka, kukengeuka katika utamaduni, imani, falsafa na desturi asili ya vyama hivyo na kuanza kuenenda, na kutamka yale ambayo kwayo, yanatufanya kujiridhisha kuwa sasa wako kwenye project ya mabwana wale; na ndiyo maana wameacha sasa kuhubiri na kusimamia yale ambayo mtoa mada ya msingi ameelezea na kuanza kubeba agenda zisizo wahusu watanzania bali mabwana wale.

Soma; Intarnational relations(by Emmanuel Wallestain).
 
Kumbuka mwanzisha uzi anaongelea kuhusu wapinzani na ndani yake ametaja yale ya CCM. Tayari anaongelea vyama hata kama wengine wanahusika walengwa wakuu ni vyama vya upinzani. Mfano huu hapa chini.
- Waeleze namna gani wataboresha shule za kata zilizojengwa na serikali ya CCM ikiwa ni pamoja na kuzipatia vifaa vya maabara vya kutosha au kuzifanya zifanane na shule kongwe nchini ambazo kipindi cha nyuma ziliaminika ni shule za vipaji maalumu.
Kama uzi ni kuhusu wapinzani na wapinzani wakuu au wanaofahamika ni vyama sioni wewe unakikmbilia wapi. Ili hao unao waita mabwana zao wafanye yao na kieleweke vyama lazima vihusike (kwa siasa za Tanzania). Hivyo usijifanye wewe una upeo kuliko wengine kwenye hili kwani mada ya msingi ni kuhusu wapinzani, ili waje na sera mbadala kama mleta uzi anavyo shauri ni lazima vyama vihusike. Kumbuka hata wagombea huru hatuna Tanzania.
Swali langu-kwa vile wewe umeona wapinzani hawana agenda bali ajenda za bwana zao, yaani kwa ufupi unasema watanzania hawawezi kufikiri-sasa tuambie CCM wao wanafikiriwa na nani? Mabwana zao ni nani?
 
Sawa wameichoka lakini pamoja na hayo wananchi hawaoni mbadala wa kuwapeleka nchi ya ahadi Mana wote wanaonekana ni wachumia tumbo tu.Yaani afadhali ya walioko madarakani kuliko hao
 
Sawa wameichoka lakini pamoja na hayo wananchi hawaoni mbadala wa kuwapeleka nchi ya ahadi Mana wote wanaonekana ni wachumia tumbo tu.Yaani afadhali ya walioko madarakani kuliko hao
Kama wananchi hawaoni mbadala CCM ingeacha tu sanduku la kura liamue kiuhalali tuone mambo yatakavyo kwenda.Acha kukaririshwa na fix za kina slowslow!
 
Una uelewa wa mambo na maarifa pia hoja lakini umekosea taget ulipoilekeza hoja yako
 
Nadhani kabla hujauliza usome aya yangu ya mwisho nilivyo hitimisha; ila inategemea upeo na utayari wa akili kuelewa.
 
Nadhani kabla hujauliza usome aya yangu ya mwisho nilivyo hitimisha; ila inategemea upeo na utayari wa akili kuelewa.
Bado inaongelea vyama na hili ndio msingi wa bandiko lako. Hoja ya upeo na utayari wa akili kuelewa hiyo ni ya kwako usihamishe magoli.
 
Bado inaongelea vyama na hili ndio msingi wa bandiko lako. Hoja ya upeo na utayari wa akili kuelewa hiyo ni ya kwako usihamishe magoli.
Sasa mbona ulisema kuwa swala hili nataka kulielekeza kwingine na sio vyama wakati hitimisho langu limetanabahisha kwa vyama vya upinzani? Ndiyo maana nikakuelekeza usome aya ya mwisho. Akili ikikosa utayari wa kuelewa madhara yake ni hayo.
 
Sasa mbona ulisema kuwa swala hili nataka kulielekeza kwingine na sio vyama wakati hitimisho langu limetanabahisha kwa vyama vya upinzani? Ndiyo maana nikakuelekeza usome aya ya mwisho. Akili ikikosa utayari wa kuelewa madhara yake ni hayo.
Uliandika: "Akili yako inakomea kwenye vyama. Wenye upeo wanafikiri zaidi ya hapo, kwakuwa wanaotumika kutimiliza azma za mabwana nilio wataja, hawako kwenye vyama pekee, hata nje ya vyama; na kwa maana hiyo, sisi tunawapima kwa matendo yao". Sioni hapa tunabishania nini. Ahsante na kwa heri.
 
Lazima uage maana huna uwezo wa kujadili kwa akili bali kelele; sasa kona niliyokupeleka ni kwa wenye akili. Hata hivyo machache niliyokueleza yamekusaidia kuwa mstaarabu hata kwa kuaga kwa uungwana, nakushukuru sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…