Upinzani na Mafisadi - CHADEMA Hapa Wameboronga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upinzani na Mafisadi - CHADEMA Hapa Wameboronga!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Uncle Rukus, Sep 28, 2010.

 1. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi sina vita yeyote na upinzani hasa CHADEMA, lakini CHADEMA
  kumuingiza Marando na kumpa jukwaa kuongea na wananchi siliafiki.

  Mimi nimekuwa nikuwafuatilia sana wanasiasa wakiwepo wa upinzani.
  maswala mazima ya usafi na kukubalika kwao na jamii. Uchafu kwa wana
  CCM ni jambo la kwaida, tumelizoea lakini kwa upinzani tunategemea
  kuona mfano usafi. Kuwa mbali na ufisadi au uchafu wa aina yeyote.

  Wapo baadhi ya wanasiasa kuanzia kwa Nyerere na hata mpaka sasa
  wanajulikana kwa usafi wao na wengine kwa uchafu wao. Nyerere kuwaita
  Akina marando na wenzake maumbwa wakati wa enzi ya Lyatonga na NCCR
  Mageuzi sio jambo la kunyamaza kimya. Nyerere aliwajua fika kuwa
  hawafai hata kwa lolote. Ndio maana alimwita Lyatonga akamwambia
  kagombee ubunge maana huko NCCR huna watu.

  Bila kupoteza muda, mimi wasiwasi wangu ni huu, Marando ataleta jipya
  gani CHADEMA? Au ndio hayo mafarakano aliyoyaacha NCCR wakati wa Mrema
  na baada yake? au ndio akina LAMWAI wanaotanguliza tumbo kwanza ndio
  Watanzania baadaye?, Mimi nina mwona Marando kama mwanasiasa wa Tumbo
  akipata cha tumbo humuoni tena. CHADEMA wajihadhari, kwa sababu yeye
  ni Mtanzania anayo haki ya kujiunga na chama chochote, lakini asipewe
  madaraka mpaka aondoke mwenyewe. Huyo ni traitor na hatatufaa upinzani
  hata kidogo. ANgerudi tu CCM kama wenzake

  Nawashauri akina mbowe, Slaa na wazee wa chama waliangalie sana hili
  kabla halijaleta mafarakano
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Angalisho zuri hili.
   
 3. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  naona hujui unalosema
   
 4. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shut up! Hujui kuwa hii forum unatakiwa kusifia Chadema tu. :lol:
   
 5. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Si ni Nyerere huyo huyo ndiye alituaminisha Mkapa ni Mr Clean na leo hii kadhia ya ufisadi inayolididimiza taifa iliasisiwa na huyo mteule wa mjuvi Nyerere?
  Acha kuja na hekaya za Abunuwasi hapa. Marando ni mzalendo kuliko wengi wenu.
   
 6. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Aisee! nimegundua hilo now! ila kwa style hii hatutafika popote.
   
 7. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Subirini muone uzalendo wake.
   
 8. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tumeshauona hatuhitaji kusubiri
   
 9. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Siwezi kubishana na wewe maana naona uelewa wako ni mdogo sana kwenye haya maswala.
   
 10. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwenye uelewa mkubwa utaletaje mifano inayokinzana? Jibu hoja acha kuleta vioja. humuamini Marando kwa sabau Nyerere hakumwamini, lakini ni Nyerere huyo huyo aliyetulisha kasa kwa Mkapa.
   
 11. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #11
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  wanataka tumwamini makamba na kyabo.
   
 12. magessa78

  magessa78 JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 28, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani CHADEMA wamelamba dume maana Marando alikuwa mkuu wa usalama wa Taifa huko nyuma.kwa vyovyote vile anaijua idara hiyo na watu wake,so ni rahisi kwake kupata habari nyingi zinazoihusu CHADEMA ndani ya usalama na kuzileta huku CHADEMA na kueleza nini kinaendelea.Ndo maana CHADEMA inagundua mambo mengi ya siri toka CCM
   
 13. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  crap
   
Loading...