Upinzani na karata ya TANGANYIKA

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Chama kama Chadema kinaweza kuvuna wanachama wengi ikiwa tu watasimamia kwa uwazi urudishwaji wa Serikali ya Tanganyika ,Yaani kwa hapa tulipo karata ya kuirudisha Tanganyika ni dume lisiloshindika.

WaTanganyika mna tatizo moja ambalo ni kuogopa kuirudisha Serikali ya Tanganyika ,au tuseme kuiondoa serikali ya Tanganyika nyuma ya pazia la Muungano. SIelewi wale G55 wamepotelea wapi au wamepatiwa fupa na hivyo wapo katika kushughulikia ulaji huo wa fupa.

Wiki iliyopita kazuka MTanganyika ambae ataenda mahakamani kudai uwepo wa Tanganyika ,kuna sherehe za Uhulu ,sherehe hizi za Uhuru ni za Uhuru wa Tanganyika ,Fedha inayotumika ni fedha ya serikali ya Muungano ,hapa vipi ??

WaTanganyika kama WaTanganyika ni lazima mumuunge mkono huyo jamaa ,kwa hali na mali ili irudi Tanganyika na kuliondoa hili jinamizi linaloitwa Muungano.

Lipo tatizo ambalo litahitaji kupapartuana na utawala uliokuwepo CCM, na serikali zake kwani kurudi kwa Tanganyika ni kuvunjika kwa serikali iliopo madarakani ,serikali ya Muungano.

Kuwadhibiti mafisadi nalo ni tatizo iwapo Tanganyika itarudi ,hawa mafisadi nao hawapo tayari kuona Tanganyika inarudi wanajua wazi watakuwa na wakati mgumu kuliko wakati wowote ule katika maisha yao.

Chama kama Chadema kinaweza kuvuna wanachama wengi ikiwa tu watasimamia kwa uwazi urudishwaji wa Serikali ya Tanganyika ,Yaani kwa hapa tulipo karata ya kuirudisha Tanganyika ni dume lisiloshindika.
 
Nadeclare intrest. Mimi ni M4C. Sababu moja wapo ya kuipenda CDM ni CDM kupenda Tanganyika. Sasa nasema hivi:
Bila Tanganyika hakuna katiba mpya wala amani.
 
Back
Top Bottom