Upinzani Kutumika Kukwamisha Juhudi Za Rais Magufuli katika Suala Madini

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Kuna dalili tosha kwenye kambi ya upinzani wameanza kutoa taarifa za kupotosha hatua aliyechukua Rais Magufuli katika masuala ya madini.

Rais aliunda tume ya wasomi waliobobea na wao wakatoa mapendekezo kwa Rais na akalipeleka kwa Spika kwanini tuanze kumlaumu Rais kwa juhudi zote hizo.

Tundu Lissu acha kuwadangaya watanzania kama upo kwenye payroll ya Acacia tuambie . Bunge litajadili hili suala na utakuwa na nafasi ya kutoa maoni yako. Usikimbilie mitandao ya kijamii kuwapoteza watanzania na acha kurukaruka na statements nyingi na kama umekuwa mwanasheria wa ACACIA tuambie.

Mheshimwa Spika naomba uwashauri hawa wabunge waache kujadili hili suala nje ya bunge kwani hili suala liko mikononi mwako.
 
Upinzani haujawahi kukwamisha juhudi zozote za serikali,ndani au nje ya bunge.kama wangekuwa na uwezo huo tusingekuwa na haya "masahihisho"ya makosa yaliyo kumbatiwa na CCM kwa miaka 20.Kama wanaweza kupitisha miswada ya hovyo kwa dharura tena bila kuzingatia akidi, sasa hivi watashindwa nini?.

CCM wana kila kitu cha kuwawezesha kufanya mambo yaende yawe mema au mabaya. Shida ni kuwa ccm huamua kuufuja uwingi wao bungeni na kuyafuja mamlaka ya kidola. Amini nakwambia Magufuli et-al anawahitaji akina Lissu na Zitto ili kuona upande wa pili. CCM wakiamuwa nani wa kuwazuia?????????...................
 
Hapo Kuna conflict of political interest ili kushika Dola.Kamwe wakina Tundu Lissu na timu yake hawataweza kumsupport Rais Dr John Magufuli.

Pole watakapokubali kumsupport tu maana yake hakuna sababu ya wao kuwa upinzani.
 
ukipelekwa mahakamani unaweza elezea namna anavyokwamishwa, au utabaki kama yule askari aliyeshikishwa ukuta Mahakamani
 
Kuna dalili tosha kwenye kambi ya upinzani wameanza kutoa taarifa za kupotosha hatua aliyechukua Rais Magufuli katika masuala ya madini.
Rais aliunda tume ya wasomi waliobobea na wao wakatoa mapendekezo kwa Rais na akalipeleka kwa Spika kwanini tuanze kumlaumu Rais kwa juhudi zote hizo.
Tundu Lissu acha kuwadangaya watanzania kama upo kwenye payroll ya Acacia tuambie . Bunge litajadili hili suala na utakuwa na nafasi ya kutoa maoni yako. Usikimbilie mitandao ya kijamii kuwapoteza watanzania na acha kurukaruka na statements nyingi na kama umekuwa mwanasheria wa Acacia tuambie.
Mheshimwa Spika naomba uwashauri hawa wabunge waache kujadili hili suala nje ya bunge kwani hili suala liko mikononi mwako.
lete porojo tu CCM wanajuhudi gani ikiwa miaka 55 hawakufanya juhudi wataweza leo ni siasa tu hizo hawana lolote waache wangojee 2020 waibe kura basi jengine silioni
 
Tundu Lissu acha kuwadangaya watanzania kama upo kwenye payroll ya Acacia tuambie . Bunge litajadili hili suala na utakuwa na nafasi ya kutoa maoni yako. Usikimbilie mitandao ya kijamii kuwapoteza watanzania na acha kurukaruka na statements nyingi na kama umekuwa mwanasheria wa Acacia tuambie.
Mheshimwa Spika naomba uwashauri hawa wabunge waache kujadili hili suala nje ya bunge kwani hili suala liko mikononi mwako.

si ungeomba namba yake tu ukampigia ukatoa hili povu?
 
Lissu na wapinzani ndio Wako sahihi na ndio wanaositahili kuitwa mashujaa,wakati wanapinga mikataba mibovu isipitishwe CCM walikuwa wanashangilia na kupiga vigeregere kwa kufanikiwa kupitisha mikataba ya wizi.

CCM na viongozi wake wanachokifanya hivi sasa ni kucheza mdundo wa ngoma uliopigwa na wapinzani hapo awali,wapinzani wanachokifanya sasa hivi ni kuikosoa serekali kwa kuionyesha matobo kuwa pamoja na kwamba mumeamua kucheza mdundo huu lakini mnatakiwa mzibe matobo haya na haya.

CCM kwa kuwa ni wakushangilia na kupigia makofi kila kitu wamesalia kusema kuwa wapinzani siyo wazalendo kwa kuwa wanapinga mazuri yanayofanywa Rais bila kujua kuwa mazuri haya ni ya wapinzani ambayo walikuwa wanataka serekali ifanye tangu awali.

CCM haijui kuwa pamoja na nia nzuri ya Rais lakini nia nzuri isipofanywa kwa akili na kwa tahadhari nayoinaweza ikakudhuru,nia njema haitofautiani na nia njema aliyo nayo dereva anayeendesha gari la abiri kwa speed kubwa nia yake huwa ni nzuri ya kutaka kuwafikisha abiria wake mapema lakini ndani ya nia njema hiyohiyo ya dereva kutaka kuwawahisha abiria wake asipokuwa na tahadhari anaweza akawaua abiria wake kwa speed kubwa.
 
Sasa kapotosha wapi nakati ile riport ya osoro ni ya 6 na zimeanza tokea 2002 na hazitekelezwi?
 
Upinzani wanadai wote waliohusika kuingia mikataba hii ya wizi wafikishwe mbele ya sheria, wanadai kinga ya marais iondolewe ili marais wastaafu waliotumia madaraka yao kuisaliti nchi wawajibishwe na wafilisiwe mali walizojipatia kwa ufisadi, wanadai mikataba yote mikubwa iliyoingiwa sirini iwekwe wazi na kupelekwa bungeni ili ijadiliwe na kurekebishwa na bunge, wanadai IFUATWE SHERIA na siyo kukurupuka ili makampuni yote yaliyokiuka mikataba kutuibia wafukuzwe na mali zao kutaifishwa.

Wanadai sheria ibadilishwe ili tabia ya watawala kujifungia na wawekezeji na kuwekeana mikataba ya kitapeli na kutuibia ikome.

Wanadai wahusika wote wa ufisadi kama IPTL yenye ESQROW, RICHMOND, LOLIONDO, LUGUMI, EPA, BOMBA LA GESI, BARABARA ZA CHINI YA KIWANGO, TWIGA KUPANDISHWA NDEGE, ule 'MTUMBWI' CHAKAVU nk wachukuliwe hatua.

Kama huko ndiko kukwamisha juhudi za magufuli bora waendelee kwa kweli.
 
Ni kweli kabisa maana
1. Upinzani Ndio ulikuwa unaongoza nchi wakati tulipoingia hii mikataba
2. Upinzani Ndio waliopitisha hii Mikataba kwa kusema Ndiooooo
3. Ofisi ya mwanasheria Mkuu ipo chini ya upinzani
4. Sera ya madini iliandaliwa na upinzani

Hongera kwa bandiko zuri
 
Hawatoweza lolote wacha mkuu apige kazi hongera sanaaa Rais wetu tuko pamoja nawe na MUNGU yuko pamoja nasi usikate tamaa kwani wanajitahidi kwa kila namna ili wakukwamishe lakini hawatoweza chochote na watajambaaaaaa
 
Wapinzani wanaposema ukweli CCM kwa uzuzu wao wanaona wanatumiwa. Haya matatizo kwenye sekta ya madini yalipigiwa kelele na hao wanaoitwa wapinzani kwa takribani miongo miwili sasa lakini serikali ya CCM na wabunge wake wakaamua kubeza, kudharau na hata kuwafukuza kwenye vikao vya bunge.

Leo Rais anapobeba jambo ambalo lilipigiwa kelele kwa zaidi ya miaka ishirini kwa staili ambayo inaonekana kuzalisha matitizo mengine na yeye akiwa kwenye kundi hilo lililokuwa linabeza na kudhihaki, iweje ajikite kwenye kuomba ama kulazimisha kushangiliwa badala ya kushirikisha hao walioliona tatizo tangu awali badala ya kuendelea kuwakebehi na hata kutoa maelekezo wafukuzwe kutoka kwenye vikao na yeye kuahidi kuwashughulikia kikamilifu???.

Agenda ya ccm na wabunge wake katika hili jambo ni nini hasa. Hivi tatizo kwenye sekta ya madini liko kwenye MAKINIKIA tu?. Kwa nini taarifa za hizo kamati hazigusii jambo lolote kuhusu MATOFALI YA DHAHABU yanayosafirishwa kila mwezi kutoka kwenye hiyo migodi. Je! ni kweli kuwa serikali inapata mapato halali kutokana na hayo MATOFALI YA DHAHABU na kuwa udanganyifu na wizi unafanywa kwenye MAKINIKIA tu?
 
Kuna dalili tosha kwenye kambi ya upinzani wameanza kutoa taarifa za kupotosha hatua aliyechukua Rais Magufuli katika masuala ya madini.

Rais aliunda tume ya wasomi waliobobea na wao wakatoa mapendekezo kwa Rais na akalipeleka kwa Spika kwanini tuanze kumlaumu Rais kwa juhudi zote hizo.

Tundu Lissu acha kuwadangaya watanzania kama upo kwenye payroll ya Acacia tuambie . Bunge litajadili hili suala na utakuwa na nafasi ya kutoa maoni yako. Usikimbilie mitandao ya kijamii kuwapoteza watanzania na acha kurukaruka na statements nyingi na kama umekuwa mwanasheria wa ACACIA tuambie.

Mheshimwa Spika naomba uwashauri hawa wabunge waache kujadili hili suala nje ya bunge kwani hili suala liko mikononi mwako.
Mkuu tatizo nia njema,serikali ikubali uhalisia,itende haki kwa wote,ndio kutapatikana mapenzi,na umoja wenye nguvu.
 
Back
Top Bottom