YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,908
- 51,904
Katika vitu ambavyo kwa utafiti nimevigundua ni kuwa viongozi wa upinzani hawajui namna ya kufanya kazi na viongozi wa serikali kwenye maeneo yao ili kuleta maendeleo eneo husika.Unakuta mtu kachaguliwa kuwa diwani,mbunge au meya anaota mapembe anajiona kama vile yeye ni raisi wa eneo husika na hana haja ya kushirikiana na kiongozi yeyote wa serikali kwa lolote awe wa wilaya,mji,jiji,mkoa ,wizara nk.
Hawaelewi kuwa hata ukipata pesa za msaada wa kufanya kitu katika eneo lazima ushirikishe serikali kwanza kabla ya kufanya huo mradi hata kama unataka kuufanya kwa pesa zako.MFANO MTU UKIWA meya umepewa pesa za msaada wa kujenga hospitali kubwa kama ya muhimbili na wafadhili huwezi ibuka tu ukasema mimi nina pesa zangu najenga sihitaji cha mkuu wa mkoa wala waziri wala nani.
Ukianza process waweza kataliwa na serikali kujenga hiyo hospitali yako.Sababu kubwa ni kuwa misaada nayo huratibiwa.Mfadhili akijenga hilo hospitali na kuweka kila kitu mbeleni nani atagharimia uendeshaji wa hiyo Hospitali? Lazima kieleweke sababu kama baadaye madaktari na gharama zote mradi ukikamilika serikali ndio itawajibika kugharimia
Ina maana huo msaada umekuja kuongeza matumizi ya serikali mbeleni wakati serikali haijajipanga kwenye hilo kwani matumizi kuongezeka ina maana serikali mbeleni itawajibika kuongeza kodi ili ipate pesa za kuendesha hilo hospitali koko la msaada lililokuja ghafla bila kuwekwa kwenye mipango ya maendeleo ya serikali.
Hata ukiwa na pesa za kujenga kituo cha polisi lazima uongee na serikali sababu ijipange kuajiri askari wapya kwa ajili ya hicho kituo na gharama zingine za uendeshaji mbeleni. Tatizo la viongozi wa upinzani waliochaguliwa wanadhani unaweza ishi bila serikali na shughuli zako zikaenda sio kweli kuna maeneo ukifika utakwama.
Wanatakiwa wajitahidi mno kutokuwa na BIFU na serikali.Iwe na polisi au kiongozi yeyote wa serikali kama kweli wamepania kuleta maendeleo kwenye maeneo yao.Kila wanachotaka kufanya washirikishe serikali kuanzia hatua za mwanzo kabisa ili viwekwe kwenye mipango ya maendeleo ya serikali.
Ushauri wangu kama hawajui jinsi ya kufanya kazi na serikali watafute washauri toka nchi zilizoendelea wawashauri.Na wanatakiwa wajue kuwa wamechaguliwa na watu wote sio wa vyama vyao tu.Hivyo wakati wa utumishi wao wasiweke jeuri ya vyama vyao mbele bali maslahi mapana ya walio wengi waliowachagua ambao wengi wao si wanachama wa vyama vyao